text
stringlengths
0
4.5k
Mambo mnayowafanyia wanawake mngefanyiwa ninyi ingekuwa vita...ila mkiwafanyia wanawake huwa mnaona n sawa tu mna haki ya kufanya hivo...huo n ubinafsi wa hali ya juu....mnaangalia sana tamaa zenu za mwili bila kujali upande wa pili
Tatizo lenu mnataka kujilinganisha na wanaume ndo shida yenu, mwanaume Ni kichwa na atabaki kuwa kichwa, mwanaume Ana wanawake wawili na wewe mwanamke unataka ushindane naye
Likes: Mtoto wa Baba
Mtoto wa Baba
Mwisho wa hiyo Vita wenyewe mnakuja kulia mwishoni, kwani Babu yako alikuwa Ana mke mmoja?
Yaan hakuna kulia tutakomaa had mwisho...mmeshajiwekea kwamba tutalia hayo n mawazo yenu....babu zangu wote walikuwa na wana mke mmoja mmoja hadi leo.
Nafikiri hamaanishi mke wa ndoa, anamaanisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke nje ya ndoa.
Kwa hiyo ni kweli, mwanaume ambaye hana uhusiano na mwanamke mwingine nje ya yule rasmi, inawezekana kwa kipindi fulani tu, sio maisha yake. Au akiwa hayuko vizuri kiuchumi, au akiwa kwenye matatizo mazito, au kwa kuogopa kitu fulani, mfano anatarajia kuomba/kugombea cheo cha kisiasa!
Ila kama kila kitu kiko sawa, lazima atakuwa na mchepuko tu!
Kwa hiyo biblia inasema Mungu alihalalisha wanaume kuendekeza tamaa? Halafu hao unaowarefer n wanaume wenye tamaa kama ninyi tu ...ila sidhani kama Mungu alikuwa anapendezwa na maisha yao ya kuwa na wanawake wengi
Arsenal yatamba baada ya kutwaa Ngao ya Jamii - M-MEDIA Tz
Klabu ya Arsenal jana ilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuishinda Chelsea kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamnii uliopigwa katika uwanja wa Wembley.
Arsenal ilipata ushindi huo baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea ambao walikuwa wa kwanza kupata bao la kuondoza dakika 46 likifungwa na Victor Moses lakini Arsenal walisawazisha kupitia kwa mchezaji aliyesajiliwa karibuni kutoka klabu ya Shalke ya Ujerumani Sead Kolasinac dakika ya 82.
Leo ni siku ya tatu kuanzia Harmonize na mpenzi wake Wolper waanze kuposti picha wakiwa mtwara kwa wazazi wa harmonize. I am h...
TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA
Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinga...
PICHA 20: Kutoka kwenye msiba wa Ivan Don, Kampala Uganda
wakati watanzania wakijiuliza chanzo cha kukithiri mauwaji ya watu kuchinjwa ,kumetokea tukio lingine ,baada ya watu wanane wa familia ...
KWA wanaofuatilia kwa karibu suala la uvamizi wa kisiwa cha Anjouan, Comoro bila ya shaka watakuwa wameisikia taarifa ya redio ya Marekani (Voice of America) iliyoonyesha jinsi Tanzania inavyojiimarisha kama nchi yenye nguvu na ushawishi mkubwa katika eneo hili la Afrika.
Jumatatu iliyopita, redio hiyo ilionyesha namna rais Jakaya Kikwete anavyopanda chati katika eneo hili la Pembe ya Afrika. Kuchaguliwa kwake Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) mapema mwaka huu kuliashiria hilo.
Tayari majeshi hayo yamekirejesha kisiwa hicho chini ya himaya ya serikali ya muungano wa Comoro.
Wapo waliopinga matumizi ya kijeshi. Hawa ni pamoja na Afrika Kusini. Binafsi, naunga mkono mtazamo huu, kutokana na ukweli kuwa daima nguvu za kijeshi hazileti mafanikio ya kudumu.
Kiongozi wa kisiasa na wa ki-imani wa India, aliyeshiriki katika kuleta uhuru kwao miaka ya 1940 aliwahi kusema: “Napinga utumiaji nguvu kwa azma yoyote ile, kwa sababu iwapo nguvu itaonekana kuleta mafanikio, basi mafanikio hayo ni ya muda tu, lakini uovu utakaofuatia ni wa kudumu.”
