content
stringlengths 1k
24.2k
| category
stringclasses 6
values |
---|---|
Hatua hiyo imeelezwa ni moja ya sababu ya kushindwa kufikia malengo ya kujikwamua na lindi la umasikini.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema aliyewakilishwa na Ofisa Elimu Sekondari, Benjamini Sipetro aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Airtel katika kijiji cha Nyakasungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza utakaohudumia zaidi ya vijiji saba.“Naamini mawasiliano ya uhakika yatamfanya mkulima kutumia teknolojia inayomzunguka kufanya biashara na kupata masoko ya mazao yao na malipo kupitia huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma ya Airtel Money,” alisema.Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya Airtel Kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael alisema” Tunajisikia furaha kusogeza huduma za mawasiliano ya simu ya uhakika kwa wakazi wa Sengerema na Geita, na maeneo ya pembezoni ya nchi.”Wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie amekabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule ya sekondari ya Nyakusungwa vilivyotolewa na Airtel kuwawezesha wanafunzi wa maeneo hayo kupata nyenzo muhimu katika kuboresha elimu. | uchumi |
Kutokana na hatua hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeelezea kuridhishwa hatua hiyo, huku Mwenyekiti wake, Michael Mwanda akisema sasa ataanza kupata usingizi.Kuthibitika kuanza kwa majaribio hayo mwezi ujao kumeelezwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya TPDC, Kampuni ya Gesi ya Taifa (GASCO), Kapuulya Musomba wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya TPDC waliokagua maendeleo ya ujenzi huo mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.Walikagua vya kupokelea gesi Kinyerezi na Tegeta, Dar es Salaam, vituo vya udhibiti wa usalama wa miundombinu ya bomba vilivyojengwa kuanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kwa umbali wa kilometa 30, kituo cha kupokea gesi cha Somanga Fungu wilayani Kilwa, MnaziBay mkoani Mtwara inakopatikana gesi na pia kijiji cha Madimba, Mtwara unakojengwa mtambo wa kuchakata gesi.Akizungumzia maendeleo ya mradi huko, Musomba alisema unakwenda vizuri na kwamba kwa hatua iliyofikiwa, sasa majaribio yanaweza kuanza mwezi ujao.“Pamoja na changamoto kadhaa, naweza kusema tumefika pazuri na wakati wowote mwezi ujao majaribio ya kusafirisha gesi yanaweza kuanza…nia yetu ni kuhakikisha kama ilivyokuwa imepangwa, Juni mwaka huu tuwe tumekabidhi mradi kwa serikali,” alisema Musomba.Kutokana na kauli hiyo ya msimamizi mkuu wa mradi, Mwanda alisema kutokana na kazi hiyo mradi huo utakamilika kama ulivyopangwa Juni, mwaka huu. Maelezo hayo yalimkuna Mwanda na kusema: “Tujaribu kuwaeleza wananchi juu ya maendeleo ya mradi, kwamba unakwenda vizuri." | uchumi |
WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo Hamisi Kilomoni kwenye Kamati ya Midhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, achukuliwe hatua kwa kosa la kutumia kivuli cha udhamini kudhoofisha brand ya timu hiyo, suala hilo limemuibua mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Ismail Rage.Rage amezishauri pande zote mbili kukutana na kumaliza tofauti zao na sio kuendelea kubishana kwenye vyombo vya habari, jambo ambalo si muharobaini wa kumaliza sintofahamu hiyo inayoendelea kila siku.Ni muda mrefu sasa Simba imekuwa ikitunishiana misuli na Kilomoni jambo lilofanya uongozi wa wekundu hao kutoka hadharani na barua kutoka serikalini iliyoweka bayana kwamba Kilomoni sio mdhamini.Akizungumza jana Rage alisema viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu Kilomoni ameitumikia timu hiyo toka inaitwa Sunderland si mtu mdogo wanapaswa kumuita kuongea naye.“Sidhani kama kuendelea kubishana kila siku kwenye vyombo vya habari kunaweza kuleta suluhisho ni vyema uongozi wa Simba ukubali kukutana kuyajenga masuala haya kwa busara, “ amesema Rage.Amesema Kilomoni hapaswi kujibiwa na Magori, kwa kuwa Magori ni mwajiriwa analipwa mshahara kama wafanyakazi wengine kinachotakiwa viongozi wa bodi wafanye mchakato wa kukutana kuweza kumaliza jambo hili.“Unajua Kilomoni anachokidai ni cha msingi kabisa kutaka mwekezaji aweke kiasi cha bilioni 20 kwenye akaunti ndipo wapatiwe hati sasa tatizo liko wapi anachokidai ni sahihi wanatakiwa kufanya hivyo asikilizwe wayamalize,“ amesema Rage. | michezo |
MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) inatarajia kutumia takribani Sh bilioni 26.5 kwa ajili ya kufi kisha huduma za mawasiliano katika kata 214 zenye vijiji 521.Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo yanayofanyika jijini hapa kwenye viwanja vya Nyerere. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Peter Ulanga na kuongeza kuwa ifikapo Mei mwaka huu watatangaza zabuni ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata na vijiji hivyo ambapo utekelezaji utaanza mara moja baada ya tathmini kukamilika mwishoni mwa Juni.“Bado kuna maeneo ambayo hayana huduma za mawasiliano ambapo mfuko huo umejikita kuhakikisha yanapata huduma muhimu na Mei mwaka huu mfuko utatangaza zabuni ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 214, zenye vijiji 521,”alisema. Alisema serikali itatenga fedha kwa ajili ya maandalizi ya zabuni nyingine yenye vijiji zaidi ya 500 itakayotangazwa katika mwaka wa fedha 2019/20 kwa gharama ya Sh bilioni 26.Akizungumzia mafanikio ya ndani ya kipindi cha miaka 10 ya mfuko, Ulanga alisema Sh bilioni 118 zimetumika kufikisha mawasiliano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009. Alisema serikali kupitia mfuko huo imeshafikisha huduma za mawasiliano katika kata 703, zenye vijiji 2,501 na wakazi zaidi ya milioni tano kote nchini.Ulanga alisema mchango huo wa serikali ni wastani wa asilimia 26 ya gharama za ujenzi na uendeshaji wakati watoa huduma wamechangia asilimia 74 kufanikisha uwekezaji huo. Alisema tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kushirikiana na wadau mbalimbali wa mawasiliano nchini, kushirikisha wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano.“Wakati mfuko huu unaanza takribani asilimia 45 tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yaliyofikiwa na mawasiliano ya simu, mpaka tunavyoongea takribani asilimia 94 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu, ambapo zaidi ya asilimia 70 ni watumiaji wa huduma hizo huku asilimia 10 imechangiwa na mfuko,”alisema.Aidha, Ulanga alisema hadi sasa mfuko umepeleka vifaa vya Tehama katika shule zaidi ya 500 ambapo kila shule ilipata kompyuta tano na printa moja kwa wastani. Akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofikia kilele chake Aprili 30 mwaka huu yakiwa na kauli mbiu ya ‘Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati’, Ulanga alisema yatakwenda sambamba na uzinduzi wa Klabu za Tehama katika Shule za Sekondari za Dodoma na Msalato. “Mfuko pia utagawa kompyuta kwa Wilaya ya Gairo pamoja na kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilaya ya Bahi ikiwa ni kielelezo cha miradi ambayo inatekelezwa maeneo mengi nchini Tanzania Bara na Visiwani,”alisema. | kitaifa |
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile amesema wana mpango wa kuhamishia kambi ya upimaji virusi vya ukimwi kwenye viwanja vya michezo ili kuhamasisha wanaume kujitokeza kupima. Akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kutembelea maonesho ya Utamaduni ya Jamafest, Dk Ndungulile alisema sababu kubwa ya kutaka kuhamishia kambi viwanjani ni baada ya kugundua wanaume wengi wanakwepa kupima, huku baadhi yao wakionekana kufa zaidi kwa kutozingatia maelekezo.“Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza kuliko wanaume, tumeona twende kwenye makambi kuwafuata na mojawapo ni viwanja vya michezo ili kutoa elimu ya upimaji kwao,”alisema. Alisema hata kwa baadhi wanaokutwa na maambukizi huchelewa kuanza dawa za kuua makali jambo ambalo limechangia baadhi kufa mapema huku akiwahimiza kuuona ugonjwa huo wa kawaida kama yalivyo mengine.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema ujio wake katika tamasha hilo una mahusiano makubwa na Utamaduni kwasababu wamekuwa wakifanya kazi n’a wasanii mbalimbali kufikisha jumbe za afya. “Michezo, sanaa na Utamaduni yana mahusiano tumekuwa tukifanya nao kazi, lakini pia ningependa kuona wasanii wanaibua mada mbalimbali za afya kwa mfano masuala ya lishe na mambo mengine tuweze kuyafanyia kazi,”alisema. Alizungumzia Jamafest alisema ameona kazi nyingine nzuri na kuona kuna bidhaa nyingi ambazo zinauzwa kuuzwa nje na kuwapongeza wizara ya Habari na Maliasili na utalii kwa maandalizi mazuri. Alisema tamasha lijalo wawashirikishe wawe pamoja kwani kuna mambo mengi yanahitaji kuzungumziwa kwa ushirikiano na wasanii. | michezo |
SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kutangaza kuwavua nyadhifa zao makamanda wa polisi wa mikoa mitatu kwa sababu tofauti, zikiwemo kukaidi agizo la kutokomeza rushwa na kulinda wauzaji wa dawa za kulevya na biashara ya magendo, imebainika baadhi yao bado wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.Juzi Waziri Lugola aliwataja makamanda waliopoteza nyadhifa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lakula na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Ramadhan Nganzi.Pamoja na uamuzi huo, Waziri Lugola alimtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (Trafiki) nchini, Fortunatus Muslim, kujitafakari na kujipima kama anatosha katika nafasi yake. Hata hivyo, jana baadhi ya makamanda hao walipoulizwa walisema wanaendelea na kazi.Muslim na ‘Operesheni Nyakua’ Kamanda Muslim alisema hana taarifa kuwa ameambiwa na Waziri Lugola, ajitathmini na kujipima kama anatosha katika nafasi yake hiyo. Alipoulizwa saa sita mchana jana kuhusu agizo hilo, Kamanda Muslim alisema hajui lolote kuhusu agizo la Waziri na kuanza kumuuliza mwandishi wa habari hii lini agizo limetolewa.“Alisema kuna nini? Hebu niambie maana mimi nipo huku mikoani kwenye operesheni, sina taarifa kama nimetakiwa kujitathimini wala kujipima … hebu niambie nini kimetokea?” Alisema anaendelea na operesheni, kuhamasisha vita dhidi ya wavunjifu wa usalama barabarani, huku akielezea kuwapo kwa maendeleo mazuri ya Operesheni hiyo maarufu kama “Nyakua”.“Yani hadi sasa sina hizo taarifa, ila labda pengine kwa baadaye, ila sasa sijui lolote kuhusiana na hilo ndugu mwandishi,” alisema. Hamduni aendelea kuchapa kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Hamduni ambaye naye alitajwa na Waziri Lugola kuvuliwa wadhifa wake, jana alibainika kuendelea na majukumu yake kama kawaida.Wakati gazeti hili lilipokuwa linafuatilia tukio la kuzuka kwa moto katika majengo ya Seminari ya Segerea wilayani Ilala, liliwasiliana na Kamanda huyo na akapokea simu, akieleza kutokea kwa tukio hilo na alipohojiwa wadhifa wake, alijitaja kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wa Kipolisi wa Ilala.Maoni ya wadau Baadhi ya wadau waliozungumza na gazeti hili, walieleza kuwepo kwa ukakasi wa kisheria kutokana na Waziri Lugola kuwavua nyadhifa zao makamanda hao, badala ya kuacha suala hilo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro.Akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo, Wakili Jebra Kambole alisema Sheria ya Jeshi la Polisi Sura Namba 322 iliyorejewa Mwaka 2002, ndiyo inatoa Mamlaka ya Waziri na IGP ambapo Kifungu cha 7(1) cha sheria hiyo kinampa Waziri uwezo wa kumpa IGP, maelekezo na miongozo mbalimbali kisera.Alisema Kifungu cha 7(2) cha sheria hiyo, kinampa mamlaka IGP uwezo wa kupanga maofisa na kuwapandisha na kuwashusha vyeo. “Japo sheria pia inampa uwezo waziri kutoa maelekezo kwa IGP juu ya utendaji kazi huo, kifungu hicho cha sheria kimetumia neno “May” ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri Tanzania Kifungu cha 53 Sura Namba 1 ya Sheria za Tanzania Kama ilivyorejewa 2002, ‘May’ lina maana hiari, sio sharti la lazima.“Hivyo Waziri hana mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao, bali kumpa maelekezo mwenye mamlaka afanye hivyo, ambaye ni IGP ambaye naye si lazima atende alivyoambiwa, bali anatumia akili yake na mamlaka yake kuamua…hafanyi kama kasuku.Kwa maoni yangu haikuwa sahihi Waziri kuwatimua wakuu hao kwa mujibu wa sheria,” alisema Kambole. | kitaifa |
Wafanyabiashara hao, walifanya ziara kwenda kujionea fursa mbalimbali za kibiashara katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kuwa wa viwanda na biashara.“Serikali imetenga eneo la hekari 22,000 sawa na hekta 9,000 katika eneo hili maalumu la uwekezaji hapa Bagamoyo, na tunahamasisha wawekezaji wakiwemo wa mji wa Vallejo kuja kuwekeza hapa,” alielezea ujumbe huo ambao umeongozwa na Meya wa Vallejo, Osby Davis.Zawadia alisema kwa sasa Serikali inayo mipango ya kujenga miundombinu mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi, hivyo wafanyabiashara hawanabudi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanzisha viwanda na biashara na huduma mbalimbali.“ Mji wa Bagamoyo kutokana na kuwa eneo maalumu la uwekezaji, kutajengwa Bandari kubwa ya kisasa kupita zote nchini ili kuunganisha na maeneo mengine ya nchi na nje ya nchi,” alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa Bagamoyo itakuwa kiungo kikubwa kwa biashara nchini.Mbali na bandari, Zawadia alisema kuna mradi mwingine wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa na reli itakayounganishwa na Reli ya Kati na Tazara na miundombinu yote hiyo, inalenga kuweka mazingira bora ya kibiashara na uwekezaji.Ugeni huo wa wafanyabiashara hao kutoka mji wa Vallejo, walitembelea maeneo hayo ya uwekezaji, likiwemo eneo la hekta 300 la Kamal Industrial Estate, linalomilikiwa na mtu binafsi.“ Ujumbe wa wafanyabiashara hawa wengi wao wamefurahishwa na Serikali ya Tanzania kutenga maeneo hayo kwa ajili ya viwanda na biashara,” aliongeza mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa wako tayari kuja nchini kuitumia fursa waliyoiona Bagamoyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi mbili.Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Weusi wa Mji wa Vallejo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Carl Davis Jr alisema wao wanahitaji kufanya biashara katika mji wa Bagamoyo kwa faida ya miji hiyo miwili. | uchumi |
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga Clement Sanga ajiuzulu.Ametangaza uamuzi huo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam."Na ninajiuzulu kwa masikitiko kwa sababu pia naamini bado na kipindi kingine cha kuitumikia Yanga mpaka 2020 aah kwa mujibu wa Katiba yetu lakini kilichonipelekea kufanya hivyo ni namna ambavyo sehemu ya utamaduni mpya ambao unaanza kujitokeza" amesema.Kwa mujibu wa Sanga, ameamua kujiuzulu kwa kuwa yeye na familia yake wametishiwa usalama."Siku ya Ijumaa iliyopita nimeona clip mbalimbali zinatembea kwenye mtandao lakini clip hizi, zipo nyingi za kubeza za kufanya nini hizo sio shida sana kwa sababu ndiyo dhamana ambayo tumepewa na unaongoza watu wenye tabia tofauti lakini shutuma zimekuja, zimefikia kwenye clip inayotembea inaelezea kwa uwazi kabisa kwamba, inahamasisha watu mbalimbali kuja nyumbani kwangu na mapanga, na majembe, na shoka, aah sasa mimi nikafikiria huku mimi nina shamba ninapoishi kiasi kwamba wanataka kuja kulima au kuna nini" amesema Sanga."Hizi ndio tuhuma pekee nzito katika maisha yangu kuzisikia zinaelekezwa kwa kiongozi wa mpira wa miguu kwamba watu kuhamasishana kuna na mapanga kwenye nyumba ya mtu anapoishi, unatafuta sababu huwezi kuielewa"amesema.Sanga ameiongoza Yanga tangu Yusuph Manji alipojiuzulu uenyekiti. | michezo |
BARAZA la Chuo Kikuu Mzumbe limeiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kushughulikia tatizo la ukosefu wa takwimu sahihi za wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu zinazoonesha mwenendo wa ajira, kuajiriwa katika sekta ya umma na binafsi ili kubaini ukubwa wa changamoto ya ajira na kusaidia kuwa na mipango maalumu.Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga (pichani) alisema hayo hivi karibuni kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta kuwatunuku wahitimu Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Umahiri, Shahada ya Kwanza, Stashahada na Astashahada kwenye Mahafali ya 17 mjini hapa.Profesa Luhanga alisema changamoto kubwa ya Chuo Kikuu Mzumbe ni uhaba wa ajira kwa wahitimu ambayo ni pamoja na kwa vyuo vikuu vingine nchini, licha ya baadhi ya wahitimu kujiajiri wenyewe.Pia alisema changamoto hizo hazijapewa kipaumbele kutokana na kutokuwa na tawimu sahihi ya idadi wanaohitimu vyuo vikuu na hawafahamiki ni asilimia ngapi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaajiriwa kuwa kazini, kazi zipi pamoja na takwimu za walio katika ajira za sekta binafsi.Alitumia fursa hiyo kuiomba TCU yenye jukumu la kufanya tathimini na kutangaza takwimu sahihi za ukusanyaji wa ajira wa wahitimu wa elimu ya juu kuja na majawabu hayo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili hatimaye changamoto zitakazojitokeza zifanyiwe kazi na mamlaka zinazohusika.Makamu wa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Lughano Kusiluka aliishukuru serikali kwa kukiwezesha kupatiwa fedha kiasi cha Sh bilioni 6.5 kwa ajili ya kujenga hosteli za kisasa kulaza wanafunzi.Katika mahafali hayo, wanachuo 2,233 kati yao watatu wa Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Kampasi Kuu Mzumbe walitunukiwa shahada zao, ambapo wahitimu wa mwaka huu kwa kampasi zote tatu za Chuo Kikuu hicho ni 3,724, wanawake wakiwa ni asilimia 49.5 na wanaume ni asilimia 50.5. | kitaifa |
Hii ni mra ya kwanza kwa Wakenya kutamba katika mbio hizi, ambazo mwaka huu zilianzishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala, ambapo mwaka jana nafasi tatu za mwanzo zilishikwa na Watanzania.Mshindi wa kwanza kwa wanaume katika mbio hizo za mwaka huu alikuwa Mkenya, Joseph Mbata kwa kutumia saa 1:04.54.12 akifuatiwa na Mkenya mwenzake, Benard Mussa aliyetumia muda wa saa 1:05:09.59 Wakati Mtanzania wa kwanza ni Pascal Mombo aliyeshika nafasi ya tatu kwa saa 1:06:05.71.Kwa upande wa wanawake, Wakenya waliendelea kutamba baada ya mwanariadha wake, Monica Cheruto kumaliza wa kwanza kwa kutumia saa 1:15:07 huku Mtanzania Failuna Abdul alimaliza wa pili kwa saa 1:15:20. Failuna alikuwa miongoni mwa wanariadha wa Tanzania walioshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Gold Coast, Australia iliyomalizika Aprili 15.Hakufanya vizuri katika mbio za meta 5,000 na 10,000.Kwa upande wa kilometa tano, mkimbiaji wa siku nyingi wa Tanzania, Mary Naali (Arusha) alimaliza wa kwanza kwa upande wa wanawake alipotumia dakika 17:40.65 wakati mshindi wa pili ni Rozalia Fabiani alitumia dakika 17:55.56 (JKT) wakati wa tatu ni Anastazia Mkama wa Mara alitumia dakika 18:01.40 .Katika mbio za kilometa tano kwa wanaume mshindi wa kwanza ni Elibariki Buko wa JKT alitumia dakika 14:14.81 huku mshindi wa pili ni Marco Sylvester wa JKT alitumia dakika 14:14,86.Kwa mwaka jana katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake washindi wa kwanza wa mbio hizo zinazodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alikuwa Faraja Lazaro wa JKT na Failuna Abdi wa Talent Club ya Arusha, ambao walishinda mbio hizo kwa kutumia saa 1:03.42 na 1:03.52.Mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wanaume na wanawake, kila mmoja mwaka huu ameondoka na Sh milioni 1 wakati mshindi wa pili amebeba Sh 500,00 huku wa tatu Sh 250,000, mshindi wa nne Sh 100,000 na watano Sh 80,000.Mbio hizo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 700 kutoka ndani na nje ya Tanzania. Mbali na mbio za kilometa 21 na tano, pia kulikuwa na mbio za watoto ambao walikimbia umbali wa kilometa 2.5. | michezo |
WAFUGAJI samaki katika maji baridi mkoani Morogoro wameshauriwa kuchukua tahadhari wakati wa kuandaa mabwawa ya samaki ili kuzuia magonjwa ya aina mbalimbali ukiwemo wa kupasuka na kukatika kwa vichwa vya kambale.Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Ugani wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dk Claudius Luziga alisema hayo hivi karibuni wakati alipotoa maelezo juu ya ufugaji bora wa samaki, magonjwa ya samaki, kinga na tiba wakati wa maonesho.Dk Luziga alisema samaki huugua magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na minyoo, fangasi na pia hupatwa na chawa, na wanaweza kubeba vimelea vya magonjwa kama taifodi na kipundupindu.Hata hivyo, alisema kituo kimeendelea kufanya utafiti wa kupata tiba ya kukabiliana na magonjwa ya samaki na hasa ugonjwa unaowashambulia samaki ujulikanao kama kuvu au ukungu ama fangasi, unaojulikana kitaalamu kama Saproleniass.Dk Luziga alisema ugonjwa wa kupasuka na kukatika vichwa kwa kiwango kikubwa unawaathiri zaidi samaki aina ya kambale, wanaofugwa katika mabwawa yaliyojengwa kwa saruji, yenye kina kifupi yasiyo na matope na kupitisha mwanga wa jua.Alisema, ugonjwa huo husababishwa pia na lishe duni na hasa ukosefu wa upungufu wa Vitamin C na tatizo hilo huwapata kambale wa rika zote ingawaje tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa samaki wa miezi minne na kuendelea.Alitaja dalili zake ni samaki kuvimba tumbo, macho kuwa makubwa na kutoka nje ikiwa na kujitokeza mstari mwekundu kati ya kichwa na kiwiliwili, samaki kuwa na kidonda kikubwa kati ya kichwa na kiwiliwili, kichwa kukatika au kupasuka na mwishowe samaki kufa.“Tunashauri kinga ni bora kuliko tiba,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za ugani wa SUA, Dk Luziga. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, ufugaji wa samaki ni miongoni mwa shughuli zinazokua kwa kasi nchini katika miaka ya hivi karibuni.Dk Luziga aliyataja baadhi ya maeneo ambayo samaki hufugwa kwa wingi katika maji baridi (maji yasiyo chumvi) ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya na Morogoro.Baadhi ya wafugaji wa samaki kutoka Manispaa ya Morogoro waliopata fursa ya kupatiwa elimu hiyo kwa nyakati tofauti walisema kuwa, elimu waliyopata itawasaidia vyema katika kuboresha ujenzi wa mabwawa ya samaki ili kuzuia magonjwa. | kitaifa |
SERIKALI imetoa onyo la mwisho kuhusu matumizi mabaya ya simu za mkononi yanayofanywa na baadhi ya watu wanaopiga picha miili ya watu wanaokufa kwenye ajali na kuzirusha mitandaoni.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametoa onyo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili ya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited waliokufa juzi mkoani Singida kwenye ajali ya barabarani.“Acheni kurusha picha za vifo vya ajali mitandaoni, utakuta mtu anarusha picha bila kujali kuwa waliokufa ni binadamu na wana ndugu zao, unadhani ndugu zao wanapoziona picha hizo wanajisikiaje, onyo hili ni la mwisho, hatutasema tena, Sheria ya Makosa ya Mtandao itaanza kufanya kazi yake,”alisisitiza Waziri Mwakyembe.Wafanyakazi hao waliokufa kwenye ajali hiyo na kuagwa jana Makao Makuu ya Kampuni hiyo ni Salim Mhando, Silvanus Kassongo, Charles Wandwi, Florence Ndibalema na Said Haji.Marehemu Salim Mhando alizikwa jana kwenye makaburi ya Manzese- Sweetcorner jijini Dar es Salaam, Charles Wandwi atazikwa leo kwenye makaburi ya Sinza, wakati mwili wa Said Haji ulisafirishwa jana kwenda Hale-Tanga, Kassongo alisafirishwa kwenda Iringa na mwili wa Florence Ndibalema utasafirishwa leo kwenda Bukoba kwa maziko.Katika salamu zake za rambirambi, Dk Mwakyembe alisema kuanzia sasa serikali haitaongea tena kuhusu tabia ya watu kurusha matukio ya vifo vya ajali mitandaoni badala yake Sheria ya Makosa ya Mtandao itaanza kuwashughulikia wenye tabia hiyo.Pamoja na onyo hilo, Dk Mwakyembe pia aliipongeza Azam Media Limited kwa mchango mkubwa wanaoutoa katika tasnia ya habari na taifa kwa ujumla.Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, alisema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo umeshaanza na dereva wa lori lililogongana uso kwa uso na basi aina ya Coaster lililowabeba wafanyakazi hao wa Azam ameshakamatwa.Alisema Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani linaendelea kukusanya ushahidi kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo ili taratibu nyingine za kisheria zifuate.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando, alisema wafanyakazi hao waliokufa waliondoka Jumapili jioni kwenda Chato mkoani Geita kwa ajili ya kurusha moja kwa moja uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato uliofanywa na Rais John Magufuli jana.Alisema wafanyakazi hao walilala Singida na saa moja asubuhi waliendelea na safari yao, lakini baada ya muda wa saa moja na nusu baadaye wakapata ajali na kupoteza maisha.Kutokana na msiba huo Tido aliishukuru serikali na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa ushirikiano mkubwa waliowapatia, lakini pia akatoa wito kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao hao kuwasiliana na menejimenti ya Azam Media Limited wakati wowote kama wanahitaji ushauri au msaada wa jambo lolote.Aidha taasisi na watu mbalimbali walituma salamu za rambirambi kwa msiba huo.Miongoni mwa taasisi hizo ni Chama Cha Mapinduzi.“Wafanyakazi hawa wa Azam Media Limited wamekufa kishujaa kwa sababu wamekufa wakiwa kazini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumefanya nao kazi kwa karibu sana,” alieleza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama hicho.Wengine waliotoa salamu za rambirambi ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Ilala (CCM), Musa Azan Zungu, Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Wilfred Kidao.Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk James Kilaba, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile, Deodatus Balile aliyetoa salamu kwa niaba ya Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na Hamisi Mzee alitoa salamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). | kitaifa |
Hata hivyo, mamlaka hiyo imeonya kuwa bei hiyo ya mafuta nchini haitaweza kupungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kutokubadilika kwa ushuru mbalimbali wa ndani wa mafuta.Pamoja na hayo, Kampuni ya Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PICL) imeiomba Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini kuingilia kati na kuihamasisha Serikali iongeze ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta Kurasini, ambayo kwa sasa hayako salama na ni hatari kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.Akiwasilisha taarifa ya ukokotoaji wa mafuta kwa kamati hiyo Dar es Salaam jana, Mtaalamu kutoka EWURA, Lorivii Long’idu, alikiri kuwa ni kweli kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imekuwa ikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.“Bei hizi zimeshuka kutoka dola 100 hadi kufikia dola 60 kwa pipa ambayo ni sawa na asilimia 40 kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la Ulaya katika kipindi hiki na kuwepo kwa tofauti za mitazamo ya kisiasa hasa katika nchi za Marekani na Urusi,” alisema Long’idu.Hata hivyo, alisema pamoja na bei hizo kushuka tangu Julai hadi Desemba mwaka jana, kwa kawaida kwa Tanzania huchukua takribani miezi miwili bei hiyo kuweza kufikia soko la ndani.Alisema bei zote za mafuta katika soko la ndani, zimekuwa zikishuka kuanzia robo ya mwisho wa mwaka jana sambamba na kushuka katika soko la dunia na kwamba bei hizo hukokotolewa na Ewura kwa kutumia kanuni maalum, inayotumia gharama halisi za uagizaji mafuta nchini, zinazotokana na meli za mafuta yaliyopokelewa mwezi husika yaliyonunuliwa mwezi wa nyuma yake.Alisema uhusiano wa bei za soko la dunia na soko la ndani, unapishana kwa miezi miwili na kwamba mafuta yanayotumika mwezi huu, Ewura ilikokotoa bei zake tangu Novemba kulingana na bei ya mafuta yaliyonunuliwa katika soko la dunia mwezi huo.Long’idu alisema kwa hali ilivyo sasa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia, zitaendelea kushuka kama hakutakuwa na tukio lisilo la kawaida duniani, hali itakayochangia kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la ndani japo si kwa kiwango sawia.Alisema pamoja na bei kushuka katika soko la dunia kwa kiwango chochote kile, bei ya ndani itashuka kulingana na thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani lakini pia ushuru uliopo ambao katika petroli unatozwa Sh 878, dizeli Sh 754 na mafuta ya taa Sh 701 kwa lita ambao wenyewe haubadiliki.Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Nishati na Madini, Jerome Bwanausi, aliagiza Ewura na PICL wanapokokotoa bei za mafuta kuhakikisha wanatoa ufafanuzi wa hali halisi ya bei za soko la dunia na utaratibu mzima wa uingizaji wa mafuta nchini ili kuondoa habari potofu zinazosambazwa juu ya bei hizo za mafuta.Aidha, aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuchukua hatua za haraka na kushughulikia suala la ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta ili kudhibiti hali ya hatari ya kulipuliwa kwa matangi hayo na kuhatarisha usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.“Hii ni hatari sana kwa namna yale mabomba yalivyo hayana ulinzi, watu wanatoboa mabomba na kuiba mafuta na kuweka maboya, endapo mtu yeyote akitupa moto pale Dar es Salaam nzima itakuwa haipo, hatua za haraka zichukuliwe, na kamati ipatiwe taarifa za ulinzi wa sasa katika eneo hilo,” alisisitiza.Aidha, alisema kutokana na hali ya hatari ya usafirishaji wa mafuta iliyopo sasa kupitia malori hasa katika vijiji malori hayo yanakopita na kulala, ni vyema Serikali ikaanza mchakato wa kuchimba mabomba ya kusafirishia mafuta na kufufua reli ili kudhibiti usalama wa wananchi. | uchumi |
BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na wawakilishi wa kimataifa Simba leo wana kazi nzito ya kusaka ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ya Congo.Kitendo cha kutinga hatua hiyo ni historia nyingine mpya baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2003. Kipindi hicho kutinga hatua ya makundi ilikuwa ndio robo fainali tofauti na sasa mambo mengi yamebadilika kwenye michuano hiyo. Sasa wawakilishi hao wanatamani mafanikio zaidi na nia yao ni kucheza fainali za michuano hiyo. Wekundu hao wa Msimbazi waliwahi kufika hatua hiyo miaka 26 iliyopita mwaka 1993 na tangu hapo uwakilishi wao kwenye michuano ya kimataifa haukuwa wa kuridhisha.Bila shaka kutokana na ubora walionao sasa chini ya mwekezaji wao Mohamed Dewji anayependa mafanikio, kila kitu kinawezekana lakini mtihani walionao ni kuwatoa TP Mazembe. Simba ilibezwa kufika mbali ikadhihirisha mbele ya mashabiki wake na watanzania kwa ujumla kuwa inaweza. Ikahakikisha maadui zake wote hawatambi nyumbani kwake. Ili kuwadhibiti kwa kutumia uwanja wa nyumbani Al Ahly ya Misri anayeogopwa Afrika kwa ubora lakini kwenye uwanja wa Taifa alifungwa bao 1-0, ikampiga AS Vita ya Congo aliyefanya vizuri Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kwa kufika fainali, mabao 2-1, JS Saoura ya Algeria.Hiyo ilikuwa ni harakati za makundi lakini leo wapo katika hatua ya robo fainali hatua ngumu kwa vile ni mtoano. Simba inatakiwa kuendeleza ule moyo wa kushinda nyumbani ila ni muhimu kwao kubadilika kwa kushinda mabao mengi zaidi na kutowapa nafasi wapinzani wao kupata bao la ugenini. Kuna makosa yalifanyika kwa wekundu hao katika mechi tofauti kuanzia hatua ya awali walizocheza nyumbani kwa kuruhusu wapinzani kupata mabao ya ugenini. Dhidi ya Mbabane walishinda 4-1, dhidi ya Nkana 3-1 na dhidi ya Vita 2-1 jambo ambalo ni hatari kwao hasa katika hatua hii waliyofikia sasa ambapo umakini unahitajika.Kingine wamekuwa wakiwadharau Mazembe na kusema msimu huu eti sio bora kama miaka mingine. Kama wangekuwa sio bora wasingefika hatua hii muhimu hivyo, wakiwadharau wanaweza kuwaadhibu kwasababu ni timu yenye uzoefu mkubwa na ina wachezaji wengi wazuri. Mazembe sio mara ya kwanza kuja kucheza katika ardhi ya Tanzania, wanaujua vizuri uwanja wa taifa, Dar es Salaam. Waliwahi kucheza nao mwaka 2011 katika mchezo wa pili hatua ya makundi kwenye uwanja huo Mazembe ikashinda 3-2 na ule wa kwanza uliochezwa kwao ikashinda 3-1.Kwa maana nyingine, mechi hii ni wakati sahihi kwa Simba kulipa kisasi kwa Mazembe. Timu hiyo ya Lubumbashi, Congo tayari itakuwa imeshawasoma wapinzani wake kwa kujua kuwa kumbe inakuwa wakali hasa kwenye uwanja wa nyumbani, wanaweza kuja na mbinu zao nyingine kuwadhibiti wekundu hao. Udhaifu uliopo kwa Simba ni kushindwa kumudu michezo ya ugenini.Takwimu za hatua ya makundi katika michezo iliyopita inaonyesha hawakupata bao hata moja katika michezo mitatu tena wakiruhusu kufungwa mabao mengi. Ukitizama kule Misri ilifungwa 5-0 dhidi ya Al Ahly, kule Congo ikafungwa 5-0 dhidi ya Vita na kule Algeria ilifungwa 3-0 dhidi ya JS Saoura. Kutokana na udhaifu huo, hawana budi kubadilika kama wanataka kusonga mbele kwa sababu huenda Mazembe wakaja kutafuta sare kisha wakaona wanaweza kumaliza mchezo wakiwa kwao. Ni ukweli usiopingika kuwa Simba kwa upande wa Tanzania ndio timu tishio kwa sasa kwa sababu kati ya timu 20, ndio pekee imepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 22, ikishinda 18 na kupata sare tatu, ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 57.Wanapewa uwezekano wa kuwaengua vinara Azam inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 62 katika michezo 29 na Yanga inayoongoza katika michezo 29. Sababu wekundu hao wako nyuma michezo saba, ikiwa watashinda watachukua uongozi huo kiulaini. Ukiachana na ubora wao katika ligi, wana kikosi kizuri chenye washambuliaji hatari na tegemeo kama Mnyarwanda Meddie Kagere, Mganda Emmanuel Okwi na Mtanzania John Bocco. Kagere ameifungia timu yake mabao 15 kwenye ligi na michuano hiyo ya kimataifa mabao sita hivyo sio wa kubezwa.Bocco ana mabao 11 na Okwi ana saba kwenye ligi. Simba ikiwa nyumbani bado inajivunia safu bora ya ulinzi baada ya kuruhusu nyavu zake kuguswa mara saba pekee ikiwa ndio timu iliyofungwa mabao machache ingawa kimataifa bado hawako vizuri. Kwa upande wa TP Mazembe sio timu ya kudharauliwa kwani katika ligi ya kwao bado wapo kwenye ubora, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 58 nyuma ya AS Vita inayoongoza kwa pointi 65. Timu hiyo ina wachezaji wengi hatari na wenye uzoefu mkubwa kama Tresor Mputu, Kelvin Zatu, Meshaki Elia na Jackson Muleka.Katika michezo yao iliyopita ya hatua ya makundi timu hiyo inaonekana kutokuwa na rekodi nzuri ugenini. Michezo mitatu waliocheza, miwili walipata suluhu dhidi ya Africain, sare ya bao 1-1 dhidi ya Ismaily na kufungwa 3-0 dhidi ya Constatine. Kwa kutizama na takwimu hizo inaonesha kuwa wanaweza kuja na lengo la kutafuta sare wakiamini nyumbani kwao ndio sehemu wanakoweza kupindua matokeo.Mechi zao za marudiano dhidi ya timu hizo walizocheza kwao zinaonesha namna gani matokeo ya nyumbani yaliwabeba. Ilishinda mabao 8-0 dhidi ya Africain, 2-0 dhidi ya Constatine na 2-0 dhidi ya Ismaily. Mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa kila mmoja, hasa wekundu hao wanahitaji matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani kisha kujipanga na mechi ya marudiano ya ugenini itakayochezwa April 13, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems anasema anawaheshimu Mazembe hivyi ataingia kwa tahadhari. “Mazembe nimeifuatilia, ni timu bora na inafanya vizuri kwenye mechi zake, nimewaandaa wachezaji wangu, tutaingia kwa tahadhari kubwa,” anasema. | michezo |
Fainali hizo zimepangwa kufanyika Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Dilunga ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu ameeleza kuwa wengi wamekuwa wakiitazama Singida kama timu iliyowatoa Yanga kwenye robo fainali na inapewa nafasi kubwa kutokana na hilo kitu ambacho si sahihi.Aliongeza kuwa, ingawa Singida ni timu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu na kuonesha ushindani wa kutosha lakini siyo kigezo cha kuonekana wanaweza kuibuka mabingwa mbele yao.“Unajua Singida siyo timu ngeni kwetu, watu waelewe kwamba tulishakutana nayo mara mbili msimu huu kwa hiyo tunawafahamu na isitumike kigezo cha kuwatoa Yanga ikaonekana kama inaweza kupata ubingwa mbele yetu.“Ila niseme tu, wao wamepambana kufika hapo ina maana wapo vizuri kwa hiyo na sisi tunajipanga zaidi na zaidi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo wa fainali,” alisema Dilunga aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-0 kwenye nusu fainali dhidi ya Stand United.Kabla ya kukutana kwenye fainali hiyo tayari timu hizo zilishakutana mara mbili kwenye Ligi Kuu ambapo katika mechi ya kwanza iliyopigwa Manungu, Morogoro zilitoka suluhu na ile ya marudiano kwenye uwanja wa Namfua, Mtibwa ilishinda kwa mabao 3-0. | michezo |
WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (AEAC) kutoka Tanzania, wameeleza njia muafaka ya kuondoa vikwazo visivyo vya ushuru katika jumuiya hiyo ni uanzishwaji wa kamati ya kusimamia biashara.Aidha, wabunge wamepongeza jitihada za serikali katika kuharakisha kupitisha makubaliano, yanayofanywa kwenye jumuiya hiyo, huku ikiwa makini katika kulinda maslahi ya nchi. Pia, wabunge hao wametaka Watanzania kujivunia nchi yao, kwa kuwa na amani, huku Rais John Magufuli akisifika kwa kuhakikisha rushwa inaondoka nchini. Wabunge hao wameitaka Tanzania kuenzi Kiswahili katika EAC na kuhakikisha wimbo wa jumuiya hiyo, unaimbwa katika shule za msingi.Walisema hayo walipozungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kabla ya kuanza ziara ya siku tano nchini Tanzania. Katika ziara hiyo, watakutana na wadau mbalimbali nchini ili kujua vikwazo, mafanikio na nini cha kufanya kwa watanzania katika kukamata fursa za kibiashara zilizopo katika mtangamano wa jumuiya hiyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa waandishi wa habari, kabla ya kuanza ziara hiyo, walieleza bayana kuwa bado kuna changamoto kwa Watanzania kutambua na kukamata fursa zilizopo katika jumuiya hiyo. Mwenyekiti wa wabunge hao, Dk Abdullah Makame (pichani) alisema moja ya changamoto kubwa kwa watanzania na wananchi wengine ndani ya jumuiya hiyo ni kushindwa kuundwa kwa kamati ya kusimamia biashara EAC, ambayo ni utekelezaji wa Ibara ya 24 katika makubaliano ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.“Kuundwa kwa kamati hii kutakuwa mwarobaini wa matatizo, kwani kutapunguza vikwazo visivyo vya kibiashara, kwani itifaki inazungumzia kuwa kila nchi inatakiwa kuwa na wajumbe watatu wenye utaalamu wa sheria na forodha, kwani kazi ya kamati hii kwa sasa inafanywa na mawaziri,“alisema. Alipongeza kazi za kukabili vikwazo zinavyofanywa na mawaziri, lakini kwamba ni vema kuwa na wataalamu.Alisema vikwazo hivyo siyo suala la kuvusha bidhaa pekee, bali pia binadamu kwenda katika nchi nyingine kupata ajira na kupata fursa mbalimbali. Makame alisema katika ziara yao iliyoanza jana, watakutana na wataalamu katika sekta binafsi na ile ya umma, kuona jinsi Tanzania inavyotekeleza makubaliano ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja pamoja na changamoto zake.Pia, watakutana na wanafunzi wa vyuo vikuu katika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Aidha, watapata nafasi ya kukutana na asasi za kiraia, wananchi na wafanyabiashara katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya kwenda mikoani na nchi jirani cha Ubungo, Dar es Salaam, ambapo watapata nafasi ya kutoa elimu kwa watanzania kuhusu mtangamano wa EAC.Wakizungumzia tuhuma zinazotolewa mara kwa mara na baadhi ya vyombo vya habari ndani ya EAC, kuwa Tanzania inakwamisha utekelezaji wa makubaliano kadhaa, Mbunge wa jumuiya hiyo, Adam Kimbisa alibainisha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza, kwa kupitisha na kutekeleza mikataba mingi ya jumuiya hiyo. “Ni vema kueleza kuwa Tanzania ndiyo nchi kubwa katika EAC huku ikiwa ni mmoja wa waanzilishi, kuna baadhi ya maamuzi ni lazima kufanywa kwa umakini sana,” alibainisha Kimbisa.Mbunge mwingine wa jumuiya hiyo, Fancy Nkuhi alisema kuna baadhi ya masuala ya utekelezaji wa makubaliano, yanakuwa shida kutekelezwa kutokana na sheria kuwa tatizo, hivyo ni vema kufanyia kazi ili kurahisisha utekelezaji wake, kwani watendaji wanabanwa na sheria. Alitaka vijana kujitokeza katika mkutano, watakaofanya Jumatano jioni UDSM ili kufahamu namna ya kujiandaa kiutendaji na kutumia fursa zilizopo katika jumuiya.Mbunge Habib Mnyaa alisema Tanzania imejiweka mbali katika kuhakikisha umoja wa EAC unaimarika, kwa wimbo wake kuimbwa kwa ufasaha na watu wake, hivyo kutaka kuanza utaratibu wa kutumika katika shule za msingi. Alisema kwa sasa wimbo huo unaotumia lugha ya Kiswahili, hutumika katika nchi za Rwanda, Burundi na nyingine. Alisema pia bendera ya EAC ni vema ianze kupeperushwa katika wizara zote ili kujifahamisha na siyo kuwapa nguvu wengine.Alisema Tanzania ni mmoja wa waanzilishi wa EAC lakini nadra kuona bendera hiyo. Mbunge Ngwaru Maghembe alitaka watanzania kujivunia kuwa na amani katika ukanda huo. Alisema hivi karibuni walifanya ziara katika kambi za wakimbizi kwenye Jumuiya hiyo na ni Tanzania pekee ambayo haina wakimbizi kwenye makambi.Pia alieleza kuwa Tanzania inajivunia Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli ambaye anasifika katika ukanda huu katika kupambana na rushwa na amedhamiria kuiondoa nchini. Mbunge Pamela Maasay alitaka watendaji kuhakikisha kunakuwa na viwango sawa vya bidhaa katika EAC, ili kuwezesha wananchi kutoka pande zote kuvifuata na kunufaika. Kuhusu uanzishwaji wa Baraza la Vijana EAC, alisema muswada umepitishwa tayari na lengo ni kuwezesha vijana kukamata fursa mbalimbali. | kitaifa |