Kwa upande mwingine, utumiaji wa nguvu hautokani na maamuzi huru. Inajulikana wazi kuwa AU haina uwezo wa kifedha kugharamia harakati za kijeshi.
Kwa mfano, tunaambiwa vifaa na sehemu kubwa ya fedha zilizogharamia uvamizi wa Anjouan, zilitolewa na Ufaransa. Kidogo tu ndio walitoa nchi wanachama wa AU ikiwamo Libya.
Ufaransa imekuwa inajiingiza katika migogoro ya Comoro mara kwa mara tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1975. Hadi sasa, Ufaransa inakishikilia kisiwa cha Mayotte.
Wakazi wa kisiwa hiki, walipiga kura na wakaamua kubakia chini ya Wafaransa, koloni la zamani la Comoro, ingawa serikali huru ya Comoro na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), uliapa kukikomboa.
Hadi leo hii, si kwa njia ya kijeshi, wala ya mazungumzo, bado Mayotte haijakombolewa. Si Kikwete wala kiongozi mwingine yeyote aliyethubutu angalau kutamka neno “kupeleka jeshi Mayotte” ili kuiondoa Ufaransa katika ardhi ya Afrika.
Kwa hakika, nchi nyingi zilizopata uhuru barani Afrika, pamoja na utajiri lililonao bara hili, bado wananchi wake wanasumbuliwa na umasikini mkubwa. Hiyo inatokana na viongozi wengi kujilimbikizia mali. Pengine hilo ndilo lililowafanya wananchi wa Mayotte kuamua kubakia chini ya ukoloni.
Kutokana na hali hiyo, anaonekana kama anatumiwa tu na nchi za Magharibi kwa maslahi yao. Inampasa aangalie vizuri kabla ya kuadhirika kama ilivyomtokezea Mobutu Sese Seko wa iliyokuwa Zaire.
Maana hebu fikiria. Je, iwapo Ufaransa isingegharamia uvamizi wa Anjouan, Kikwete angekuwa na ubavu wa kung’ang’ania uvamizi? Hapa pia kuna suala la undumila kuwili katika kufanya maamuzi.
Kuna utata kuhusu mgogoro wa Darfur, kwani AU inashikilia kupeleka majeshi ya kulinda amani. Amani gani inayolindwa wakati makundi mbalimbali yangali yanapigana na serikali ya Khartoum na hayataki kusaini mkataba wa amani?
Rais Hassan Al-Bashir hakubali kufuata masharti ya Marekani kwa hivyo Marekani inawaona waasi wa Darfur ni halali na kwamba wana haki ya kupigana na serikali ya Khartoum.
Na katika kutimiza azma yao, akina George W. Bush wamebuni fitina mbaya zaidi, kwamba majeshi ya serikali ya Khartoum yanafanya mauaji makubwa jimboni Darfur yanayofanana na yale ya kimbari au yale ya Bosnia.
Kwa kuwa na ushawishi mkubwa wa maamuzi kwenye Umoja wa Mataifa (UN), hasahasa Baraza la Usalama, Marekani imefanikiwa kushinikiza vikwazo dhidi ya Sudan.
Inadai kwamba nchi hiyo inafanya “mauaji kwa raia wake Darfur.” Maazimio hayo hayataji kabisa “mauaji ya kimbari.”
Hii ni tofauti na nchi nyingine kama vile Chad au DRC, ambako Marekani huona ni halali majeshi ya serikali kupigana na waasi.
Tanzania pia imekubali kutuma vikosi kulinda amani Darfur, na bila ya shaka hili lilizungumzwa wakati Bush alipozuru Tanzania Februari mwaka huu, na kufanya mazungumo ya faragha.
Wakati Kikwete na Bush wanatia saini mkataba wa kuipatia Tanzania msaada wa dola 700 milioni za Marekani, baadhi ya wachunguzi wa mambo walisema fedha hizo zina jambo, maana haijatokea Marekani ikatoa fedha nyingi bila ya kuweka akiba kwa ajili ya maslahi yake baadaye. Ingali mapema kuanza kuvitambua vitakavyokuja?
HALI YA HEWA
KAMERA YA MTAA KWA MTAA
KANDA YA ZIWA
KUPATWA KWA JUA
MAKAMU WA RAIS
MIFUKO YA JAMII
MTAA KWA MTAA TV
UMOJA WA TAIFA
WAZIRI MKUU
Serikali ya Jamuhuri ya Cuba imetiliana Saini Mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.