KIUNGO wa zamani wa Yanga Athumani China amewatipia lawama mabeki na kipa wa timu yake hiyo zamani kwa kuruhusu bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa kufungwa bao 1-0 na Stand United na kuhitimisha safari ndefu ya timu hiyo kutokupoteza mechi kwenye ligi hiyo.China aliyewahi pia kutamba na Simba kwenye miaka ya 1990 alitazama goli hilo kupitia video na kuwatupia lawama mabeki Kelvin Yondani, Andrew Vicent’Dante’ na kipa Claus Kindoki.“Wote wanastahili lawama, huyu beki wa pembeni(Yondani) kwa kuruhusu krosi kwani alikuwa na muda mwingi wa kumsogolea yule wingi kisha akazuia krosi. Lakini kipa nae(Kindoki) na mabeki wa kati(Dante na Gadiel) walitakiwa kujiandaa na tukio lolote ikiwa krosi imepigwa na hawakufanya hivyo.“Ndio mpira wa kitanzania mapungufu yapo lakini hatujifunzi kile tunachotazama kwenye televisheni. Kitu cha kwanza kwa mchezaji yoyote aliyepo nafasi ya pembeni ni lazima afanye kila afanyalo kutoruhusu krosi kuingia golini kwenu kwani unakuwa haujui wenzako wamejipangaje, kwani krosi ni nusu goli,”alisema.China baada ya kuangalia kipande hicho cha video. Hata hivyo nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania alisema kuwa bado timu yake hiyo ya zamani ina nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu kama hawataruhusu makosa kama hayo yajirudie. | michezo |
POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma Shule ya Sekondari St Apostos, Yela Sylvester maarufu Cosmas (17), kwa kosa la kudanganya wazazi wake kuwa ametekwa ili ajipatie fedha.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jumanne Muliro amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo ni la Aprili 27, mwaka huu saa nne usiku katika Mtaa wa Mahaha wilayani Magu.Amesema hiyo ni baada ya kijana huyo kusindikizwa kwenda shule na mzazi hadi kwenye Kituo cha Mabasi cha Buzuruga jijini Mwanza na kupakizwa kwenye basi la Sheratoni, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Geita.Lakini, hakwenda shule na badala yake aliitumia simu namba 0689447247 na kutuma ujumbe mfupi kwa baba yake, huku akiificha laini yake ya zamani ya simu, kwa madai kuwa alikuwa ametekwa kwa lengo la kujipatia fedha.“Kwenye ujumbe aliomtumia baba yake, alidai kuwa endapo wasipomtumia fedha hizo atapelekwa na watekaji nchini Zambia kufanya kazi, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,” amesema Kamanda Muliro.Amesema polisi walifanya ufuatiliaji wa taarifa hizo za kutekwa kwa mwanafunzi huyo na kumtia nguvuni kijana huyo akiwa salama Lamadi wilayani Magu, akiwa na laini ya simu aliyoitumia kumdanganya baba yake kuwa alikuwa ametekwa.“Tunaendelea kumhoji na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake,” alisema Kamanda Muliro.Katika tukio jingine, Polisi imewakamata watu watatu kwa kosa la kupatikana na kilogramu 15 za bangi na watuhumiwa wengine wawili kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi lita 33.Kamanda Muliro alisema tukio hilo ni la kati ya Machi na Aprili katika operesheni kabambe inayoendelea.Aliwataja watu waliokamatwa na bangi kuwa ni John Marwa (26), Bhoke John (30) na Maria Stephano (25) wote wakiwa ni wakazi wa Kishiri Wilaya ya Nyamagana.Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa na lita 33 za pombe ya moshi kuwa ni Mkemwa Matono (45), mkazi wa Fumagila na Vedastina Tibikunda (30) ambaye ni mkazi wa Bugarika jijini Mwanza.“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa, na siku hizi mtaona waliokamatwa ni wanawake, siku hizi unakuta mwanamke anasafirisha bangi kama furushi,” alifafanua. Aliongeza kuwa polisi inaendelea na mahojiano na watuhumiwa watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika. | kitaifa |
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow, alisema ujumbe wa simu utawawezesha wateja kwa haraka kufuatilia miamala inayofanyika katika akaunti zao.“Kwa kuleta, huduma hii itawawezesha wateja wetu kutambua muamala uliofanyika isivyo halali hivyo kuweza kuchukua hatua ya haraka,” alisema Jallow. Kwa mujibu wa Jallow, taarifa za ujumbe zitatumwa kutoka katika miamala itakayokuwa ikifanyika katika mashine za ATM au vituo vya mauzo vitavyokuwa vimetoa huduma kwa kutumia kadi zao za benki.Huduma hiyo inatolewa bure, hivyo wateja wa NBC hawatalipia chochote watakapokuwa wakipokea ujumbe katika simu zao. Wateja wa NBC hawatahitajika kujisajili kwa huduma hiyo, kwani ujumbe utatumwa kupitia namba zao za simu zilizohifadhiwa katika kumbukumbu za NBC.Ofisa huyo wa benki alisema, wateja wote wenye namba za simu zilizo hewani watapokea ujumbe mara watakapofanya muamala kwenye ATM au katika vituo vya mauzo wakitumia kadi za manunuzi.“Mteja yeyote asipopokea ujumbe, basi inawezekana hatuna namba yake ya simu iliyosajiliwa na benki katika kumbukumbu zetu ama namba iliyosajiliwa siyo sahihi,” alisema. Aliendelea kusema, “Ikitokea hivyo tunashauri wateja kuchukua hatua ya haraka kwenda katika tawi la NBC lililo karibu ili kuhakiki taarifa zao, ili waanze kufurahia huduma hii.” | uchumi |
MENEJA wa timu ya Mbao FC Almas Moshi amesema timu yao ipo tayari kuhakikisha inapambana kwa hali na mali ili iweze kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Simba SC kwenye Kombe la Sportpesa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zitacheza leo kuanzia saa nane mchana kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo, huku mechi nyingine ya fainali itazikutanisha timu za Kenya, ambazo ni Kariobangi Sharks dhidi ya Bandari FC.Moshi amesema kuelekea mchezo huo wachezaji wake wote wapo kamili kuweza kuikabili Simba SC,ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili katika mashindano hayo.Alisema mpaka sasa anafarijika sana na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mashindano hayo.Katika michezo miwili, timu hiyo iliyocheza, Mbao FC imeshinda mechi moja dhidi ya bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Gor Mahia kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1, huku ilifungwa mechi moja dhidi ya Kariobangi Sharks kwa penalti 6-5 baada ya sare ya bila kufungana.Moshi alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka wa klabu yao wajitokeze kwa wingi kuhakikisha wanaishangilia timu yao katika mchezo wao wa leo pamoja michezo mingine ya Ligi Kuu iliyobakia.Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo David Mwasa alisema watapambana ili waweze kutimiza lengo lao la kushika nafasi ya tatu ya michuano hiyo, baada ya kuikosa ya kwanza. | michezo |
SERIKALI imewashauri wanaume nchini kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ambazo zimethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pindi watakapokuwa na uhitaji huo. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ametoa ushauri huo Bungeni Dodoma, leo Jumatatu, wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kutaka kujua sababu za kuongezeka kwa matumizi ya dawa hizo na ikiwa serikali imezichunguza na kujua zinafaa. Hata hivyo, Dk Mwinyi ameeleza kuwa zipo dawa ambazo hazina kemikali na zimethibitishwa na TFDA kutokuwa na madhara, hivyo wanaohitaji watumie hizo, na sio dawa zisizothibitishwa. Aliongeza kuwa hakuna dawa za kuongeza maumbile ya kiume ambazo zimefanyiwa utafiti na kubainika kuwa salama kutumia, hivyo wananchi wasirubunike kununua dawa hizo. “Wananchi acheni kutumia dawa hizi kwani mtapata madhara, taarifa niliyo nayo ni kwamba hakuna dawa ambazo zimethibitishwa kitaalamu na kupewa kibali kwa ajili ya kuongeza maumbile,” alifafanua. | kitaifa |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema hakuna nchi au ukanda, unaoweza kuwa na uchumi endelevu pasipokuwa na maendeleo ya kidijiti, hususani katika sekta ya afya.Amebainisha hayo Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa saba wa Afya na Sayansi wa Afrika Mashariki. Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili.Samia alisema juhudi zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kuleta mabadiliko ya haraka ya teknolojia na kidijiti katika kusaidia utekelezaji wa mipango ya sekta ya afya, ni hatua sahihi katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) Namba 3 na mpango wa afya kwa wote.Aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa kuwekeza katika sekta ya afya na teknolojia sahihi za kidijiti ni muhimu kwa maendeleo ya jumuiya nzima, lakini pia utekelezaji wa Mkataba wa EAC hususani Kifungu cha 118 kinachotaka kuwepo kwa ushirikiano katika sekta ya afya, na vipengele vingine ninavyohusu soko la pamoja.“Nimefurahi kuona kwamba mkutano huu, siyo tu kwamba unahudhuriwa na wanasayansi kutoka Afrika Mashariki pekee, lakini pia umewaleta pamoja washiriki na wajumbe kutoka Afrika nzima na nje ya Afrika. Naamini mkutano huu utawapatia fursa ya kubadilishana taarifa kuhusu maendeleo ya sasa na kuja na mbinu za kukuza teknolojia za ubunifu ambazo zitaharakisha kufikia mpango wa maendeleo endelevu,” alisema Samia.Kwa kuwa sayansi na teknolojia ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya, Samia aliwapongeza waandaaji wa mkutano huo kwa kuchagua kaulimbiu inayoendana na wakati, inayosema “Teknolojia kwa ajili ya mageuzi ya mifumo ya afya na kufikia Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.”Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, kaulimbiu hiyo imekuja wakati mwafaka ambao dunia iko katika mageuzi ya nne ya viwanda, ambapo matumizi ya sayansi na teknolojia yanaongoza katika nyanja zote.Alisema suala la kuwa na maendeleo endelevu halitawezekana, kama uwekezaji katika teknolojia za kisasa hautafanyika ili kuzisaidia nchi hizo kuwa na majibu na ufumbuzi kwa matatizo na changamoto nyingi za kiafya kwa umma.Samia alisema Tanzania tayari imeshaanza kujenga mfumo wa kidijiti wa huduma za afya kupitia Wizara ya Afya na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo, ikiwemo Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Alisema matumizi ya kidijiti yameiwezesha serikali kufuatilia usafirishaji wa dawa tangu zinaponunuliwa na hadi zinapopokelewa katika eneo husika.Lakini, pia kupitia NHIF, imesaidia katika usimamizi wa uanachama wa mteja, madai na mchango na kupitia TFDA, imesaidia kupata taarifa za uagizaji bidhaa na uuzaji nje bidhaa pamoja na kupata taarifa kimtandao kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya dawa na vipodozi.“Kuhusu kile kinachofanyika katika taasisi zetu, tumeweka mfumo wa usimamizi wa hospitali katika hospitali zote za serikali. Mfumo huu hutoa taarifa za wakati na unaweza kufuatilia hali ya mgonjwa na akiba ya dawa, hivyo tumekuwa na matokeo mazuri tangu tuanze matumizi ya mfumo wa kidijiti ikiwemo kuboresha huduma za afya, kuongeza ufanisi na kuokoa muda na kuimarisha usalama wa taarifa,” alieleza Makamu wa Rais.Samia aliwaeleza washiriki hao kuwa ufanisi katika kutekeleza mpango huo wa kikanda, unategemea siyo tu ufanisi wa uratibu kutoka kwa Tume ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki, bali pia kutoka kwa nchi washirika wa EAC, washirika wa maendeleo na kila mdau wa sekta ya afya katika nchi washirika. | uchumi |
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wazazi na walezi wilayani Karatu kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule hata kama hawana sare za shule.Aidha ameagiza uongozi wa serikali ya kijiji cha Lositete kuchukuliwa maelezo na polisi kuhusu sababu za kutochangia maendeleo ya elimu, badala yake wanaingiza siasa na kusababisha saruji kuganda.Gambo ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Lositete, kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu alipokwenda kukagua hali halisi ya madarasa pamoja na idadi ya wanafunzi walioanza masomo ya kidato cha kwanza.Ameagiza hivyo kutokana na taarifa ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Upper Kitete, Josephat Mau iliyodai kuwa wanafunzi tisa kati ya 171 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo wameripoti shule.Mwalimu Mau amesema wanafunzi hao 162 hawajaripoti shuleni hapo kutokana na kukosekana na sare za shule huku walioripoti wakiwa ni tisa kwa sababu ya wazazi au walezi wao kutouza maharage kwani hakuna soko.Baada ya mwalimu huyo kutoa taarifa hiyo, Gambo aliagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni na nguo za nyumbani hata kama hawana sare ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakisubiri kuwanunnulia mahitaji ya shule."Rais ameagiza elimu bure hivyo wazazi au walezi watoeni watoto wenu majumbani ili waende shule bila ya kuwa na sare za shule huku mkiendelea kutafuta sare lakini pia nasisitiza nyie wananchi acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo, "amesema.Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete, Gambo aliagiza mwenyekiti wa kijiji cha Upper Kitete, William Safari pamoja kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wanadai hawajasomewa tangu mwaka 2017 hadi mwaka jana.Awali, baadhi ya wananchi walidai kuwa wameshindwa kujenga madarasa pamoja na maabara kwa sababu walichanga fedha ambazo inadaiwa zililiwa na aliyekuwa mkuu wa shule hiyo, Andrew Sulle.Anadaiwa kuchukua Sh milioni nane.Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema wananchi zaidi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete wanapenda kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo.Amesema amejitahidi kutatua changamoto zao ikiwamo kuhakikisha mwalimu huyo anachukuliwa hatua za kinidhamu na ameshahukumiwa kifungo.Amesema wanafunzi 5,313 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana huku wanafunzi 4,000 sawa na asilimia 75.3 walifaulu.Wanafunzi 3,446 wamepangwa kwenye shule za kata zilizokuwa na madarasa 83 na wanafunzi 539 walikosa nafasi.Alisisitiza kuwa wanafunzi hao 539 waliokosa nafasi hivi sasa wameshaanza masomo katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwapo shule ambazo wanafunzi hawakupangwa.Alisema wanaandika barua kwa wadau na kuhamasisha wanananchi kujenga madarasa pamoja na kukarabati viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma. | kitaifa |
ZIKIWA zimebakia siku chache, tamasha la Sauti za Busara 2020 kuanza, waandaaji wake wamesema mwaka huu wanataka kutumia katika kukemea unyanyasaji wa kijinsia suala ambalo linaendelea kutesa tasnia ya muziki na jamii. Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Februari 13 hadi 16 katika eneo la kihistoria la Ngome Kongwe Zanzibar ambapo watazamaji wataweza kupata burudani ya muziki mubashara kutoka kwenye majukwaa matatu tofauti. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmud alisema tamasha la mwaka huu linaunga mkono juhudi za kukuza muziki unaopigwa mubashara wakati huo huo, kukemea unyanyasaji wa kijinsia. “Suala hili la unyanyasaji wa kijinsia litashughulikiwa chini ya kauli mbiu isemayo ‘Paza sauti yako, sema hapana kwa unyanyasaji wa kijinsia’ ikikusudia kubadilisha mitizamo, kuhamasisha mazungumzo na kuhimiza heshima kwa wanawake kwa kukuza uelewa juu ya udhalilishaji wa kijinsia,”alisema. “Hivi sasa nchini Tanzania, tunaona ni wanawake wachache tu wanaofanya muziki wa asili na wenye kuvutia. Hii ndiyo sababu kwa tamasha la Sauti za Busara la 2020 tulichagua wasanii kama Siti & the Band (Zanzibar), Thaïs Diarra na Mamy Kanouté (kutoka Afrika Magharibi), Pigment (Reunion), Evon na Apio Moro (Uganda) na wengine kutoka mkoa wa Afrika Mashariki,”aliongeza. Alisema hao ni wanawake wenye hisia kali ambao hutumia muziki kufikisha ujumbe na kujielezea. Wakati huo huo, bado wote ni waburudishaji wazuri kwa kupiga mubashara. | michezo |
['Red Bull Salzburg imeweka bei ya pauni milioni 86 kama dau la usajili kwa mshambuliaji Erling Braut Haaland, 16. (Tuttosport - in Italian)', 'Arsenal inaweza kumuuza kiungo wake Granit Xhaka ,27, mwezi Januari baada ya kuvuliwa unahodha. (Mirror)', 'Manchester United wanafuatilia maendeleo ya winga wa Burnley na timu ya umri wa miaka 21 ya England Dwight McNeil, 19 (Sun)', 'Aston Villa itakataa ofa yoyote ya Manchester United kwa kiungo wa uskochi John McGinn,25.(Birmingham Mail)', 'Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri atafaa sana kwa Manchester United, anasema kocha wa zamani wa timu ya taifa Italia Marcello Lippi. (Mail)', 'Allegri atakua chaguo zuri kwa Bayern Munich, anasema mshambuiaji wa zamani Luca Toni.(Sport1, via Goal)', 'Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amesema angependa kushika nafasi iliyoachwa wazi kwenye klabu ya Bayern Munich. (Bein Sports)', 'Kiungo wa pembeni wa Chelsea na timu ya taifa ya England Mason Mount, 20, amekana kauli ya mchezaji mwezake wa zamani Mitchel van Bergen kuwa huenda akajiunga na Madrid au Barcelona. (Express)', 'Makamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward alitaka kumsajili kiungo wa Paris St-Germain Marco Verratti,27 na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Real Madrid Raphael Varane,26,(Manchester Evening News)', 'Real Madrid wamefanya mazungumzo na kiungo wa Napoli Fabian Ruiz,23, kuhusu uhamisho muhimu kuelekea Bernabeu msimu ujao. (ESPN)', 'Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema ana furahia namna anavyojitoa Christian Eriksen, 27 ingawa mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na taarifa za kuachana na klabu hiyo.(Football London)', "Arsenal inapaswa ''kutumia pesa nyingi'' kumpata Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers kwenye klabu hiyo, anasema mchazaji wa zamani Paul Mason. (Sky Sports)", "Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina Mauro Icardi, 26, anafanya ''kila kitu'' kufanikisha uhamisho wake kwa mkopo kutoka Inter Milan kwenda Paris St-Germain kuwa wa kudumu (RMC - in French)", 'Barcelona itamtazama kwa karibu kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Kai Havertz,20, juma hili katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico Madrid.(ESPN)', 'Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 05.11.2019', 'Unalitamkaje jina la nyota huyu wa Liverpool?', "Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema anafahamu mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe,20 ''ana ndoto'' ya kukichezea kikosi cha mabingwa wa La Liga. (Goal)", 'Rangers striker Alfredo Morelos, reportedly a target for Aston Villa, says he has had no contact with any club but the Colombian, 23, added: "Many teams that would be offering a good amount of money for me." (Antena 2, via Birmingham Mail)', "Mshambuliaji wa Rangers Alfredo Morelos, anayeripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Aston Villa, amesema hana mawasiliano na klabu yoyote lakini mchezaji huyo 23, amesema ''labda itokee timu itakayotangaza ofa nzuri kwake.''(Antena 2, via Birmingham Mail)"] | michezo |
UGANDA imetimiza ndoto zake za kutengeneza magari ambapo inakuwa nchi ya nne kati ya sita za Afrika Mashariki.Nchi hiyo iko mbioni kutengeneza mabasi ya kisasa ya abiria kwa ajili ya biashara ndani na nje ya Afrika Mashariki wakati wa Krismasi kwa gharama ya Sh milioni 95 za nchi hiyo, huku kukiwa na fursa ya kulipa kwa awamu.Magari hayo yatatengenezwa na kampuni ya Kiira Motors Corporation (KMC) inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Paul Musasizi, wanajiandaa kutengeneza mabasi ya kisasa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.“Bado tupo katika maandalizi na tunaongezea ujuzi na Wizara ya Sayansi. Tumeshatengeneza magari ya mfano na kufanyia majaribio katika maeneo ya Kisoro na Karamoja, hatukuona shida yoyote, hivyo tupo tayari kuanza kutengeneza magari kwa ajili ya biashara,” alisema.Musasizi aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuihamishia KMC kutoka Wizara ya Viwanda kwenda Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk Ruhakana Rugunda.Alisema mabasi ya Kiira yatakayotumia nishati ya umemejua, yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 90 kwa wakati mmoja.“Tutaajiri watu wetu na mabasi yatauzwa kwa gharama inayokadiriwa kuwa Sh milioni 95 za Uganda,” alisema na kuongeza kuwa, mbali ya mabasi, watatengeneza pia magari madogo, malori, magari madogo ya kubeba mizigo na mengine kwa ajili ya matumizi mbalimbali.Ajira 14,000 zikiemo 2,000 za moja kwa moja zinatarajiwa kuzalishwa na TMC kwa ajili ya mafundi mbalimbali, wakiwemo wa spea za magari.Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Elioda Tumwesigye alisema wanakamilikisha makubaliano na China juu ya kusaidia masuala ya ufundi na kwamba tayari wataalamu wa Uganda wapo nchini China kwa mafunzo zaidi ya teknolojia ya utengenezaji magari.Waziri Mkuu alisema mabadiliko ya kuihamisha taasisi hiyo ya Serikali ni ya kawaida, yenye lengo la kuhakikisha mradi unapata maendeleo zaidi.Alikipongeza pia Chuo Kikuu cha Makerere kupitia Kitivo chake cha Uhandisi, kwa kutoa fursa kwa vijana kuonesha ubunifu wao.Wazo la ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji wa magari, lilianza mwaka 2011 baada ya juhudi na maarifa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere kutengeneza gari linalotumia umeme la Kiira EV na linalotumia nishati ya jua la Kayoola EV mwaka 2016.Kutokana na mafanikio hayo ya wanafunzi wa chuo kikubwa barani Afrika, mwaka 2014 serikali ilitenga kipande cha ardhi mashariki mwa Jinja kwa ajili ya kiwanda cha magari ya KMC, huku Rais Yoweri Museveni akiwa mstari wa mbele kuhakikisha dhamira ya Uganda kutengeneza magari yake inafikiwa.Uganda inayoagiza wastani wa magari 50,000 kwa mwaka, itakuwa na soko la uhakika na magari ndani na nje ya nchi, hasa Ukanda wa Afrika Mashariki ambayo kwa asilimia kubwa huagiza magari kwa gharama kubwa kutoka Ulaya, Marekani na barani Asia katika nchi za Japan, Korea, India na China.Inakadiriwa kuwa, nchi za Afrika Mashariki huagiza wastani wa magari 250,000 kwa mwaka na mahitaji yanatarajiwa kupanda hadi kufikia magari 500,000 kufikia mwaka 2030.Juhudi Afrika Mashariki Tayari nchi nyingine za Afrika Mashariki zikiwamo Tanzania, Rwanda na Kenya zinaongeza kasi ya uzalishaji wa magari kwa ajili ya soko la nchi hizo na nyingine jirani.Mathalani, Kampuni ya Hanspaul Automechs Limited (HAL) iliyopo eneo la viwanda Njiro jijini Arusha, Tanzania inatengeneza magari makubwa ya kubeba watalii maarufu kwa jina la ‘War Bus’.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Satbir Hanspaul, yanauzwa Kenya, Afrika Kusini na nchi za Ulaya.Kampuni hiyo imebuni na kutengeneza pia magari maalumu ya kubeba taka, yanayofaa kwa mazingira ya Tanzania, ikiwemo hali ya hewa, aina ya barabara na mfumo wa maisha wa wananchi wake.“Watu wengi hawataamini kwamba, nchi zenye viwanda vya kutengeneza magari kama Afrika Kusini na zile za Ulaya sasa zinanunua magari kutoka Tanzania, lakini ukweli ndio huo, wananunua pia magari kutoka Afrika, hususan Tanzania.Magari hayo yenye nembo za Toyota, Nissan na Land Rover, yanatengenezwa Tanzania kwa kutumia mashine za kisasa zikiwemo roboti kama ilivyo kwenye viwanda vya magari katika nchi zilizoendelea.HAL ilianzishwa mwaka 2007 na imelenga kuteka asilimia 25 ya soko la magari na spea zake katika nchi za EAC.“Tuna kila kitu kinachohitajika, mitaji kutoka kwenye taasisi za benki, intaneti yenye kasi, mawasiliano ya simu, nguvukazi ya kutosha na ardhi ya kutosha, tunachohitaji sasa ni watu kubadili mitazamo yao,” alisema Hanspaul.Volvo yaingia Kenya Moja ya kampuni kubwa katika utengenezaji wa magari ya aina mbalimbali, Volvo imeingia nchini Kenya na kuwekeza Sh bilioni 2.5 za nchi hiyo ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda kinachotarajiwa kuanza na uzalishaji wa magari 500 kwa mwaka na baadaye kufikia magari 2,000 kwa mwaka.Kiwanda hicho kilichoingia ubia na kampuni ya NECST Motors ya Kenya, kinatarajiwa kuzalisha ajira 300 za moja kwa moja kiwandani hapo, lengo likiwa kushika asilimia 20 ya soko la Afrika Mashariki.Ni kiwanda cha tatu barani Afrika, vingine vikiwa Morocco ambako imeshika asilimia 20 ya soko na Afrika Kusini inakoshika asilimia 18 ya soko la magari. Kwa Kenya, kitakuwa kiwanda cha nne cha magari.Volkswagen kimeanza tena kazi baada ya kusitisha uzalishaji miaka 40 iliyopita. Kampuni za Peugeot, Toyota zimeanza pia uzalishaji, huku Iveco, Ashok Leyland pia wakitangaza nia ya kuanza uzalishaji wake nchini Kenya.Rwanda nako safi Nchini Rwanda, Volkswagen ya Ujerumani walizindua kiwanda cha uzalishaji wa magari mwaka jana, wakianza na gari madogo ya kampuni hiyo aina ya Volkswagen Passat, Volkswagen Polo na Volkswagen Teramont.Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa VW nchini Afrika Kusini inayosimamia pia kiwanda cha Rwanda, Thomas Schafer, Wanatarajia kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka, ajira zinazotarajiwa kuzalishwa ni kati ya 500 na 1,000 yakiwa ni matunda ya uwekezaji unaokadiria kufikia Dola za Marekani milioni 20.Rwanda pia kupitia Kampuni ya Pikipiki Rwanda (RMC) inatengeneza aina mbalimbali za pikipiki na tayari soko lake limeanza kukua katika nchi jirani, zikiwemo Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).RMC inatengeneza aina saba za pikipiki zikiwemo Ingenzi, Indakangwa, Indahigwa, Imparage, Infarasi na Inzovu. | uchumi |
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuongoza maelfu ya washiriki wa Rock City Marathon zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Clement Mshana, ushiriki wa Waziri Kigwangalla unaenda sambamba na ushiriki wa viongozi wengine waandamizi wa serikali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ambaye tayari amethibitisha kushiriki. “Uwepo wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya utalii kwenye mbio hizi unatokana na yeye kuunga mkono agenda iliyobebwa na mbio hizi ambayo mbali na kukuza vipaji vya mchezo huo ni kutangaza utalii hususani katika ukanda wa Ziwa kupitia mchezo wa riadha,’’alisema. Mbio hizo zilizo anzishwa miaka 10 iliyopita zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii. Aidha, zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kufanyika kwa mbio hizo, tayari wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki wameonesha kufurahishwa na zawadi zitakazotolewa kwa washindi na washiriki zikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya sh milioni 30. “Pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh mil 2 kwa washindi wa pili na sh. Milioni 1 kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi 15 watapata medali na fedha taslimu. “Kwa upande wa mbio za kilomita 21, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Sh milioni 2 kila mmoja, Sh milioni 1 kwa washindi wa pili na Sh laki 7 kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja,’’ aselima. Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates), Mshana alisema inatarajiwa kuwa zitaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ualbino, ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee. | michezo |
NI mechi ya kufa ama kupona kwa Simba inayotarajiwa kucheza na AS Vita ya Congo DR mechi ya mwisho ya kundi D kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mshindi wa mechi hiyo atafuzu robo fainali za michuano hiyo hivyo ushindi kwa yeyote ni jambo muhimu zaidi leo. Simba inatarajiwa kutengeneza historia nyingine mpya iwapo itatumia vyema uwanja huo wa nyumbani kupata matokeo baada ya kufanya vizuri katika mechi zote za nyumbani tangu kuanza kwa michuano hiyo msimu huu hatua za awali hadi makundi.Jambo la kufanya vizuri katika kila mechi ya nyumbani, ni moja ya sababu zinazoipa kiburi Simba leo ikijua kuwa inao uwezo wa kushinda mechi hiyo, hata hivyo haipaswi kujiaminisha sana kwani wapinzani wao si wa mchezo mchezo. Kwenye michuano hiyo, kundi D linaonekana kuwa gumu zaidi kwani mpaka leo timu yeyote inayo uwezo wa kusonga mvele ikishinda mechi yake.Zinahitajika timu mbili za kwenda robo fainali. Simba inashika mkia ikiwa na pointi sita, ikishinda inafikisha pointi 9 hivyo itakuwa rahisi kwake kufuzu. Katika mechi nyingine, Al Ahly ya Misri inacheza na JS Saoura ya Algeria, mechi hii nayo inatakiwa ushindi, sare yoyote itaivusha Saoura Timu zote mbili zinakutana zikiwa na rekodi mbaya ya kufanya vibaya mechi za ugenini.Je, Vita itaendeleza rekodi hiyo au itavunja uteja? Kama ni ubora timu zote mbili zinafanya vizuri kwenye ligi zao, Vita inaongoza kwao ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza michezo 23, ikishinda 20, sare mbili na kupoteza mmoja. Simba imecheza michezo 20, imeshinda 16, sare tatu na kupoteza mmoja ikiwa nyuma michezo saba ili kulingana na wengine.Utofauti wa timu hizo mbili unakuja kwenye vikosi, ambapo Simba ina wachezaji wengi wa kulipwa kutoka nje karibu 10 tofauti na Vita yenye wachezaji wanne wa kulipwa na wengine wanatoka kwao. Furaha ya wekundu hao ni kurejea kwa beki wake aliyekuwa majeruhi Erasto Nyoni. Pia, Emmanuel Okwi na Paschal Wawa waliokuwa majeruhi huku ikitarajiwa kumkosa kiungo Jonas Mkude anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano. Washambuliaji hatari wa kuchungwa pande zote mbili ni Jean Makusu wa Vita na Meddie Kagere wa Simba ambao wamekuwa waking’ara katika michezo tofauti iliyopita. | michezo |
Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba aliyetembelea Uwanja wa Ndege wa Bukoba kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja huo.Massawe alisema kutokuwepo na ushindani kunachangia wakazi wa mkoa huo kutozwa nauli kubwa.Alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa Bukoba kutafanya idadi ya abiria kuongezeka kwa hiyo pindi ikianzishwa safari nyingine kutoka ATCL jambo ambalo pia litapandisha pato la Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla .Massawe pia alisema changamoto nyingine kuwa ni suala la fidia kwa wananchi ambao walifanyiwa tathmini ili kupisha ujenzi wa uwanja huo ambapo zililipwa bilioni 1 kwa watu 18 kati ya 41 ambapo wamebaki watu 23 ambao wanadai Sh milioni 900, hivyo wamekuwa wakiibua manung’uniko ya mara kwa mara.Kwa upande wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba akitoa ufafanuzi juu ya hayo alisema tatizo la ukiritimba wa shirika moja la ndege na kupandisha nauli ovyo kutokana na kukosekana ushindani litaisha kwa kuwa ATCL wako mbioni kuagiza ndege nyingine ya CRJ ambayo itakuwa ikifanya kazi za masafa ya mbali kwa hiyo ndege iliyokuwa ikitumika katika ruti hizo itafanya safari za hapa nchini. | uchumi |
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gift Msuya amesema kuna fursa ya kuwekeza kwenye ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali na mazao yake.Amesema ofisini kwake kuwa, wanahitaji viwanda vidogo kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao la asali linalozalishwa kwa wingi kwenye wilaya hiyo.“Lakini pia kuibrand asali yetu katika ubora na kuiwezesha kufika katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Branding ni pamoja na kuispecify (kuitambulisha) kwamba hii ni asali halisi ya Uyui, lakini branding katika packanging material ya packaging, mashine za kuichuja na kuiweka katika viwango ambavyo vinakubalika kitaifa na kimataifa.”amesemaAmesema kuna jumla ya ekari 38,078 za misitu inayofaa kwa uwekezaji kwenye ufugaji nyuki ikiwemo ya kwenye kata za Kizengi, Tura, Goweko, Loya, Igalula, Kigwa, Shitage, Ndono, Uvuruma, na Sikizya.Msuya pia amesema, wanahitaji wawekezaji kwenye maeneo ya utoaji huduma vikiwemo vituo vya mafuta, benki, hoteli, masoko, vituo vya mabasi, sehemu za watu kupumzika.“Tunahamasisha watu wetu waje kuwekeza kwenye maeneo hayo kwa sababu huduma nyingi za msingi tunazipata Tabora manispaa kwa sasa” ameyasema hayo wakati anazungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo mkoani Tabora kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo.Amesema, baadhi ya kata zimeshatenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji zikiwemo za Goweko, Sikizya, Ilolangulu, Kigwa, Miyenze, Loya na Bukumbi.“Mpaka sasa Halmashauri yetu haina hata kituo kimoja cha mafuta, haina maduka, haina hoteli kwa hiyo ni hitaji kubwa ambalo tunafikiri ni muhimu sana kwa ajli ya huduma kwa wananchi wetu” amesema Msuya.Amesema, wilaya hiyo pia ina maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa ranchi za mifugo.“Wilaya mpaka sasa ina ng’ombe wapatao 441,090 lakini hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuanzisha ranchi. Maeneo makubwa yametengwa kama hifadhi kwa hiyo tunafikiria tukiazisha ranchi inaweza kuwa ni msaada kwa wakulima kwa ajili ya kuongeza lakini pia kwa Halmashauri kama chanzo kimojwapi cha mapato ya Halmashauri” amesema.Amesema, Wilaya hiyo inahitaji uwekezaji kwenye machinjio ya kisasa.“Lakini pia tunahitaji uwekezaji kwenye kiwanda cha kusindika ngozi, tuna wafugaji wengi na ngozi nyingi huwa wafugaji wakishapeleka pale ng’ombe zikichinjwa na kuuzwa ngozi huwa zitupwa au zinazikwa kwa sababu hatuna utaalamu wa kuzichakata na kuzitengeneza ili ziweze kutengeneza bidhaa nyingine. Kwa hiyo tunahitaji kiwanda cha kuiongezea thamani ngozi na bidhaa za ngozi” amesema.Amesema, kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, na kwamba, hamashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) ipo kwenye mchakati wa kuyapima na kuyapatia hati. | uchumi |
Alisema mradi huo wa nyumba unajengwa katika eneo la Iyumbu, karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma. Alisema hatua hiyo itapunguza uhaba wa nyumba za makazi na biashara katika manispaa ya Dodoma, kwa kuwa miradi mingine ya nyumba za biashara itajengwa katika eneo Meledeli.Akifafanua, Gambalagi alisema NHC itatekeleza miradi miwili ya nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri za Chamwino na Bahi ambapo zaidi ya nyumba 50 za kuuza zitajengwa katika mwaka huu wa fedha.Alisema katika kutekeleza miradi hiyo NHC itajenga nyumba za kuuza kwa zile halmashauri zitakazoonesha zina mahitaji na utayari wa kulipia au kuwepo kwa soko la nyumba zitakazojengwa.Gambalagi alisema kwa nyumba za kupangisha, shirika linaendelea kuzifanyia matengenezo makubwa nyumba zake inazomiliki katika Manispaa ya Dodoma. Alisema hivi karibuni, shirika lilibadilisha madirisha ya kizamani na kuweka madirisha ya kisasa kwenye nyumba zake zilizopo eneo Mpwapwa ya zamani na zile zilizoko barabara ya Iringa.Alisema shirika pia limesaidia vijana kwa kila halmashauri ya wilaya, mkoani hapa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana ili kuwapa ajira na kuwaondolea umasikini. | uchumi |
Rais John Magufuli amewakaribisha wananchi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waje kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo saruji, sukari, mafuta, bidhaa za chuma, na vyakula yakiwemo mahindi.Rais Magufuli pia amewakaribisha wananchi wa DRC waje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda, kilimo, uvuvi, utalii, madini nk.Amewakaribisha wananchi wa DRC kuja kuuza madini kwenye masoko ya madini nchini.'Kwa hiyo kila kitu, tunakaribishana na sisi wote ni ndugu, na kwamba, watu wa DRC waione Tanzania kama nchi yao, na Watanzania waione DRC kama nchi yao" amesema Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.Amesema Tanzania na DRC zimekubaliana kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji ili wananchi katika nchi hizo watumie fursa zilizopo."Na katika kufanikisha hilo tumekubaliana kuzihimiza taasisi zetu za kifedha hususani benki kufungua matawi kwenye nchi zetu mbili ili kuwarahishia wananchi kupata huduma za kibiashara..."Hii ni opportunity (fursa) nyingine kwa wakuu wa mabenki mbalimbali. Nakumbuka CRDB wamefungua matawi mpaka Burundi, sasa ni wakati wa kufungua matawi mpaka DRC ili kusudi kufacilitate (kuwezesha) biashara itakayokuwa inafanyika kati ya wananchi wa nchi hizi mbili"amesema Rais Magufuli.Amesema, Tanzania imeamua kuongeza muda wa kutunza mizigo ya DRC katika bandari ya Dar es Salaam kutoka siku 24 hadi 30, imeondoa katazo la ufunguaji makontena na imefuta tozo ya kusindikiza mizigo inayokwenda nchini humo.Amesema, Tanzania na DRC zimekubaliana kubadilishana uzoefu wa kutumia rasilimali ili ziwanufaishe wananchi katika nchi hizo.Rais Magufuli pia amesema, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi amekubali Tanzania ipeleke walimu wa Kiswahili nchini humo wakafundishe kwenye vyuo vikuu. | uchumi |
SERIKALI imepiga marufuku uchomaji matofali kwa njia ya tanuri kwa kutumia nishati ya kuni hasa katika maeneo ya mijini na badala yake imewataka wachomaji hao watumie pumba kama nishati mbadala.Onyo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wakati alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita ikiwa ni ziara yake kwanza ya kikazi kwa mikoa ya kaskazini magharibi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Kanyasu alisema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia upotevu mkubwa wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.Alifafanua kuwa matofali yachomwe kwa kutumia pumba za mazao badala ya kuni hali itakayosababisha kunusuru nchi kuwa jangwa huku akiagiza kamati hiyo ya mkoa huo kuanza kulisimamia agizo hilo mara moja.Alisema sehemu kubwa ya nchi kwa sasa uharibifu wa mazingira umeongezeka kutokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa matofali kwa kutumia kuni.“Mimi sipo tayari kuona nchi inageuka kuwa jangwa, ni lazima nisimamie kwa kuanza katika maeneo ya mjini ikiwemo Geita ambapo unakutana na tanuri za kuchoma matofali kwa kutumia kuni, hili sikubaliani nalo,” alisisitiza.Alisema kwa mujibu wa takwimu, Tanzania imekuwa ikipoteza zaidi ya hekta 372,000 za misitu kila mwaka. Katika hatua nyingine, Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ihakikishe inasimamia ipasavyo mipaka mipya ya baadhi ya misitu ya hifadhi mkoani Geita ambayo imehaulishwa kwa kuhakikisha imetangazwa kwenye Gazeti la Serikali.Aidha, ameutaka uongozi wa mkoa huo kutii agizo lilitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alilolitoa mwaka jana la kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka, kwa kulitekeleza ipasavyo. | kitaifa |
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars na Klabu ya Aston Villa ya England, Mbwana Samatta amewaomba mashabiki Watanzania kuacha kutoa maneno ya kashfa au yenye malengo mabaya yanayoweza kusababisha mahusiano mabovu uwanjani na wachezaji wenzake.Samatta ametoa wito huo jana kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kufuatia mashabiki wengi Watanzania kuendelea kutoa maneno hayo kwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii ya Villa kwa kuwatolea maneno makali baadhi ya wachezaji wakidai hawakumpa ushirikiano Samatta katika mechi alizocheza.Samatta alisema hafurahishwi na hali hiyo ingawa anafahamu mashabiki wanapenda afanye vizuri kwenye timu hiyo lakini anawaomba waache na kama wataendelea wanaweza kumtengenezea mazingira magumu na wachezaji wenzake.“Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye malengo mabaya na timu na wachezaji, binafsi sifurahishwi nayo,” aliandika Samatta kwenye kurasa zake.Katika mtandao huo wa Villa mashabiki wengi Watanzania wanamlalamikia mchezaji, Jack Grealish ambaye ni kiungo mchezeshaji kwenye kikosi hicho baada ya kushindwa kuonesha ushirikiano kwa kumpasia pasi za mwisho kwenye mchezo uliopita dhidi ya Bournemouth FC ambao hata hivyo Villa walipoteza kwa mabao 2-1 huku Samatta akipachika bao la kufutia machozi.Samatta awali kabla ya mchezo huo, alishatoa kauli kwa Watanzania akiwataka kuwa na uvumilivu kwenye kipindi hiki kwani amejiunga na timu mpya amekutana na wachezaji wapya hivyo anahitaji muda wakutengeneza muunganiko na maelewano mapya na wenzake.Grealish ndiye mchezaji tegemeo kwa sasa ndani ya kikosi hicho amefunga mabao saba akiwazidi wengine na kutoa pasi tano zalizozaa mabao. | michezo |
Ahadi hiyo imetolewa na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Peter Ngota. Alisema hayo alipokuwa akikabidhi zawadi za Mwaka mpya kwa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu jana jijini Dar es Salaam.TTCL ilitoa zawadi ya vyakula kwa vituo vya Kiwohede, Salvation Army na Msongola vyote vikiwa vya jijini Dar es Salaam.“Watanzania waendelee kutumia na kujiunga na huduma zetu kwa mwaka 2014,” alisema, na kuongeza kuwa wataimarisha na kuingia zaidi katika teknolojia mpya ili kukidhi mahitaji ya wateja.Alisema kampuni hiyo itaendelea kupanua huduma zake za simu za mkononi mijini na vijijini kama njia ya kutekeleza sera ya Serikali kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wote kwa maendeleo.Alisema mbali na teknolojia mpya, kampuni hiyo itaendelea kuunganisha wateja zaidi ndani na nje ya nchi katika Mkongo wa Taifa na ili kuyafanya mawasiliano kuwa ya haraka na uhakika zaidi.Kaimu Ofisa Mkuu Idara ya Fedha katika kampuni hiyo, Alinanuswe Mwakitalima mbali na kuwatakia mwaka mpya mwema watoto hao aliwataka kusoma kwa bidii ili waje kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye Stella Mwambenja, ambaye ni ofisa kutoka kituo cha Kiwohede, ambacho ni miongoni mwa vituo vilivyopata zawadi, aliishukuru TTCL akisema kuwa zitawasaidia katika kuwatunza watoto katika kituo chao.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Silvia Mulokozi, kutoka kituo cha Salvation Army alishukuru huku akiwataka watu na taasisi nyingine kuiga mfano wa kampuni hiyo ya mawasiliano.“Hatuna maneno ya kuonyesha furaha yetu…asanteni sana,” alisema. | uchumi |