Madaktari hao 15 ambao Wanane wa Mwanzo wataanza Mafunzo yao Mwezi ujao wakifuatiwa na wengine 7 wa awamu ya Pili ni Miongoni mwa Wanafunzi waliomaliza masomo yao kupitia mpango wa masomo ulioasisiwa kati ya Serikali ya Cuba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Saini ya Mkataba huo kwa Serikali ya Cuba imewekwa na Balozi wa Nchi hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernades na kwa upande wa Zanzibar Saini ikatiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum.
Hafla hiyo fupi ya Kihistoria imeshuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyejumuika pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Wizara husika, Watendaji wa Wizara hizo na kufanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernades alisema Cuba bado inaendelea kutafakari maeneo mapya zaidi inayoweza kushirikiana na Zanzibar katika kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi za Kiuchumi na Maendeleo.
Balozi Lucas alisema suala la kuwafanya Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba wanakuwa katika ustawi ulio bora zaidi wa afya na kipato limepewa kipaumbele na Serikali ya Cuba kuliko jambo jengine lolote la ushirikiano wa pande hizo mbili.
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania alielezea faraja yake kutokana na ukarimu anaoushuhudia wa Watu wa Zanzibar kwa wageni jambo ambalo limempa nguvu na ari zaidi ya kuona jinsi gani anaweza kuitumia fani yake ya Diplomasia katika kudumisha udugu wa pande hizo mbili.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mkataba huo wa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar Nchini Cuba umejenga historia mpya ya ushirikiano kati ya Zanzibar na Cuba katika Sekta ya Afya kuelekea mfumo wa kisasa wa Sayansi na Teknolojia Ulimwenguni.
Balozi Seif aliishukuru na kuipongeza Jamuhuri ya Cuba kupitia Balozi wake Nchini Tanzania kwa ukarimu wake wa kupungua kima cha malipo kwa Wanafunzi hao wa Fani ya Udaktari katika ngazi ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Balozi Lucas Domingo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanmzania zitaendelea kuupa ushirikiana ubalozi huo ili uendelee kutekeleza vyema majukumu yake ya Kidiplomasia.
Mapema Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo alisema uhusiano wa Sekta ya Afya kati ya Zanzibar na Cuba umeanza kupata baraka zaidi kufuatia Ziara ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar aliyoifanya Nchini Cuba Mnamo Mwaka 2008.
Waziri Mahmoud alifahamisha kwamba mafunzo hayo yamekuwa yakiendelea kwa makundi mengine ya Udaktari kila Mwaka ambapo mfumo uliopo hivi sasa kwa mafunzo hayo umejumuishwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA}.
Alisema ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Jamuhuri ya Cuba na Zanzibar umeasisiwa Mnamo Mwaka 1964, Cuba ikiwa ni miongoni mwa Mataifa Matano ya Kwanza yaliyoitambua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Jamuhuri ya Cuba kupitia Balozi wake Nchini Tanzania katika Mkataba huo uliowekwa saini imeridhia kupungua kima cha malipo kwa kila Mwanafunzi katika Kundi hilo la Madaktari 15 Wazalendo wa Zanzibar katika ngazi ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakisaini Mkataba wa Usomeshwaji wa Madaktari Wazalendo 15 wa Zanzibar Nchini Cuba katika Fani ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.Nyuma yao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na aliye simama mbele yao ni msaidizi wa Balozi wa Cuba Meylin Suarez.
Profesa Lucas Domingo Kushoto na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bibi Halima Maulid Salum wakibadilishana nyaraka za Mikataba mara baada ya kusaini.
Balozi Lucas Domingo akizungumza kabla ya utiaji saini kwenye Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimwa Mahmoud Thabit Kombo.
Balozi Lucas Domingo Kushoto akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya utiaji saini mkataba wa usomeshwaji wa Madaktari wa Zanzibar Nchini Cuba.
Balozi Lucas Domingo Kushoto akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Moh’d Aboud Moh’d.
Nyuma na Mheshimiwa Moh’d Aboud ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Idriss Muslim Hijja.
Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo Kushoto akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Kulia na Msaidizi wake Bibi Meylin Suarez pamoja na Mtoto wake. Picha na – OMPR – ZNZ.