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ocean Business Partners, Abdulsamad Abdulrahim wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu safari hiyo inayotarajiwa kufanyika Juni 8 mwaka huu.Alisema safari hiyo ambayo itakuwa ya siku tatu nchini humo, imeratibiwa kwa pamoja baina ya kampuni ya Ocean Business, Gallery Tours, chemba ya biashara ya Comoro na kampuni ya ndege ya ATCL ambayo imetoa punguzo kubwa la tiketi za kwenda na kurudi kwa ujumbe wa Tanzania.Alisema watakwenda kuwapa taarifa sahihi wafanyabiashara wa Comoro kuhusu fursa za kibiashara, zinazopatikana nchini ili wachukue uamuzi sahihi wa kuja kuwekeza nchini na kwamba wafanyabiashara wa Tanzania nao watapata fursa ya kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji nchini Comoro.Alisema ujumbe huo wa watu 21, utajumuisha wafanyabiashara wakiwemo wanawake kutoka sekta mbalimbali kama mafuta, gesi, mawasiliano, uzalishaji, chakula, uchapishaji, wataalamu wa baharini, ulinzi, utalii na usafirishaji, waagizaji wa bidhaa teknlojia, hoteli, afya na sekta nyingenezo.Alitaja malengo mengine kuwa ni kuelezea maendeleo yaliyopo katika sekta mbalimbali kama njia ya kwenda kuwekeza kwa kutoa elimu ya kutosha kwa sekta ya umma na ya binafsi kuhusu uagizaji bidhaa toka nje, uuzaji bidhaa nje ya nchi zao na fursa nyinginezo za kibiashara.Alisema lengo la mpango huo ni kuwahamasisha watanzania wengi kwenda kufanya biashara nchini Comoro na wale wa nchini humo kuja kuwekeza Tanzania, kwa kuwapa wawekezaji watarajiwa taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji zilizoko hapa nchini na mazingira ya uwekezaji kwa ujumla.Alisema Tanzania ina uhusiano mzuri na visiwa vya Comoro na nchi hizi zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali za kibiashara, uchumi na kijamii. Nchi hizi zina fursa mbalimbali ambazo zinaweza kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo. | uchumi |
Akitoa mada kwenye mkutano unaohusu matumizi ya sayansi na teknolojia katika kukuza uchumi wa nchi jana jijini Dar es Salaam, Mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Juma Kitima alisema vivutio hivyo vinaweza kuwa hasi au chanya.Alisema maji yanayotumika viwandani yakichujwa yanaweza kuhifadhiwa na yakatumiwa tena kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa umeme na matumizi mengine ya manufaa kwa maisha ya binadamu.Alisema miongoni mwa vivutio hivyo ni kuwasamehe ushuru wenye viwanda mara wanapoagiza mitambo hiyo ambayo alikiri kuwa gharama za ujenzi wa mitambo hiyo ni mkubwa.Alitoa mfano kuwa walifanya utafiti na wakashirikiana na kiwanda cha pombe kali cha Banana kilichoko mjini Arusha kujenga mtambo huo ambao uligharimu Sh milioni 800.Hata hivyo alisema mtambo huo ni bora zaidi na una faida kubwa kwa mwenye kiwanda na jamii inayokizunguka kiwanda hicho.Lakini pia alisema Serikali inaweza kutunga sheria kali zitakazowabana wenye viwanda na akasema kwa sasa wenye viwanda wanaendelea kuharibu mazingira kwa vile hakuna sheria inayowabana na hata kama ipo haiheshimiwi.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk Hassan Mshinda alisema mkutano huo ulikuwa unajadili mambo kadhaa kuhusu mradi ulionzishwa kati ya tume hiyo na Shirika la Maendeleo la Sweden kuona namna ambavyo sayansi inaweza kusaidia kukuza uchumi na utunzaji wa mazingira.Alisema mkutano huo pia ulikuwa na lengo la kuona namna ambavyo Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi katika kufadhili tafiti mbalimbali kwa manufaa ya jamii na akatoa mfano kuwa utafiti wa Profesa Kitima kwenye kiwanda cha Banana ni mfano wa mashirikiano hayo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Banana Investiment cha mjini Arusha Adolf Olomi, alisema kabla ya kujenga mtambo huo, kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinachafua mazingira, lakini kwa sasa mambo ni shwari.Alisema maji yanayotoka kiwandani yanachujwa tena na mtambo huo na wanayatumia kwa ajili ya umwagiliaji na wanaangalia namna ambavyo wanaweza kutumia maji hayo kuzalisha umeme utakaotumiwa na kiwanda hicho. | uchumi |
Alitoa mwito huo jana wakati akifungua semina ya siku tano juu ya mafunzo ya kuingia makubaliano na mikataba kwenye sekta ya madini kwa wanasheria wa sekta ya umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.Katika mkutano huo ulioanza jana jijini Dar es Salaam, Pinda alisema wanasheria wanapaswa kujali wananchi walio masikini kwa sababu wao hawana fursa ya kuingia kwenye vikao kama vyao na kutoa sauti juu ya kile wanachokitaka.“Licha ya umasi kini wao, wanaishi juu ya ardhi ambayo chini yake kuna utajiri tele wa madini na rasilimali nyingine. Ninawasihi sana muwafikirie watu hawa kabla ya kufanya uamuzi wowote,” alisisitiza.Alisema ili jambo hilo liweze kufanikiwa ni lazima, wanasheria kama wadau wa mwanzo kabisa, wakubali kukataa kupokea fedha chafu na vishawishi kutoka kwa wawekezaji na siku zote waweke uzalendo mbele kwa maslahi ya nchi zao.Alisema rasilimali za a Afrika hazijaleta maendeleo kwa wakazi wake kwa sababu wanaofaidika ni kampuni kubwa kutoka nje na watu wachache wenye nafasi huku walio wengi wakiambulia patupu.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, ni theluthi moja ya mikataba ya uchimbaji madini inayofaidisha bara zima la Afrika ikilinganishwa na faida ambayo bara la Amerika Kusini inanufaika nalo.Ili kuepukana na hali hiyo, Waziri Mkuu alisema umefika wakati wa kukataa kutoa misamaha ya kodi kwa kampuni za kimataifa na kuhakikisha zinalipa kodi katika kila nchi husika ya Afrika Mashariki.Alisema umefika wakati wa kuhakikisha Serikali za nchi husika zinaweka sera madhubuti na miongozo ya kisheria itakayohakikisha mikataba inayoandaliwa kwa ajili ya utafutaji na uendelezaji wa madini na rasilimali zake inazinufaisha nchi kwanza.Akimkaribisha Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema sekta ya madini ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa haraka nchini lakini inachangia chini ya asilimia moja ya ajira zote nchini. Washiriki wa mkutano huo ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania. | uchumi |
SERIKALI imenunua korosho ghafi za tani 214,269.684 zenye thamani ya Sh bilioni 717.1 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji wa zao hilo.Takwimu hizo zilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). Mdee alitaka kujua hadi sasa ni kiasi gani kimetumika kununua korosho na fedha hizo zimetoka katika chanzo kipi na tani ngapi zimenunuliwa.Mgumba alisema kiasi hicho kimenunuliwa ni kwa makadirio ya uzalishaji ya korosho msimu wa mwaka 2018/19 ambacho ni zaidi ya tani 240,000 za korosho ghafi. Alisema ununuzi wa zao hilo unafanywa na taasisi ya serikali ambayo ni Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo malipo yanaingizwa kwenye akaunti ya wakulima. Hadi Januari 30, mwaka huu, Sh bilioni 424.8 zimewekwa kutokana na mauzo ya korosho tani 134,535.4. Aidha, alisema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni taasisi ya kibiashara yenye lengo la kupata faida na mtaji wake unaotokana na ruzuku kutoka serikalini na mikopo kutoka taasisi za fedha kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), NMB na CRDB.Alisema jumla ya wakulima 390 wameshalipwa hadi kufikia Januari 30 mwaka huu. Aidha, vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa. Alisema Operesheni Korosho inatarajia kukamilika Februari 15, mwaka huu. Akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe (Chadema) alihoji kwa nini serikali iliahidi kununua korosho kwa Sh 3,300 lakini inalipa kwa Sh 2,600. Mgumba alisema ni kweli Rais John Magufuli aliutangazia umma kwamba korosho itanunuliwa kwa bei hiyo na kinachofanyika ni kwamba wakulima wanalipwa bei hiyo, isipokuwa kwa korosho daraja la kwanza. “Korosho daraja la pili wanalipwa asilimia 80 ya bei hiyo, ambayo ni sawa na Sh 2,640 na korosho za daraja la chini wanarudishiwa wakulima, kwani serikali haiwezi kulipa vigae na mawe badala ya korosho,” alisema. | kitaifa |
WAKATA miwa wa Morogoro Mtibwa Sugar wameahidi ushindi leo dhidi ya KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.Mchezo huo huenda ukawa mgumu hasa kwa Mtibwa ambao walipoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kufungwa mabao 3-0. Ili kusonga mbele katika hatua inayofuata Mtibwa inahitaji ushindi kuanzia mabao 4-0. Iwapo itapata sare au kufungwa basi itakuwa imejitoa moja kwa moja kwenye michuano hiyo. Kocha wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila alisema wana kazi kubwa ya kupambana kuhakikisha wanapata ushindi. “Tunajua kazi iliyopo mbele yetu sio rahisi, tumejipanga vizuri kusawazisha makosa yetu kwa kuhakikisha tunapambana kugeuza matokeo,”alisema.Alisema wachezaji wake wanapaswa kujitambua kwa kufanya kazi wanayoelekezwa. Mtibwa inawategemea nyota wake muhimu kama Jaffary Kibaya, Haruna Chanongo waliofunga mabao manne, katika mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Northen Dyanamo ya Shelisheli. Lakini wakata miwa hao wanahitaji kuingia kwa tahadhari kubwa dhidi ya wapinzani wao, kwani wana uzoefu wa kutosha na michuano ya kimataifa. KCCA ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri Afrika na msimu uliopita walicheza hatua ya makundi. Yeyote atakuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo kulingana na maandalizi ya kila mmoja. | michezo |
SHULE ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salam imeongoza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa wanafunzi wengi katika 10 bora kwa wasichana na wavulana na kupeleka wanafunzi wengi shule za vipaji maalumu.Hayo yalibainika jana wakati wa mchakato wa kuwapangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa Novemba mwaka huu na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kwenye matokeo hayo, shule hiyo imetoa wanafunzi saba kwenye 10 bora kwa upande wa wasichana Mkoa wa Dar es Salaam na wanafunzi watano katika 10 bora kwa upande wa wavulana.“Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa kwanza kitaifa na Tusiime kwenye wanafunzi 20 bora kwa upande wa wasichana na wavulana jumla ya inawanafunzi 12 hivyo ni dhahiri kwamba imesaidia sana kufanikisha ushindi huo wa Mkoa wa Dar es Salaam kitaifa na Wilaya ya Ilala,” alisema Mwalimu wa Taaluma, Makson Binomtonzi. Alisema shule ya Tusiime ilikuwa na watahiniwa 240 ambayo ni idadi kubwa kuliko shule zote na wote walipata alama A kwenye matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Necta.“Vile vile shule hii imeongoza Mkoa wa Dar kwa kutoa wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu nchini si jambo la bahati hili limewezekana kutokana na maandalizi ambayo huwa tunawapa wanafunzi wetu kwa kuwapa programu maalum ya masomo ya ziada,” alisema Binomtonzi. Alisema katika nafasi 28 zilizotengwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanafunzi na kwenda kwenye shule za vipaji maalumu, Tusiime imepeleka wanafunzi 16 kwenye shule hizo za vipaji maalumu na kati ya hao, watano ni wasichana na 11 ni wavulana. | kitaifa |
Kamati hiyo ilibainisha kuwa moja ya mapungufu ya mkataba huo ni pamoja na msamaha wa kodi usioeleweka, uliotolewa kwa kampuni inayotengeneza leseni hizo ya M/s Tracking Inovations LTD.Akiwasilisha taarifa ya mwaka ya kamati hiyo bungeni Dodoma juzi, Mwenyekiti wa PAC, Kabwe Zitto, alisema pia kamati hiyo imebaini kuwa mfumo mzima wa kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya leseni, hautumiki kikamilifu hasa katika uwekaji wa kumbukumbu za makosa ya barabarani.“Mheshimiwa Spika askari wa barabarani huweka kumbukumbu za makosa ya barabarani kwa kutumia makaratasi badala ya kuweka kumbukumbu hizo kielektroniki,” alisema Zitto.Alisema katika eneo la msamaha wa kodi uliotolewa kwa kampuni hiyo ya M/s, haueleweki, kwa sababu kipengele cha 14 cha mkataba huo kinamruhusu kufidia kodi anayotakiwa kulipa, wakati huo huo kwenye kipengele kinachoelezea wigo wa kazi kinabainisha kuwa bidhaa zote zitakazoingizwa na kampuni hiyo nchini kwa kwa jili ya mradi wa leseni zitakuwa na msamaha wa kodi.“Vipengele vinavyokinzana kama hivi katika mkataba vinaweza kurahisisha ukwepaji wa kulipa kodi na kuikosesha Serikali mapato, ambao pia huweza kutumiwa kwa ajili ya kuongeza muda wa mkataba,” alisisitiza.Alisema Kamati yake inaitaka TRA ihakikishe inapitia upya mkataba huo na vipengele vyenye mapungufu ili virekebishwe.Aidha, aliitaka TRA na Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha mfumo wa leseni za udereva unatumika kwa asilimia 100 ili kukuza mapato ya Serikali.“Kwa lengo la kuangalia tija iliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mkataba huo, Kamati imemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalum na kuwasilisha taarifa yake kwenye Kamati,” alisema.Aidha, alisema kamati hiyo ya PAC inapendekeza kuwa mikataba itakayohusisha utoaji wa misamaha ya kodi iwe inapitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kusainiwa. | uchumi |
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alibainisha hayo jana baada ya kikao chake na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria ,Youcef Yousfi na wataalamu wa wizara hizo mbili.Alisema hatua hizo ni kati ya miradi mingi ya ushirikiano katika sekta hizo, ambapo ujenzi wao ukikamilika utapunguza gharama kwa asilimia 45 au nusu ya gharama ya sasa.Profesa Muhongo alisema Algeria ina uzoefu katika kusindika gesi asilia ambapo kwa mwaka jana pekee ilisambaza gesi hiyo tani milioni 115 mijini na vijijini nchini humo.Alisema wamekubaliana na wataalamu kuwa ifikapo Juni 30 kwenye mkutano wa kuandaa miradi hiyo utakaofanyika Algeria, wataalamu wapeleke namna ya utekelezaji wa miradi hiyo.“Wataalamu watueleze eneo wanalopendekeza kujenga kiwanda, gharama za ujenzi, masoko ya gesi pamoja na teknolojia itakayotumika ili kufahamu gharama za uwekezaji huo,” alisema Muhongo.Alisema kutokana na kiwanda hicho, Watanzania wataachana na matumizi ya mkaa na kuni, jambo litakalosaidia uhifadhi wa mazingira.Alisema kampuni za nchi hizo zinazohusika na masuala ya gesi zitahusika katika kujengwa kwa mitambo hiyo na uendeshaji wao.Akizungumzia usambazaji umeme alisema kampuni hizo mbili zitashirikiana kusambaza umeme mijini na vijijini na kisha kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme masafa marefu.Profesa Muhongo alisema pia Algeria ina utaalamu na uzoefu mkubwa katika madini, na hivyo itaanzisha migodi ya Fosiforasi kutengeneza mbolea na kuuzwa ndani na nje ya nchi.Alisema nchini kuna aina nyingi ya madini hayo, lakini hakuna utaalamu wa kuyatumia ambapo kwa sasa inatengenezwa mbolea ya aina moja ya Minjingu. Alisema pia nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika utunzaji wa takwimu na taarifa.Waziri Muhongo alisema ili kusaidia Watanzania kuwa na wataalamu wake, Algeria inatoa ufadhili wa mafuta na gesi kwa vijana na kwa kuanzia, mwaka jana walikwenda vijana 50, mwaka huu 60.Waziri Yousfi alisema ushirikiano huo wa kiuchumi hautaishia katika miradi hiyo pekee bali itakuwa na wigo mpana zaidi.Alisema katika nchi yake yenye wananchi milioni 38 asilimia 98 wanapata umeme majumbani huku idadi kubwa ikitumia gesi kupikia.Alisema nchi yake imevutiwa kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kutokana na ushirikiano wa kisiasa uliopo kwa miaka mingi baina ya nchi hizo mbili, kuwapo rasilimali nyingi na utulivu wa kisiasa.Alisema nchi yake inatarajia kufaidika na uzoefu wa masuala ya madini ambayo Tanzania inayo huku zikibadilishana uzoefu katika masuala ya kiuchumi. | uchumi |
Timu hiyo ya Ligi Kuu iliongoza baada ya bao la Willian katika dakika ya 62 na ilionekana kuibuka na ushindi. Kross ya Christensen ndani ya eneo la hatari liliiadhibu Chelsea baada ya Lionel Messi kuunasa mpira na kuifungia Barca bao la kusawazisha ugenini.Alipoulizwa kuhusu bao hilo, bosi huyo wa Chelsea, Conte alisema: "Nadhani kiwango cha Christensen kilikuwa kizuri, tunazungumzia mchezaji ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 21 hapa”."Inafurahisha kwamba alikuwa tayari kucheza mechi hii akiwa amepevuka kiakili, nina furaha sana, alikuwa miongoni mwa wachezaji bora usiku huu (juzi)."Ni ngumu kuchagua mchezaji mmoja au mwingine lakini nadhani Christensen alicheza mechi hii kwa kiwango kikubwa, nimefurahishwa na kiwango chake”.Wakati Barcelona ikitawala mchezo, Chelsea ndio iliyotengeneza nafasi nzuri, ambapo mashuti ya Willian yaligonga mwamba mara mbili katika kipindi cha kwanza na Eden Hazard alishindwa kufunga baada ya kushindwa kujiweka pazuri."Nadhani tulikuwa karibu kwenye kucheza mchezo sahihi,” alisema Conte."Nadhani tumeadhibiwa na kosa moja, lakini kama mnavyojua kucheza dhidi ya aina hii ya wachezaji Messi, kama [Andres] Iniesta, [Luis] Suarez, kama utafanya kocha litakugharimu”."Unapocheza dhidi ya Barcelona, tunajua kwamba kama unataka kucheza dhidi yao hatua kwa hatua, mnachanganyikiwa, unapoteza mechi sio kwa 1-0 au 2-0 lakini kama kilichotekea Hispania 4-0, 5-0 au 6-0. | michezo |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wakazi mkoani hapa kuitumia kwa manufaa ziara ya Rais John Magufuli ili kuuwezesha mkoa kunufaika nayo.Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya Rais, Chalamila alisema ni wakati kwa wakazi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi katika maeneo atakayopita Rais Magufuli huku pia akihadharisha watu kutotumia fursa hiyo kuonesha mabango yenye maneno ya uchonganishi yanayoweza kuvuruga amani ya mkoa.Alisema serikali mkoani hapa haijakataza kuonesha mabango ya kero za wananchi kwa Rais, lakini ni muhimu ujumbe wa kwenye mabango ubebe ukweli wenye lengo la kuujenga mkoa na si uchonganishi.“Hatujakataza mabango hata kidogo, tunachosisitiza sisi ni watu waje na mabango yenye hoja za kweli. Wananchi wa Mbeya waitumie ziara ya Rais kuufanya Mkoa uneemeke kwa matunda mazuri baada ya ujio wake na si kuibua vilio baada ya ziara hiyo. “Niwasihi pia wananchi tushikamane kwa pamoja katika ziara hii tangu Rais atakapowasili mkoani kwetu.Tujitokeze kwa wingi kila atakakopita na pia kule atakakofanya mikutano pamoja na shughuli nyingine zilizopangwa,” alisisitiza Chalamila. Akizungumzia ratiba ya ziara ya Rais Magufuli ambaye aliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Chalamila alisema leo, pamoja na mambo mengine, Rais atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe jijini hapa.Alisema kesho ataendelea na ziara katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika miji ya Kiwira, Tukuyu na kufungua Kiwanda cha Maparachichi, kuweka mawe ya msingi katika majengo mbalimbali mapya ikiwemo mabweni katika Chuo cha Ualimu Mpuguso wilayani Rungwe na kisha atakwenda wilayani Kyela ambako atazindua barabara ya Lami ya Kikusya-Matema na kufanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale wilayani humo.Alisema keshokutwa, Rais Magufuli atakuwa katika Viwanja vya Sokoine jijini hapa katika ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mbeya, Julius Nyaisonga ambapo alitoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa nne asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama. | kitaifa |
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema wako tayari kuwakabili Simba katika mchezo wa ngao ya jamii mwishoni mwa wiki hii akiamini utakuwa wenye ushindani kwa sababu timu zote zinawakilisha kimataifa. Azam FC tayari imewasili Dar es Salaam ikitokea Ethiopia ilipopoteza kwa bao 1-0 mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya huko. Akizungumzia mchezo huo katika taarifa yake iliyotumwa na msemaji wao, Jaffar Maganga, Ndayiragije alisema wanahitaji kucheza kwa nidhamu kubwa kutokana na kuwa na jukumu kubwa la kujipanga na mchezo wa marudiano dhidi ya Waethiopia. “Mchezo wetu dhidi ya Simba ni mchezo mzuri kwa sababu timu zote zinawakilisha nchi, kutakuwa na ushindani wa hali ya juu, tunahitaji kuwa na nidhamu hasa ikitegemewa kuwa kuna mchezo wa kimataifa mbele yetu,”alisema. Ndayiragije alisema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi na kuwahimiza mashabiki wajitokeze kwa wingi kupata burudani nzuri. Simba inawakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ilicheza mechi yake ya kwanza ugenini dhidi ya UD Song ya Msumbiji na kutoka nayo suluhu ambapo mchezo wa marudiano ni Agosti 25. Akizungumzia kikosi chake, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema wachezaji wake walifanya mazoezi jana asubuhi na jioni walitarajiwa kuingia kambini Mbweni. Mara ya mwisho Simba na Azam zilikutana kwenye Ligi Kuu msimu uliopita ambapo mechi ya kwanza Simba ilishinda mabao 3-1 na mechi ya pili zilitoka suluhu. Mechi ya ngao ya jamii msimu uliopita Simba ilicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. | michezo |
Jafo ameyasema hayo leo katika kata ya Kiluvya iliyoko wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, katika ziara ya kukabidhi vifaa vya kufanyia kazi kwa wanufaika wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi (YEE).Kata nyingine ambazo wanufaika walikabidhiwa vifaa ni pamoja na Malumbo na Kurui.Mradi wa YEE ulioanza mwaka 2015 hadi 2018, umedhaminiwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) na kuendeshwa na Shirika la Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara.Kuhusu viwanda, Jafo alisema ametoa agizo kwa kila mkoa kuhakikisha unaunda viwanda 100 vinavyoanzia na mtaji wa Sh milioni 2.5 hadi 10 ili viweze kutoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla.Ametoa mfano kuwa wanufaika wa mradi huo kuwa wapo mafundi cherehani, mafundi wa kuchomelea, wapishi na wapambaji na hata mafundi umeme ambao kwa pamoja wakitumia vizuri taaluma zao wanaweza kufikia mbali na kupunguza wimbi la vijana wanaokabiliwa na tatizo la ajira.Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja mradi wa YEE, Simon Ndembeka alisema kwa wilaya ya Kisarawe mradi huo umetekelezwa katika kata tano, tayari vikundi 37 viliundwa na sasa wanakabidhiwa vifaa vya kuanzia kazi kulingana na fani walizosomea. | uchumi |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaaga watalii 1,000 waliokuja nchini kutoka Israel na kuwataka wakawe mabalozi wazuri wa Tanzania nchini mwao.Mwito huo ulitolewa jana mkoani hapa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akiaga kundi la kwanza la watalii 274 ambao ni kati ya watalii 1,000 waliowasili nchini Aprili 20 mwaka huu kutembelea maeneo ya vivutio kwenye Ukanda wa Kaskazini.Watalii hao wameondoka kwa nyakati tofauti na kwa makundi tofauti kuanzia juzi usiku hadi jana usiku.Waziri Mkuu aliwaomba watalii hao wapange muda wao na watafute fursa nyingine ya kuja Tanzania kutembelea mbuga nyingine za ukanda wa Kusini pamoja fukwe nzuri za Zanzibar.“Tumefarijika sana na ujio wenu na tunaamini mtaenda kutangaza mazuri mliyoyaona kwa wengine. Tunazo mbuga nyingine za Rubondo, Katavi, Ngorongoro, Ruaha, Selous, fukwe nzuri za Zanzibar na mlima Kilimanjaro,” alisema Waziri Majaliwa.Pia amewashukuru mawakala wa utalii nchini na Mkurugenzi wa kampuni Wakala wa Utalii ya Another World kutoka Israel, Carmel Shlomo kwa kuamua kuitangaza Tanzania kama kivutio namba moja cha utalii barani Afrika.Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliwashukuru watalii hao kwa kuamua kuitembelea Tanzania licha ya kuwa wangeweza kwenda maeneo mengine yaliyo jirani na Israel.Pia alizishukuru kampuni za utalii za Tanzania na Israeli kwa kushirikiana kuleta watalii wengi kiasi hicho. Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Excellent Guides, Mauly Tours and Safaris, Matembezi, Leopard Tours and Safaris, African Queen Adventures na TAWISA zote za kutoka Tanzania.Kamuni za kutoka Israeli ni Another World, My Trip, Camel na Kampuni ya Safari. Kwa upande wao, baadhi ya watalii kutoka Israel walisema wamevutiwa na waliyoyaona hapa nchini na wameahidi kurudi tena ili watembelee vivutio vingine zaidi.Naomi Peer Moscovich na mabinti zake, Dana na Lihi walisema wamevutiwa na wingi wa wanyama waliowaona lakini pia wameguswa na ukarimu wa watu waliokutana nao.“Tunaondoka na neno moja kubwa nalo ni kwamba hatutaisahau Tanzania (we say Unforgettable Tanzania) na tutarudi tena hivi karibuni,” alisema Dana Peer Moscovich ambaye ni dada yake Lihi. | uchumi |
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kimbunga kilichopewa jina la Kenneth kutokea katika Bahari ya Hindi.Kimbunga hicho kitaathiri huduma baharini kwa asilimia 100 na athari nchi kavu, huku kikisababisha ongezeko la mvua nchini na upepo mkali.Aidha, kimbunga hicho ambacho mpaka jana asubuhi kilikuwa kilometa 600 kutoka Pwani ya Tanzania na Msumbiji, kimekuwa kikiendelea kusogea maeneo ya Pwani ya nchi, huku kikiwa na upepo wa kasi ya kilometa 100 kwa saa.Kimbunga hicho kitaathiri maeneo mbalimbali karibu na Bahari ya Hindi hasa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na maeneo mengine ya karibu na mikoa hiyo kwa umbali wa kilometa 500.Akitoa tahadhari hiyo jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Pascal Waniha (pichani) alisema inaonesha mpaka kufikia leo, kimbunga hicho kitakuwa kilometa 200 toka mpaka wa Msumbiji na Tanzania, kikiwa na upepo wa kasi ya kilometa 100 kwa saa na kuendelea kusogea mpaka Ijumaa.Kwa mujibu wa mifumo ya hali ya hewa, inaelezwa kuwa jana kimbunga hicho kilisogea zaidi kwa kilometa 450 na kufikia usiku wa kuamkia leo kitafika kilometa 250 na kufikia kilometa 150 na upepo wa kasi ya kilometa 150 kwa saa.Dk Waniha ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi TMA, alisema katika saa 24 zilizopita, mgandamizo mdogo wa hewa uliendelea kuimarika kwa kasi hadi kufikia kiwango cha kimbunga kamili na kuwa umbali wa kilometa 700 mashariki mwa Mkoa wa Mtwara.“Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga cha Kenneth kilichopo eneo la Kaskazini Magharibi mwa Kisiwa cha Madagascar kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo,” alisema na kubainisha kuwa vipindi vya upepo mkali unaofikia zaidi ya kasi ya kilometa 80 kwa saa, vinatarajiwa kujitokeza katika Ukanda wa Pwani ya Kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na iliyo karibu.“Kimbunga hiki kitaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa nchini hivyo kusababisha ongezeko la mvua zinazoambatana na ngurumo za radi pamoja na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa Pwani,” alisema mkurugenzi huyo wa TMA.Alisema kimbunga hicho kitakapoingia nchi kavu kikiwa na nguvu inayotarajiwa, kitakuwa na madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao, ambayo ni mafuriko, uharibifu wa mali na makazi, kuezuliwa mapaa kutokana na upepo mkali, uharibifu wa mazao shambani na miundombinu kutokana na mafuriko na upepo mkali.Madhara mengine ni kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari katika kipindi kifupi, kuathirika kwa shughuli za usafirishaji kwa anga, kwenye maji na nchi kavu mkoani Mtwara na maeneo jirani ya umbali wa kilometa 500.“TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kujengeka kwa kimbunga hicho kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi pamoja na mwenendo wa mifumo mingine ya hali ya hewa kwa ujumla na kutoa mrejesho kila inapobidi ili kuchukua tahadhari zaidi,” alisema Dk Waniha.Alisema kama hiyo iliwahi kutokea mwaka 1952 katika Mkoa wa Lindi, lakini mpaka kinafika hakikuwa na madhara makubwa. Mwezi uliopita, Kimbunga Idai kilizikumba nchi za kusini mwa Afrika za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe na kusababisha vifo vya watu wapatao 1,000. Serikali ya Tanzania ilituma msaada wa chakula, dawa na vifaa tiba kusaidia watu walioathiriwa na kimbunga hicho.Mkoani Mtwara, Mwandishi Wetu, Sijawa Omary anaripoti kuwa Meneja wa Kanda ya Kusini wa TMA, Daudi Amasi amewataka wakazi waishio mabondeni mkoani humo kuchukua tahadhari juu ya tukio hilo.Alisema kimbunga hicho kitakuwa na upepo mkali, mvua kubwa itakayoambatana na radi, kuchafuka kwa bahari, mawimbi ya bahari na bahari inaweza kujaa hali ambayo inaweza kuathiri wananchi wanaoishi kando ya bahari.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Amasi alisema tahadhari kubwa inapaswa ichukuliwe kwa wakazi wa mabondeni kuhama huku maeneo yenye mifereji yakisafishwa na kuondolewa takataka ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi.Alisema tukio hilo litaanza saa tatu hadi saa tano asubuhi, na saa tano hadi saa sita, mvua itaongezeka na saa sita mvua itazidi mpaka saa tisa alasiri ambako mvua zitaanza kupungua na kisha kuondoka kuelekea nchini Msumbiji.Alisema mamlaka hiyo inaendelea kufuatilia ili kuona kama kinaweza kuongezeka nguvu na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa mabondeni ikiwemo kuezuliwa nyumba zao kutokaka na upepo mkali.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema wataalamu wameona ujio wa kimbunga Kenneth kikiwa na uelekeo wa Mkoa wa Mtwara ambacho kinaweza kuleta madhara makubwa.“Ni vizuri kuchukua tahadhari mapema kuliko kuchukua hatua za kuokoa wakati hatujui nini kitakachotokea..... watalaamu wanasema kuwa kimbunga hiki kina uelekeo wa Mtwara na kitakuja na mvua, upepo, radi,” alisema. | kitaifa |
BAADA ya ya kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia watulie, sasa makali yao watayatoa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.Kauli hiyo aliitoa baada ya timu hiyo kutua nchini ikitokea Rwanda, ambako ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa kukamilisha ratiba kwa Yanga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.Kipigo hicho kiliisaidia Rayon kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo na kuipiku Gor Mahia ya Kenya, ambayo kabla ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya wawakilishi wa Tunisia, ilikuwa katika nafasi ya pili katika kundi lao.Katika mchezo huo, Makambo alitoka katika dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na Yusuph Mhilu baada ya kupata majeraha katika mchezo huo uliojaa upinzani mkubwa.“Tunajua mashabiki wetu wanataka ushindi katika kila mechi, hivyo hilo tunalifanyia kazi kuhakikisha tunawapa furaha ili waendelee kutusapoti katika ligi, ambayo tumepanga kufanya vizuri msimu huu,” alisema Makambo.Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Zahera Mwinyi alisema majeraha ya Makambo hayana madhara makubwa, hivyo wanatarajia kuendelea kumchezesha katikamechi zijazo za Ligi Kuu.“Aliumia kwa sababu ya uwanja haukuwa mzuri kutokana na mvua, ambayo ilianza kunyesha tangu tunaanza mechi, ataendelea na mazoezi ambayo nimemuachia programu Kocha Noel Mwandila ambaye yeye ndiye atawasimamia wachezaji wote kwa kipindi hiki, ambacho mimi sitakuwa na timu,” alisema Zahera ambaye ameenda kwao DR Congo kwa majukumu ya timu yao ya taifa.Yanga imemaliza mashindano hayo ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare moja, huku ikifungwa mechi zingine nne katika kundi lake. | michezo |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda amebainisha kuwa wizara yake imeingia mkataba na Kampuni ya Suma JKT kwa ajili ya ujenzi wa ofi si za wizara hiyo katika mji wa kiserikali Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma.Mkanda aliyabainisha hao alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa wakati wa kutia saini mkataba huo. Alisema kwa mujibu wa mkataba ulioingiwa pande hizo mbili, Suma JKT wanatarajia kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo ndani ya mwezi mmoja ili wizara hiyo kuhamia rasmi katika ofisi hizo mpya.“Tumeshaingia makubaliano na wenzetu wa Suma JKT ambao ndio watatujengea ofisi zetu, na mkataba unawataka kukamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja ili sisi tuweze kuingia kwenye ofisi hizo mpya,” alisema.Profesa Mkenda alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa agizo la Rais kutaka Dodoma kuwa makao makuu na wizara zote kuhamia jijini hapa wizara imeingia mkataba wa muda mfupi na SUMA JKT ili kukamilisha majengo ya ofisi.Aidha, alisema kuwa kwa kipindi ambacho watumishi wa serikali kupitia wizara hiyo ambao wamehamia Dodoma kwa sasa wanafanya kazi katika ofisi ambazo zipo barabara ya polisi na wengine wakiwa katika majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).“Pamoja na kuwa kwa sasa tunafanya kazi bila kuwa na majengo ya kutosha lakini kazi zinafanyika vizuri na kwa ushirikiano mzuri huku tukiwa tunasubiria kupata ofisi ya uhakika ambayo itajengwa na Suma JKT katika mji wa kiserikali Ihumwa jijini hapa.Aliongeza: “Ninaamini kuwa iwapo tutakaa katika jengo moja la ofisi na watumishi kufanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri zaidi na wenye tija kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla.”Aidha, Profesa Mkenda alisema kuwa mkataba huo wa muda mfupi ni ujenzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la awali. “Mkataba huu wa muda mfupi imelenga kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa ofisi ambapo litajengwa jengo kwa ajili ya ofisi na baadaye awamu ya pili ya ujenzi jengo kubwa la ghorofa ambalo wakurugenzi wote na viongozi watahamia hapo.” Hivi karibuni serikali imetoa takribani Sh bilioni 1 kwa kila wizara ili kuhakikisha inajenga jengo la wizara katika mji wa serikali uliopo Ihumwa nje kidogo ya jiji la Dodoma. | kitaifa |
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa anatamani wilaya hiyo iwe kitovu cha utalii nchini Tanzania.Amesema, Bagamoyo ina vivuto vingi vya utalii vinavyohitaji uwekezaji mkubwa zikiwemo hoteli.“Yaani hiyo ndiyo ndoto yangu. Ndoto yangu kubwa sana ipo kwenye kuifanya Bagamoyo kuwa kitivo cha utalii”amesema ofisini kwake mjini Bagamoyo.Amesema fukwe za Bagamoyo bado hazijawekezwa kikamilifu, na kwamba, maeneo ya kihistoria wilayani humo ni fursa nzuri kwa uwekezaji.Zainabu ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na kongamano hilo.“Maeneo ambayo naweza kusema hayajaguswa kikamilifu ni kwenye maeneo ya fukwe ambako tunaweza tukawa na hoteli za kitalii kwa sababu kwa ujumla Bagamoyo ina vivutio vingi sana vya kitalii ambavyo vinahitaji uwekezaji mkubwa” amesema.Zainabu amesema fursa ya utalii kwenye fukwe za Bagamoyo inahitaji uwepo wa hoteli na kwamba hata kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani hakuna hoteli za kutosha.“Lakini pia fukwe zetu za bahari bai hazijaendelezwa, zinahitaji kuendelezwa. Lakini pia kwenye sekta ya uvuvi na kwenyewe pia, uchumi wa Bagamoyo unategemea sana uvuvi”amesema. Amesema Serikali imetoa shilingi bil 1.6/- kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la samaki hivyo kuna fursa ya kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha samaki.“Kwa hiyo nawakaribisha wawekezaji wanaopenda kuja kuwekeza Bagamoyo, ardhi bado tunayo nzuri kabisa yenye rutuba katika maeneo mbalimbali. Tunavyo viwanda zaidi ya sitini vikubwa, vidogo na vya kati. Na vile vidogo kabisa sijavitaja kabisa hapo”amesema. | uchumi |
WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa siku sita kwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumpa taarifa ya kina kwa nini hawajachukua Sh bilioni 50.9 zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi.Jafo aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema iwapo uongozi huo utashindwa kutoa maelezo ya kina, fedha za mradi huo zitapelekwa kwenye halmashauri nyingine zikafanye shughuli za maendeleo.Alisema mradi huo wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi umetengewa fedha nyingi ambayo ni Sh bilioni 50.9, lakini anashangazwa ni kwa nini mpaka sasa unasuasua. Awali mradi huo ulipangwa kuanza Julai mwaka 2017 lakini mpaka sasa haujaanza.HabariLeo ilimtafuta Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana kuhusu suala hilo alisema, “Kuna mambo ya ndani ambayo yanakwamisha, ila mchakato bado unaendelea, tutampelekea taarifa kumjulisha hili, kuna mambo ya ndani ambayo sitaweza kuyaweka wazi.”Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda hakuweza kupatikana kuzungumzia kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi, kutokana na simu yake kuita bila kupokewa, hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukujibiwa. | kitaifa |
ASASI isiyo ya kiraia ya Alliance For Democratic Organization (ADO) imewapongeza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa huku ikiwataka baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani kuheshimu maamuzi hayo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo Habib Mchange, alisema kupitishwa kwa Muswada huo ni hatua kubwa kwa siasa za Tanzania na zaidi wanachama wa vyama hivyo na wananchi kwa ujumla. Alisema anaamini hatua hiyo italeta mabadiliko makubwa na hasa katika kuweka uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya siasa na kuondoa kila aina ya ubabaishaji aliodai umekithiri ndani ya siasa za Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.“Kwa dhati kabisa niwapongeze wabunge wote waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha muswada huu unapita ili uweze kuleta mabadiliko ya kweli katika siasa za Tanzania tukiamini kuwa sote lengo letu ni moja kuijenga nchi hii,” alisema Mchange. Aidha alisema endapo Muswada huo utasainiwa na Rais na kuwa sheria, mapendekezo yake kwa serikali ni kwamba isiishie kubadili vipengele vilivyomo ndani, bali inapaswa iende mbali na kuwachukulia hatua watu wote watakaokwenda kinyume na sheria husika. | kitaifa |
KATIBU Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF), Hussein Swaleh ni miongoni mwa watu 157 waliokufa katika ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka juzi asubuhi ikitoka Addis Ababa kwenda Nairobi.Swaleh alikuwa akirejea kutoka katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Ismail ya Misri na TP Mazembe ya Congo DR zilizocheza mjini Cairo, Misri, Ijumaa iliyopita, Swaleh akiwa kamishna wa mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholaus Musonye alisema jana, Baraza lake limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mdau huyo na kuiombea faraja familia yake pamoja na wakenya kwa ujumla.Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo la ndege, watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikufa. Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kulikuwa na watu kutoka mataifa 33 katika ndege hiyo iliyoanguka dakika sita baada ya kuruka kutoka kwenye Kiwanja cha Addis Ababa, Ethiopia. Ndege hiyo ilianguka saa 2:44 kwa saa za Ethiopia, ikiwa ni dakika sita baada ya ndege hiyo kuruka katika mji mkuu huo wa Ethiopia. | michezo |
['Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)', 'Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)', 'Mchezaji wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)', 'Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany - in German)', 'Sane anakabiliwa na uwezekano wa kupoteza £11m katika mshahara wake iwapo ataendelea kukataa kutia kandarasi mpya na Man City . (Sunday Mirror)', 'Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anapima uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco na beki wa Bournemouth Nathan Ake, 24. (Sunday Express)', 'Manchester United wamefanya mazungumzo ya kubadilishana wachezaji na Juventus ambapo mchezaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, na mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic wataelekea Old Trafford, huku naye mchezaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, akielekea Juventus. (Sunday Times - subscription required)', 'Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anataka kumsaini beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33 kwa mkopo wa miaka miwili. (Sun on Sunday)', 'Barcelona inajiandaa kuanza mazungumzo na PSG kuhusu kumununua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, back to La Liga. (Goal.com)', 'Kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa manchester United ameambia klabu ya Sporting Lisbon kwamba anataka kujiunga na Tottenham. (Mail on Sunday) ', 'Real Madrid wameafikia makubaliano na mchezaji mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uholanzi Donny van de Beek, lakini bado hawajakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo na klabu yake Ajax. (Marca)', 'Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anapanga kumnunua beki wa Norway Kristoffer Ajer, 21 kwa dau la £21m. (Star Sunday)', 'Barcelona wameafikia makubaliano na Real Betis kumsaijili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 Junior Firpo kwa dau la £22m. (ESPN)', "Burnley have joined Crystal Palace in the race to sign Real Betis' Spanish midfielder Victor Camarasa, 25, who spent last season on loan at Cardiff City. (Sky Sports)", 'Tottenham imejiandaa kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Ryan Sessegnon, 19, kutoka Fulham, lakini huenda ikamkosa kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 na Real Betis Giovani lo Celso kwa hatua hiyo. (Star Sunday)', 'Hatahivyo Spurs wanapigiwa upatu pamoja na Atletico Madrid kumsaini beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter, 25 kwa dau la £60m. (Bild, via 90min)', 'Tottenham wako tayari kushinda na Roma pamoja na Juventus kumsajili beki wa kulia wa napoli na Albania Elseid Hysaj, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Chelsea msimu uliopita (Sunday Express)', 'Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anasema kuwa atamuomba mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuongeza wachezaji zaidi kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho siku ya Alhamisi na anasema kwamba anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Dwight Gayle, 28, kusalia katika klabu hiyo licha ya hamu kutoka klabu ya Leeds..(Newcastle Chronicle)', 'Leicester wameripotiwa kumlenga beki wa Getafe na Togo Djene Dakonam, 27, kujiunga na klabu hiyo ili kuchukua mahala pake beki wa Uingereza ambaye anataka kujhiunga na Man United Harry Maguire, 26. (Leicester Mercury)', 'Chelsea wako tauari kusikiliza ofa ya kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, na Uingereza Danny Drinkwater, 29. (Sunday Telegraph)', 'Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza Drinkwater anatakiwa na klabu ya Brighton kwa mkopo msimu huu. (Mail on Sunday)', 'Beki wa kushoto wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, 22, huenda akakosa hadi wiki nane kupitia jeraha na hivyobasi kumaliza hamu ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya £25m (Sun on Sunday)', 'Mshambuliaji wa manchester City ambaye ni raia wa Ujerumani Lukas Nmecha, 20, atahudumu msimu 2019-20 kwa mkopo katika klabu ya Bundesliga ya bWolfsburg. (Manchester Evening News)', 'Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)', 'City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)', 'Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26. (Independent)', 'Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo,mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)', 'Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba nae. (Telegraph)', 'Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)', 'Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min)', 'Liverpool wanapima uwezekano wa kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Bordeaux na Guinea Francois Kamano na wako tayari kumgaramia kwa pauni milioni 20 kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Sun)', 'Tottenham wanauangalia mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa mchezaji wa Real Beti -Giovani Lo Celso, mwneye umri wa miaka 23. (Evening Standard)', 'Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 30.07.2019 ', 'Betis wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC - in Spanish)', 'Kiungo wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo.(Sun)', 'Newcastle wanakaribia kusaini mkataba na winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin,mwenye umri wa miaka 22, kutoka Nice katika mkataba wa pauni milioni 16.5 . (Talksport)', 'Mchezaji wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Dani Alves anakaribia kuhamia Sao Paulo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36- yuko huru baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Goal)', 'Crystal Palace wamefany amawasiliano na Cardiff City kumuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor Camarasa mwenye umri wa miaka 25'] | michezo |