[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]
MKAKATI MPYA WA KITAIFA WA KUPANDA NA KUTUNZA MITI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mbarak Abdulwakil (kushoto) akifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya M...
PICHA ZA MECHI YA SIMBA NA YANGA INAYOCHEZWA MUDA HUU UWANJA WA TAIFA, JIJINI DAR
Zoezi la uokoaji kwa wanafunzi hao likiendelea. Zoezi la uokoaji likiendelea. Majina ya Baadhi ya wanafunzi waliotambulika...
MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MZEE KINGUNGE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba wa...
MKUU WA WILAYA YA HAI ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOWE
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai katika lango la kuingilia katika shamba la Kil...
ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAFANYA UKAGUZI MABASI WA KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO
UJUMBE WA RAIS MSTAAFU MZEE BENJAMINI WILLIAM MKAPA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata ,Sheikh Khamis Said akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam...
ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE: ZAIDI YA WANAFUNZI 20 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI HUKO KARATU ASUBUHI HII
Taarifa iliyotufikia hivi punde, kuna ajali imetokea muda huu katika eneo la Rhotia Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, iliyohusisha Basi li...
Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa ambayo maendeleo ya kielimu bado yako chini sana (kuna vyuo viwili tu vya ualimu na hakuna shule nyingi - hata zilizopo ufanisi wake ni mdogo ukilinganisha na mikoa mingine).
Kwa kuguswa na suala la hilo na nikiwa pia ni mwenyeji wa huko nimeazimia kutoa huduma hiyo mimi mwenyewe (japo vijisenti havitoshi kuwekeza katika mradi huo), hivyo najipanga ili nianzishe shule yangu itakayokuwa na 3-WINGS: Shule ya Msingi (English Medium), High School (Sayansi na Biashara) na Chuo cha Ualimu (kwa ajili ya Diploma na Grade A) hususani katika maeneo ya vijijini.
Kwa hivi sasa nimeomba kuuziwa ardhi kijijini kwetu mkoani Kigoma na serikali ya kijiji na wananchi wenyewe wameafiki sana mradi huo na wako tayari kuniuzia sehemu ya ardhi kijijini hapo (eka 150) na wangependa ujenzi wa shule hizo ukamilike mapema ili watoto wao wasome.
Pamoja na kufanya biashara, malengo yangu ni kuanzisha mfumo wa kipekee katika katika kutoa elimu, mfumo ambao utawawezesha wazazi/wanafunzi kulipa ada nafuu na hivyo kuwa msaada wa maana sana kwa watoto kutoka familia maskini kwani wengi hawasomi shule nzuri za private kutokana na kukosa uwezo kifedha. Hivyo nikifanikiwa kujenga shule hizo nakusudia kuanzisha mfumo wa Learning by Doing and Earning.
Katika mfumo huo pamoja na kusoma masomo ya kawaida kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaifa wanafunzi watafundishwa pia stadi za ujasiriamali na kuanza kuzalisha bidhaa (kilimo, ufugaji, ufundi nk) wakiwa bado ni wanafunzi na kuuza bidhaa hizo hapo hapo shuleni na hata nje ya shule. Kwa hiyo mwanafunzi ataweza hata kujilipia ada yeye mwenyewe bila msaada wa mzazi - na inawezekana.
Wana JF, naombeni mnipe habari kuhusu mashirika au hata watu binafsi wanaoweza KUFADHILI mradi wangu kwa hatua za awali ili kukamilisha walau madarasa 3-5 ya kuanzia. Nimeulizia maswala ya mikopo naona suala hilo linawezekana kama tayari mradi unafanya kazi (operational) na siyo kuanzisha.
Kwa kutegemea hela yangu mwenyewe inaweza kuchukua muda mrefu kidogo kukamilisha ujenzi huo.
hizo n habari njema kwa wakazi wa kigoma na vijiji vyake. ni wazo zuri sana, kilichobaki asa, jitaidi sana angalau ujenge hata madarasa mawili na ofisi za walimu t...
habari,vipi ndugu,ulifanikiwa kutimiza lengo lako la kuanzisha shule?
Karatasi ya kupigia kura-ni siri?
kabla ya mtihani wa kumaliza shule huwa kuna Mock exams,hii inamuandaa mwanafunzi kujua mtiahani utafananaje etc,pia kuna past papers,hii pia inajenga uzoefu wa mazingira.