UUNGANISHAJI maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kwa mkopo umeshika kasi katika maeneo mbalimbali huku mamlaka ikisema inakwenda hatua kwa hatua na wakazi wote jijini watapata maji.Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na chaneli ya TBC One ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kila Alhamisi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja ameifafanua utaratibu unaopaswa kufuatwa ili kupata maji hayo ya mkopo.Akijibu maswali ya mtangazaji ikiwamo la kutaka kufahamu utaratibu unaopaswa kufuatwa na watu walio mbali na umbali ulioidhinishwa kuunganisha wateja chini ya mradi kuepuka vishoka, Luhemeja alisema mwananchi anatakiwa kuwa na fomu ya utambuzi kutoka serikali ya mtaa.Amesema mwananchi akifika ofisi za Dawasa anapaswa kupewa mkaguzi wa eneo lake na umbali unaoruhusiwa ni meta 50 kutoka kwenye bomba na kuongeza kuwa kama mteja yuko umbali zaidi ya hapo, inabidi wapeleke bomba la inchi mbili au tatu ili kuingiza wateja wengine.Akizungumzia hatua za kupata mkopo, alisema wakishafanya ukaguzi na kila mmoja akapata gharama ya kuunganishiwa maji, huduma ikipatikana wanaandikishiana mkataba unaomwezesha kulipa kwa awamu kwa miezi sita mpaka miezi 12.Akizungumzia maeneo yenye mabomba yasiyotoa maji na yale yasiyo na mabomba, Luhemeja alisema mradi huo wa usambazaji maji haujafikia asilimia 60. Ofisa mtendaji huyo alisisitiza kuwa wananchi hawahitaji kupata huduma kupitia watu wa kati ambao katika miaka takribani minne iliyopita, walikuwa wakitapeli.Kwa mujibu wa Luhemeja, gharama ya kulipa maunganisho ya kwanza ni kati ya Sh 200,000 na Sh 350,000 kulingana na umbali jambo ambalo ilikuwa mzigo kwa baadhi ya watu kulipa kwa mkupuo.Chini ya utaratibu huo wa kukopesha wateja, Dawasa imetekeleza kwa vitendo agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alilotoa Novemba mwaka jana wakati akizindua mradi wa maji wa Kiwalani.Alitaka Dawasa kuhakikisha inaunganisha wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba walipe kidogo kidogo kwani malengo ya serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.Katika hatua nyingine, Luhemeja alizungumzia kuhusu mita za maji za kabla ya matumizi kama zinazotumiwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kusema majaribio kwa wateja wakubwa 11 yamekamilika na mwaka ujao wa fedha zitaandaliwa mita 1,000.Baada ya muda watapeleka huduma hiyo majumbani. Akizungumzia wanaolimbikiza madeni, ofisa huyo mtendaji alisema wateja wa Dar es Salaam sasa wako vizuri katika kulipia ankara zao.Kwa mwezi, Dawasa ina wastani wa ankara kati ya Sh bilioni 11 mpaka 12 na inakusanya takribani Sh bilioni 11.2 sawa na asilimia 90.Amesema hivi karibuni walizindua kampeni ya ‘Tunawahitaji’ kwa ajili ya wananchi waliokatiwa maji kwa muda mrefu na hawana uwezo wa kulipa. Wamewaita na kuingia nao mkataba hivyo wakilipa ankara za sasa, wanalipia na asilimia ndogo ya zamani.Amesema wakilipa miezi sita na Dawasa ikaridhia, itafuta madeni yaliyobaki na kusisitiza kuwa huduma ya maji haipaswi kuwa vita, hivyo ni lazima iwe rafiki kwa sababu ni huduma ya watu. | kitaifa |
WABUNGE wamesema Bajeti ya mwaka 2019/20 ni ya ushindi kwani imejibu kilio cha Watanzania kwa kuondoa kodi na tozo chechefu.Wakizungumza na gazeti hili katika viwanja vya Bunge jana baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kusoma bajeti kwa saa 2, wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao walisema bajeti hiyo ni ya ushindi kwa Watanzania.Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengelwa (CCM) alisema bajeti hiyo ni ya ushindi kutokana na kwamba imejibu vilio vya Watanzania kwa kuondoa tozo na kodi ambazo zilikuwa kero katika kufanya biashara nchini.“Bajeti hii ni ya ushindi kwa sababu imesikiliza vilio vya wananchi kwa kuwaletea nafuu katika maisha kwa kuondoa tozo mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwasumbua na kama ikiekelezwa kwa asilimia 100 itakuwa mkombozi mkubwa kwao,” alisema.Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni amesema bajeti hiyo ni ya wananchi kutokana na kwamba imezingatia matakwa makubwa na mahitaji ya wananchi kwa kuondoa kero za kodi na tozo ili kuendesha biashara na shughuli mbalimbali za maendeleo.“Mazingira ya kibiashara yameboreshwa na Bluu Print iliyoandaliwa kwa ajili ya kuboresha mazingira hayo itakuwa suluhusho kwa kufanya biashara na kuboresha biashara zao,” alisema.Alisema bajeti hiyo imeongezeka kwa takribani Sh bilioni 666 ukiliganisha na ya mwaka jana lakini imejikita katika kuendeleza na kutekeleza miradi mikubwa yenye maslahi mapana kwa taifa.Dk Chegeni alisema lakini pia imejikita katika kupunguza utegemezi wa wafadhili kutoka nje na kubakia asilimia nane tu ya bajeti, lengo ni kufikia azma ya nchi kujitegemea katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.Alisema kodi na tozo katika kilimo na mifugo na sekta nyingine nyingi ambazo zilikuwa zikisumbua wananchi zimeondolewa lengo ni kuwaondolea umasikini wananchi.Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola (CCM) alisema bajeti hiyo imewakumbuka wafanyabiashara nchini kwa kuondoa kodi na tozo ambazo zilikuwa zikiwasumbua katika kufanya biashara zao.Alisema kitendo cha kuondoa tozo na kodi mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na mifugo kutaleta nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa wananchi kwa ujumla.Alisema bajeti hiyo imeangalia mahitaji ya wananchi kwa kuangalia maradi mikubwa ya maendeleo na kuhakikisha mradi hiyo inakamilishwa ikiwemo ya umeme, reli ya kisasa na masuala mbalimbal jamii kama elimu afya na huduma nyingine.Alisema bajeti hiyo imelenga kutatua kero za wananchi kwa kutenga fedha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya huduma za jamii ikiwemo maji, umeme, afya na elimu.“Lakini pia bajeti imetenga fedha kwa ajili ya makandarasi kukamilisha miradi ya mbalimbali kutokana na kutengewa fedha kwa ajili ya miradi hiyo,” alisema.Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda alisema kwamba bajeti iyo ni jibu la kilio cha wananchi kutokana na kuondoa kodi na zoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwasumbua. Mbunge wa Malindi Ally Salehe (CUF) alisema bajeti ni nzuri katika kuondoa kodi na tozo ambazo zilikuwa zikiwasumbua wafanyabiashara nchini.Alisema katika kutekeleza bajeti hiyo kinachotakiwa ni serikali kusimamia makusanyo na kutekeleza miradi ya kitaifa ambayo ndiyo italeta maendeleo, lakini wanatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya kijamii.Mbunge wa Longido, Dk Steven Kiluswa (CCM) alisema bajeti ya wananchi kutokana na ukweli kwamba imeangalia kero kubwa kwao ya kodi na hivyo kuindoa na tozo mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwasumbua wananchi.Alisema kuondolewa kwa kodi hizo, kunalenga kuwezesha wananchi katika kufanya shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo.Waziri Mpango amesoma mapendekezo ya serikali ya bajeti kuhusu makadirio ya mapatona matumizi na kuomba bunge lipitishe bajeti ya Sh trilioni 33.11 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo.Akizungumza baada ya bajeti hiyo kusomwa Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema, wabunge watakuwa na muda wa kujadilia mapendekezo ya serikali kuhusu bajeti hiyo na hatimaye kuipitisha kwa kupiga kura kila mbunge. | kitaifa |
KAMANDA wa Polisi Mkoa (RPC) wa Dodoma, Gilles Muroto amewataka viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa, kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini wao katika suala la ulinzi na usalama kwenye kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Alitoa ushauri huo alipozungumza na viongozi wa madhehebu ya dini katika kikao cha pamoja kuhusu hali ya usalama katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya. Alisema kuwa viongozi wa madhehebu ya dini, wanayo nafasi kubwa ya kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini juu ya suala la ulinzi na usalama na maeneo yao yakawa salama na amani.“Jeshi la polisi kwa kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na waumini wakiwa kitu kimoja, kuna asilimia kubwa ya kuwepo kwa salama kwa kipindi hiki cha tunachoendea sikukuu,” alisema.Kamanda huyo alitoa tahadhari kwa waumini katika kipindi hiki cha sikukuu, kujiwekea ulinzi wa kutosha kwenye maeneo yao wanayoishi Kamanda huyo aliwataka viongozi hao wa dini, kuhakikisha nyumba zao za ibada wanafunga kamera, ambazo zitasaidia kudhibiti ulinzi wa maeneo yao.Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya dini ya Kikristo Mkoa wa Dodoma Askofu Damas Mukassa, alilipongeza jeshi hilo la polisi kwa kuwatambua viongozi wa dini kwenye mchango wao wa kushirikiana suala la ulinzi na usalama.Alisema viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na waumini wanaowaogoza, watashirikiana na jeshi hilo muda wote katika suala la ulinzi na usalama, bila kuangalia kama kuna sikukuu. Alisema moja ya majukumu ya viongozi wa dini ni kuhakikisha usalama unakuwepo. Alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama, vipo kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo. | kitaifa |
SERIKALI imeombwa kuhakikisha kila kiwanda kinachozalisha mafuta ya alizeti kinakaguliwa na kupewa alama ya ubora ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo na kuleta usawa kuhimili ushindani.Rai hiyo ilitolewa mjini hapa na baadhi ya wazalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka viwanda vya kati na vikubwa waliodai wao walikaguliwa na mamlaka husika kabla ya kupatiwa alama ya ubora wa bidhaa wanayozalisha na waliingia gharama kubwa kukamilisha hilo na wanalipia kila mwaka alama ya ubora. Walidai waliingia gharama kubwa kupata alama ya ubora, wenye viwanda vidogo hawana alama hiyo kwa kuwa hawajawahi kukaguliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wala Shirika la Viwango (TBS) hali ambayo haileti usawa wa ushindani kibiashara.“Kuna ushindani usio sawa kutokana na kuwepo kwa mafuta yasiyokaguliwa wala kuthibitishwa ubora wake na TFDA au TBS. Hii inaathiri viwanda vikubwa ambavyo hutumia mamilioni ya fedha katika kujiendesha,” alisema Meneja wa Masoko wa Mount Meru Millers mjini Singida, Nelson Mwakabuta.Mzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka kiwanda cha Kati cha Singida Fresh, maarufu kama “ Kilimo Kwanza”, Jamal Shaban aliisihi serikali kusimamia kikamilifu suala la kila kiwanda kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa bidhaa zake ili walaji waweze kupata mafuta yasiyochakachuliwa. Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Dk Engelbert Bilashoboka alisema jukumu la kusimamia ubora wa mafuta ya alizeti yanazozalishwa na viwanda vidogo lipo kwa Halmashauri za wilaya, miji au manispaa.Katibu Mtendaji wa Chemba ya Wakulima, Wafanyabiashara na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoa wa Singida, Culvert Nkurlu alisisitiza umuhimu wa kuvilinda viwanda vidogo na kuwatia moyo wamiliki wake viwanda hivyo vidogo viweze kukua akikariri usemi kuwa “mbuyu nao ulianza kama mchicha.” Kutokana na alizeti kuwa moja ya zao kuu la biashara Singida, mkoa sasa una viwanda 140 vya alizeti, kimoja kikubwa, vya kati na vidogo vinavyotumia mbegu za zao hilo ili kuzalisha mafuta ya kula. | kitaifa |
SERIKALI imetoa ufafanuzi na kukanusha madai, yaliyotolewa hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya kimataifa kwamba Tanzania imekataa kuruhusu uchapishaji wa ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuhusu hali ya kiuchumi ya Taifa.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema jana bungeni kwamba hakuna sehemu ambayo imezuia, bali kinachoendelea ni mazungumzo ambayo ni sehemu ya utaratibu wa chombo hicho cha kimataifa. Dk Mpango (pichani) alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya suala hilo kuzungumziwa na Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema) wakati akichangia hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.“Kwa hiyo wasiwahishe mjadala, serikali bado inazungumza na IMF na hakuna sehemu ambayo imezuia, ni utaratibu wa IMF yenyewe,” alisema Dk Mpango katika ufafanuzi wake. Awali, katika kuchangia hotuba hiyo iliyotolewa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe mwishoni mwa wiki akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/20, mbunge huyo alisema Tanzania hakuna uhuru wa habari na kusema serikali imezuia IMF kuwasilisha taarifa yake.Kabla Spika Job Ndugai kumuomba Waziri Mpango kutoa ufafanuzi, mbunge huyo alisema amepata taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba IMF imesema inatakiwa iruhusiwe na Tanzania ichapishe taarifa ya uchumi wa nchi, lakini serikali imewazuia. Baada ya hoja hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aliingilia kati kwa kuomba utaratibu chini ya Kanuni ya 64 (1) (a) inayosema mbunge hatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.Akimtaka mbunge huyo kufuta kauli au kuthibitishia Bunge kama taarifa na ripoti aliyo nayo ni sahihi, Jenista alisema wanachojua ni kwamba kinachoendelea ni mazungumzo na si kweli Tanzania imezuia ripoti hiyo isitolewe. “Alichosema Mwakajoka ni kwamba Tanzania imewazuia IMF; IMF inaomba kibali halafu imezuiwa na Tanzania isichapishe hiyo ripoti,” alisema Spika Ndugai na kumuomba Waziri wa Fedha na MIpango kufafanua juu ya hilo.Waziri Mpango alisema katika majadiliano yanayoitwa Article 4 Consultants, timu ya IMF ilikuwa nchini kuanzia Novemba 2018 mpaka Desemba 2018 na baada ya hapo, ilitoa taarifa. Alisema kwa utaratibu, wakitoa rasimu ya taarifa, inarudi serikali ili iweze kuitolea maoni na wao waweze kuyazingatia kabla ya kuchapisha ripoti husika. Waziri alisema hiyo ripoti alikuja kuiona Machi 18, mwaka huu.“Na hiyo ripoti baada ya kuwa sisi tumepeleka maoni yetu, maoni hayajazingatiwa kwenye taarifa na nilipokuwa Washington juzi, nilizungumza na mkurugenzi wa African Department na mpaka leo saa 9 bado tutaendeleza majadiliano kuhusu jambo hili,” alisema. Aliendelea kusema, “na kwa utaratibu ni kwamba baada ya Executive Board ya IMF kuijadili hiyo taarifa, serikali inakuwa na siku 14 za kuipitia na kusema itolewe au isitolewe.”Alisisitiza mjadala usiwahishwe, kwa kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na hakuna sehemu ambayo IMF imezuiwa. Hivi karibuni, suala hili lilisambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo va habari vya kimataifa, vikidai serikali ya Tanzania imekataa kuruhusu uchapishaji wa ripoti ya IMF kuhusu hali ya kiuchumi, huku baadhi ya vyombo vikitafsiri kwamba hatua hiyo huenda ikaathiri uwekezaji na misaada kuingia nchini. | kitaifa |
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amesema elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo wa taarifa za mikopo ili kuwawezesha Watanzania kupanga matumizi bora ya mikopo.Profesa Luoga alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma kuhusu taarifa za mikopo na fedha, iliyoratibiwa na BoT kwa kushirikiana na International Finance Corporation (IFC), ambayo ni moja ya taasisi za Benki ya Dunia.Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Philip Mpango, Prof Luoga alisema taarifa za mikopo na elimu ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha Watanzania wanaondokana na matumizi ya anasa ya mikopo.“Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini,” alisema.Meneja Msaidizi wa Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina alisema kampeni hiyo ya miezi mitatu, inalenga kuongeza uelewa, mwamko kuhusu taarifa za mikopo na kukuza upatikanaji wa mikopo.”Kaulimbiu katika kampeni hiyo ni: “Pata Taarifa Yako ya Mikopo Leo. Angalia hali yako ya kifedha ili kupanga mustakabali wako bora wa kesho” inaungwa mkono na wadau mbalimbali katika sekta ya huduma za fedha.“Wadau hao wameahidi kusaidia kusambaza ujumbe kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa mikopo na jinsi Watanzania wanavyoweza kuishi maisha bora kwa kuweza kupata taarifa za mikopo yao na kujua historia ya mikopo yao,” amesema.Alisema usimamizi mzuri wa mikopo na historia nzuri ya mikopo ni muhimu katika kuwezesha kupata mkopo nafuu."Kuhakiki taarifa yako ya mikopo mara moja kwa mwaka ni huduma inayopatikana bila malipo, tena itakuletea mafanikio kwa kukuandaa vema utakapoenda kuomba mkopo."Historia nzuri ya mikopo inaweza kusaidia kustahili viwango vya chini vya riba na ada, hivyo kuondokana na kutenga fedha kwa ajili ya dharura na gharama zisizotarajiwa," amesema.Alisema mikopo inasaidia kupata mahitaji ya sasa, kama vile nyumba au ada ya shule kwa watoto, kwa kuzingatia ahadi ya kulipa kwa awamu na kwa muda uliopangwa.Meneja wa IFC Tanzania, Manuel Moses amesema taarifa ya mikopo inaonesha taarifa binafsi, utambulisho na taarifa ya mawasiliano na ikiwezekana historia ya ajira, idadi na aina za akaunti za mikopo.Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Dun & Bradstreet, Josephine Temu alisema kwa sasa kuna taasisi mbili zilizopatiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania kuandaa na kutoa taarifa za mikopo Tanzania, ambazo ni Creditinfo Tanzania Limited na Dun & Bradstreet.Alisema taasisi hizo zinakusanya na kutunza taarifa za mikopo na kutoa taarifa za mikopo kwa kampuni au watu wanaozihitaji kama vile benki.Alisema ripoti hiyo ya mikopo, inaweza kutolewa na taasisi hizo mara moja kwa mwaka bila malipo.Akifafanua kuhusu mambo muhimu ya kuangalia kwenye taarifa ya mikopo, Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Creditinfo, Tonny Missokia amesema muhimu ni taarifa binafsi kama vile jina, ndoa, anwani, taarifa za ajira na namba za mawasiliano ni sahihi. | uchumi |
Kimbunga Kenneth kikiwa na kasi ya 220 kwa saa (220km/h) kimelikumba eneo la kaskazini mwa Msumbuji usiku wa kuamkia leo, Ijumaa.Hata hivyo serikali ya nchi hiyo haijaripoti kutokea madhara kwa binadamu baada ya kupita kimbunga hicho. Kimbunga hiki kimetokea nchini humo ikiwa ni wiki sita tu zimepita tangu Msumbiji ikumbwe na kimbunga kingine kilichojulikana kwa jina la Idai na kusababisha mamia ya vifo huku maelfu wakikosa makazi na huduma muhimy baada miundombinu kuharibiwa.Msemaji wa Taasisi ya Udhibiti wa Majanga nchini humo (INGC), Paulo Tomas ameeleza kuwa tayari serikali imewahamisha watu 30,000 kutoka eneo hilo la Kaskazini.“Zoezi la kuhamisha watu kutoka maeneo hatari kwa kimbunga hiki litaendelea hadi watakapokuwa maeneo salama, na tuna mahitaji yatakayosaidia watu 140,000 kwa siku 15,” aliongeza. Taarifa za utabiri wa hali ya hewa ziliitaja Tanzania na Msumbiji kuwa ni miongoni mwa nchi zitakazokumbwa na kimbunga hicho. Hata hivyo, serikali katika miko iliyoonekana itakabiliwa na kimbunga Kenneth ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma ilichukua tahadhari mapema kwa kuwashauri watu kuhamia maeneo salama. Mamlaka mkoani Lindi iliamua kuahirisha tukio la maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kitaifa kwa hofu ya kutokea kimbunga hicho. | kitaifa |
HALMASHAURI ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma, imetoa mkopo wa Sh milioni 112.2 kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu, hivyo kufi kia lengo la kutoa mikopo isiyo na riba kwa asilimia 100 kwa mwaka 2018/19.Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Grace Quintine alisema katika awamu ya kwanza Desemba, mwaka huu, zilitolewa Sh milioni 25 kwa vikundi 10 vya wanawake na vijana ambapo wanawake walipata Sh milioni 13.7 na vijana Sh milioni 11.3.Alisema awamu ya pili mikopo ilitolewa Machi, mwaka huu, kwa vikundi saba vya wanawake, vijana na walemavu ambao walipatiwa Sh milioni 14.5, kati ya hizo wanawake walipata Sh milioni nane, vijana Sh milioni nne na wenye ulemavu Sh milioni 2.5.Kwa mujibu wake, awamu ya tatu vikundi tisa vilipata mikopo ambayo ilitolewa Mei, mwaka huu na jumla ya Sh milioni 21 zilitolewa, wanawake walipata Sh milioni 10 na vijana Sh milioni 11. Quintine alisema katika awamu ya nne walifanikiwa kutoa mikopo ya Sh milioni 24.9 na awamu ya tano na ya mwisho kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyoishi Juni 30, wametoa Sh milioni 26.Alisema mikopo iliyotolea imeleta mafanikio makubwa kwa vikundi hivyo ikiwemo kuanzisha biashara, wana vikundi kupata elimu ya ujasiriamali, uzoefu na kuongeza kipato cha familia. Aidha, alisema halmashauri ya mji Mbinga iliweka lengo la kukusanya Sh bilioni 1.1 ya mapato yake ya ndani, lakini imevuka lengo baada ya kufanikiwa kukusanya Sh bilioni 1.2 na mafanikio hayo yametokana na kazi kubwa iliyofanywa na watumishi wa ngazi zote katika halmashauri hiyo.Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye, alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji kwa namna alivyosimamia suala la ukusanyaji mapato yake ya ndani kwa asilimia 100.Hata hivyo, aliagiza kuanzia sasa vijana wote wanaomaliza mafunzo ya mgambo kuhamasishwa kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kama njia ya kukabiliana na ukosefu wa ajira pindi wanapomaliza mafunzo yao. Mmoja wa wana kikundi cha walemavu, Theresia Kapinga aliishukuru serikali kwa kupitisha sheria inayotaka kila halmashauri hapa nchini kutenga asilimia mbili kwa walemavu. | kitaifa |
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba Leo watakuwa na kibarua kigumu ugenini cha kusaka pointi tatu muhimu wakati watakapowakabili wababe wao, Kagera Sugar katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini hapa. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote kutokana na viwango bora vya timu hizo baada ya kila moja kushinda michezo yao yote iliyopita na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 20. Kagera hadi sasa ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote tatu ilizocheza ugenini hadi sasa ilipozifunga Biashara United, Alliance FC, na Mbao FC wakati Simba nayo ikishinda mechi zake mbili Mbele ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar na kuwafanya kuwa na pointi sita.Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema jana kuwa katika kipindi cha wiki mbili alikuwa akikinoa kikosi chake ili kuhakikisha kinaondoka na pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kurejesha heshima mbele ya wapenzi wa soka.Alisema pamoja na kuwakosa wachezaji wake, Michael Gadiel Mbaga pamoja na kiungo wa juu, Clatous Chama katika kikosi cha wachezaji 22, wanatarajia matokeo chanya katika mchezo huo.Nyota 22 waliotarajia kuondoka jana asubuhi kwenda Bukoba ni pamoja na Aishi Manula, Beno Kakolanya, Pascal Wawa, Tarone Santos, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yassin, Francis Kahata, Sharaf Shiboub na Hassan Dilunga.Wengine ni Meddie Kagere, Kennedy Juma, Yusuph Mlipili, Haruna Shamte, Rashid Juma, Said Ndemla, Jonas Mkude, Miraj Athuman, Deo Kanda, Ibrahim Ajib, Wilker Da Silva na Erasto Nyoni.Kwa upande wake, kocha wa Kagera, Macky Mexime alisema maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba yamepewa kipaumbele kama michezo mingine ya ligi hiyo waliyokwishacheza, huku Serikali ya mkoa wa Kagera ikiwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kuishanglia timu yao ikicheza dhidi ya Simba.Mexime alisema pamoja na Simba kupania kupata ushindi timu yake haiwezi kukubali kirahisi kupoteza mchezo huo wa kwanza nyumbani, baada ya kuanza kwa ushindi ugenini kwa kushinda mechi zote tatu. | michezo |
['Arsenal wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, lakini si kwa Manchester United ama Liverpool. (90min.com)', 'Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, ameiomba klabu yake ya Crystal Palace imruhusu ahamie Arsenal. Palace inamthaminisha streka huyo streka huyo kuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Mirror)', 'Manchester United wanamini kuwa wataweza kukamilisha usajili wa kuwanasa Sean Longstaff, 21, kutoka Newcastle na Bruno Fernandes, 24, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno. (Evening Standard)', 'Real Madrid watalazimika kulipa kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili kiungo Mfaransa Paul Pogba 26, kutoka Manchester United. (Mirror)', 'Gareth Bale yawezekana akasilia na Real Madrid baada ya klabu hiyo kushindwa kumpata mnunuzi anayemtaka winga huyo mwenye miaka 29. (Mirror)', 'Chelsea wanampango wa kumtangaza Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kabla ya wachezaji kurudi mpaumzikoni wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. plan to announce Derby. (Sun)', 'Liverpool wamefikia makubaliano na Sporting ada ya usajili ipatayo pauni milioni 7 ili kumnunua mshambuliaji kinda Rafael Camacho, 19. (Evening Standard)', "Kumefanyika mkutano baina ya viongozi wakuu wa Atletico na Real Madrid juu ya usajili wa usajili wa mshambuliaji Antoine Griezmann, 28, kuelekea dimba la Bernabeu. (L'Equipe - in French)", 'Streka wa Colombia Radamel Falcao, 33, anataka kujiunga na timu inayomilikiwa na David Beckham nchini Marekani Miami pale mkataba wake watakapofiki tamati na klabu ya Monaco. (Sun)', 'Aston Villa wapo tayari kutuma maombi ya kutaka kumsajili beki wa Southampton Matt Targett. (Express and Star)', 'Kocha wa West Brom Slaven Bilic anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani klabuni hapo Julian Dicks kujiunga naye kama sehemu ya benchi la ufundi.. (Express and Star)', 'Manchester United inafikiria kumnunua beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 23, anasalia kuwa mchezaji anayelengwa sana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich msimu huu licha ya mpango huo kusita hapo awali. (Sky Sports)', 'Mkufunzi wa klabu ya Sporting Marcel Keizer anaamini kwamba nafasi ya kumzuia kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandez katika klabu hiyo ni ndogo, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zimevutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Record, via Manchester Evening News)', 'Babake mshambuliaji wa Juventus Moise Kean, 19, ametangaza kwamba raia huyo wa Italia anataka kuhamia Inter Milan. (Mirror)', 'Atletico Madrid inafikiria kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombian James Rodriguez, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa hahitajiki tena Real . (Cadena SER, via AS)', 'Naibu mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola ataondoka Chelsea wikendi hii wakati ambapo kandarasi yake itakuwa inakamilika baada ya kukataa ofa ya kuwa balozi wa klabu hiyo. (Guardian)'] | michezo |
Akizungumzia katika warsha ya kitaifa ya wadau ya sekta ya kilimo inayofanyika Dar es Salaam yenye mada kuu ya “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi, alisema ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.Samkyi alisema, ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo, Serikali iliamua kuanzisha TADB kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo.“Katika kutekeleza majukumu yetu, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Samkyi.Kwa mujibu wa Samkyi, benki hiyo inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani.Mikopo mingine ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamba hadi upatikanaji wa masoko, alisema. Aliongeza kuwa, wamejipanga kutoa mikopo ya ununuzi wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao, ikiwamo fedha za kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao.Akizungumzia mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo, Robert Pascal alisema, benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili, mikopo ya muda wa kati ya miaka miwili hadi mitano, na mikopo ya muda mrefu.Marejesho yanaeleweka kuwa ni kati ya miezi 60 hadi 180. Aliongeza kuwa, riba inayotozwa kwa upande wa mikopo ya muda mfupi ni asilimia saba mpaka nane kwa mwaka, ambayo mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani. | uchumi |
ZAIDI ya Sh milioni 430 zimeingizwa kwenye mzunguko wa fedha wa mjini Iringa kupitia mikopo iliyotolewa na Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SIFA Saccos Ltd) kati ya Januari na Septemba mwaka huu. Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Emmanuel Magoda alisema kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika mjini Iringa hivi karibuni, kwamba mikopo hiyo imetolewa ili kusaidia ukuaji uchumi, kuchangia pato la Taifa na kuchochea ajira katika sekta binafsi. Magoda alisema kati ya kiasi hicho, Sh milioni 223 zimetolewa kwa ajili ya mikopo ya biashara, Sh milioni 184 mikopo ya walaji na zaidi ya Sh milioni 17 mikopo ya dharura, Sh milioni saba mikopo ya mshahara, na Sh 500,000 mkopo wa kilimo. “Tuna imani waliopata fedha hizo hawakuzichimbia ardhini, waliziingiza kwenye mzunguko wa fedha katika mji wetu wa Iringa hatua itakayosaidia kuchochea maendeleo,” alisema Magoda. Akizungumzia mafanikio ya Saccos hiyo yenye wanachama zaidi ya 900, alisema mpaka Septemba mwaka huu, walikuwa na hisa zenye thamani ya Sh milioni 131.6, akiba yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 156.9 na amana ya zaidi ya Sh milioni 67.3 na akiba maalumu ya Sh milioni saba. Alisema SIFA Saccos Ltd imeendelea kuendeshwa kwa faida licha ya hali ya uchumi kubadilikabadilika hatua iliyowawezesha wanachama wake kufaidika kwa kupata faida juu ya akiba na amana zao.Alitaja mafanikio waliyopata kuwa ni pamoja na kupokea maombi ya wanachama wapya 105 na kumaliza kulipa mkopo waliokopa kutoka Mradi wa Kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF). | uchumi |
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe ametoa mwezi mmoja kwa Bodi ya Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), kuzifuta tozo zote zisizo za kisheria za shughuli za usafi rishaji wa mizigo bandarini ili kuiwezesha bandari hiyo kuwa na ushindani wa kibiashara dhidi ya bandari nyingine.Aidha, ameitaka bodi hiyo kuchapa kazi kwa juhudi zote ili kuwezesha upatikanaji wa mapato na kuisaidia bandari kutimiza malengo yake na pia kukuza uchumi wa Taifa na kuchangia maendeleo.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya TASAC jijini Dar es Salaam jana, Kamwelwe alisema kimsingi kumekuwa na tozo mbalimbali zinazotozwa kwa wasafirishaji wa mizigo bandarini huku baadhi zikiwa hazitambuliki kisheria na hivyo kukwamisha utendaji kazi mzuri wa bandari hiyo.Alisema ili kuhakikisha bandari hiyo inatoa ushindani dhidi ya bandari nyingine, kuna kila sababu kwa bodi hiyo mpya kupitia tozo zinazotozwa bandarini hapo na kujiridhisha na uhalali wake na kuziacha tozo zilizopo kisheria ambazo sehemu ya mapato yanayotokana nazo yanaingia katika mfuko wa serikali.“Wakati huu ninapoizindua bodi hii naomba mkahakikishe mnaenda kufanya kazi kwa juhudi, lakini kubwa ni kuziondoa tozo zote mzigo na zisizo na manufaa na hili mkalisimamie kikamilifu mkishindwa baada ya siku thelathini nitaita vyombo vya habari na kutangaza kuzifuta,” alisema Waziri Kamwelwe.Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Profesa Tadeo Satta, mbali na kumshukuru Rais John Magufuli kwa uteuzi huo, alisema bodi hiyo inakwenda kutekeleza majukumu yake kwa weledi huku akimuahidi waziri kuwa wanaenda kuchapa kazi kwa ari ili watimize malengo yaliyokusudiwa na serikali ya sasa.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko alisema kuzinduliwa bodi hiyo ni hatua muhimu kuiwezesha TPA kutimiza malengo yake kwa ufasaha kutokana na umuhimu wa chombo hicho katika usimamizi wa meli na mizigo inayoingia na kutoka bandarini.Kakoko alisema kwa kipindi kirefu kuna shughuli katika bandarini zilizokuwa haziendi ilivyotakiwa kutokana na kutokuwepo kwa chombo hicho hatua iliyosababisha baadhi ya shughuli kuzorota huku akisisitiza umuhimu wa kila taasisi zinazofanya kazi katika bandari hiyo kutekeleza majukumu yake.Alisema kama taasisi zote zinazofanya kazi ndani ya bandari hiyo zitafanya kazi zao bila kuzembea, kuna mafanikio makubwa yanayoweza kujitokeza katika bandari hiyo na kulisaidia Taifa kutimiza malengo yake mbalimbali ya kimaendeleo iliyojiwekea ikiwemo ya elimu, afya na ujenzi wa miundombinu. | kitaifa |
SERIKALI iko katika hatua ya mwisho ya makubaliano na Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Kuimarisha Milki za Ardhi ikiwa ni katika kuhakikisha ardhi inatumika kwa tija. Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwenye wizara yake kwa mwaka 2019/20. Wizara imeomba kupitishiwa bajeti ya Sh bilioni 62.69 kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 ambapo zaidi ya Sh bilioni 27.3 zikitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku ikiweka lengo la kukusanya Sh bilioni 180. Katika hotuba yake alisema ifikapo Agosti mwaka huu, Mkoa wa Dar es Salaam utaanza kutoa hati za kielektroniki hii ni baada ya kukamilisha ufungaji wa mfumo kwenye halmashauri zote za manispaa ya mkoa huo. Alisema programu hiyo ambayo awali ilikuwa itekelezwe kwa mwaka wa fedha 2018/2019 itakuwa ni nyenzo muhimu katika kuleta mageuzi sekta ya ardhi ikiwamo kuondoa na kudhibiti migogoro ya matumizi ya ardhi miongoni mwa watumiaji, kupanua wigo wa mapato ya serikali na kuhakikisha ardhi inatumika kwa tija. Alisema pia kwa mwaka mpya wa fedha NHC, inaendelea na mikakati endelevu ya kuuza nyumba za makazi na linatarajia kujenga nyumba 1,000 katika jiji la Dodoma. Aidha, Lukuvi alisema imeandaa mfumo maalumu wa kieletroniki utakaowezesha kutoa leseni za makazi zinazotambulika kisheria kwa kutumia simu janja ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na matapeli wa ardhi. “ Mfumo huo utawezesha urahisi kwenye utambuzi wa vipande vya ardhi mijini pamoja na taarifa za wamiliki na umeanza kutekelezwa katika jiji la Dar es Salaam na utaendelea kutumika nchi nzima. Hadi kufikia Mei 15 mwaka huu, vipande vya ardhi vya matumizi mbalimbali 150,000 vimesajiliwa.” Lukuvi alisema mfumo huo utawapa wananchi uhakika wa miliki zao na kuwezesha ardhi zao kutumika kama mtaji wa kiuchumi na kwa mwaka wa fedha 2019/20 wizara yake inakusudia kusajili hatimiliki na nyaraka za kisheria 152,000. Aidha, Lukuvi alisema Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) linakuja na mfumo wa ‘Mpangaji Mnunuzi’ ili kuwezesha wananchi wa kada mbalimbali kumiliki nyumba za makazi. Lukuvi alisema katika kipindi cha utekelezaji wa bajeti hiyo, wizara itatekeleza kazi mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya TEHAMA ya utunzaji kumbukumbu na kuboresha taarifa za ardhi.Alisema kazi nyingine ni kurahisisha ukadiriaji kodi ya pango la ardhi na tozo zitokanazo na sekta ya ardhi kwa kutumia vifaa vya kieletroniki vinavyohamishika. Lukuvi alitaja majukumu mengine ambayo wizara imepanga kuyatekeleza ni kuhakikisha watu wote wa mjini wenye nyumba na ardhi isiyopimwa wanarasimishwa na kupewa hati na leseni za makazi.Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mjumbe wa Kamati hiyo, Shaban Shekilindi kamati iliipongeza serikali kwa kubuni mradi wa kujenga nyumba 1,000 kupitia Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) kwa ajili ya makazi jijini Dodoma ambalo ni makao makuu ya nchi.Kwa upande wa maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, msemaji wa kambi hiyo kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wlifred Lwakatare, upinzani unaamini katika mfumo wa umiliki ardhi ambao kila mwananchi atamiliki ardhi na rasilimali zake juu na chini ya ardhi hiyo. | kitaifa |
HALMASHAURI ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, imepata mwekezaji wa kiwanda cha mawese ambaye tayari amewasilisha barua ya kuanza kununua malighafi za zao hilo.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Masumbuko Kichego amesema hayo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk. Geoffrey Mkamilo aliyoifanya katika Mkoa wa Kigoma ikiwa ni ufuatiliaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu upandaji wa mbegu bora za zao hilo.Amesema kupatikana kwa mwekezaji huyo kutaongeza tija kwa wakulima wa zao hilo kwa kuwa watakuwa na sehemu ya kupeleka mazao yao baada ya kuvuna.“Kupatikana kwa mwekezaji huyu wilaya itakuwa na connection nzuri kwa kuwa tayari tuna mbegu za kisasa, kuna mkulima anazalisha mbegu za kisasa, kuna mnunuzi anayenunua hapahapa ambaye ataipeleka ku process hiyo product kwa hiyo chain itakuwa imekamilika,” amesema.Kichego ameiomba TARI iongeze kasi ya kuzalisha mbegu kwa kuwa wana maeneo mengi ya kupanda michikichi.Amesema mbali na kupata miche 35,000 kutoka TARI kabla ya hapo walinunua miche 3,000 kutoka taasisi binafsi ya Seed Change inayozalisha mbegu bora ya Tenera ya michikichi iliwagharimu zaidi ya sh. milioni 10/- na kwamba, gharama hiyo ilikuwa ni kubwa kwao.Kwa mujibu wa Kichego wanajipanga kuwapa wakulima miche ya michikichi itakapokuwa tayari kwa lengo la kuinua uchumi wa mkoa huo kwa kupunguza uagizaji mafuta ya kula nje ya nchi.Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Michikiki Kihinga mkoani Kigoma, Dk. Filson Kagimbo amesema kituo hicho kinafanya utafiti wa zao la mchikichi kwa kuwa kilimo hicho nchini kina changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mbegu za kisasa aina ya Tenera.“Wakulima zaidi ya asilimia 90 wanalima mbegu ya kienyeji inayoitwa dura ambayo inatoa mafuta kidogo kulinganisha na mbegu ya kisasa aina ya tenera.“Hizi mbegu za kisasa aina ya tenera upatikanaji wake ni kama asilimia 10 na za kienyeji ni asilimia 90 hivyo kituo kimeweka kipaumbele cha kuzalisha mbegu nyingi za kisasa ili kisambaze kwa wakulima waweze kuzilima,” amesema.Ametaja changamoto nyingine ni kuzeeka kwa miti ya zao hilo kwani mingi ina zaidi ya miaka 50, lakini uzalishaji wenye tija unatakiwa miti iwe na miaka minne mpaka 30.“Sasa miche mingi ina zaidi ya miaka 50 na mingine mpaka miaka 100 inapofikia umri huo uzalishaji unakuwa mdogo sana kinachotakiwa hivi sasa wakulima waing’oe hiyo ya zamani na kuipanda mipya,” amesema.Amesema jitihada za kufufua zao hilo zinafanyika ili kupunguza uagizwaji wa mafuta ya kula nje ya nchi kwa kuwa michikichi inatoa mafuta mengi kwa eka ikilinganisha na mazao mengi yanayozalisha mafuta.Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk. Mkamilo anafanya ziara mkoani Kigoma kuangalia uzalishaji wa zao hilo umefikia hatua gani tangu Waziri Mkuu Majaliwa alipotoa agizo la kupanda mbegu za kisasa.Kwa mujibu wa Dk. Mkamilo awali kulikuwa na upotevu mkubwa wa fedha za serikali kutokana na mafuta ya kula kuagizwa nje ya nchi, na kwamba, TARI imeanza kuzalisha kwa wingi mbegu hizo wakisaidiana na kampuni binafsi ili kuondoa changamoto hiyo kwa taifa. | uchumi |
SERIKALI imesitisha safari za ndege kwenda nchini Afrika Kusini mpaka wajiridhishe kwa maandishi kuhusu usalama wa abiria na ndege kutokana na vurugu zinaozendelea nchini humo.Aidha, serikali imetangaza kuwa mwezi Novemba wataingiza nchini ndege mbili aina ya Bombardier na Dreamliner huku wakikamilisha manunuzi ya ndege mpya mbili aina ya Airbus.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amebainisha hayo wakati akizindua rasmi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwa mamlaka kisheria kutoka kuwa wakala na kubainisha kuwa baada ya ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa Afrika Kusini kuwasili juzi jioni Dar es Salaam.Kamwelwe alisema ndege hiyo kwa mujibu wa ratiba ilitakiwa leo kufanya safari yake Afrika Kusini, lakini wamesitisha kutokana na fujo zinazofanywa na vijana hivyo hawawezi kupeleka abiria na chombo hicho kwani hawaamini usalama wao.“Tutasitisha kwa muda mpaka tutakapopata mawasiliano ya maandishi kutoka Serikali ya Afrika Kusini kuhusu usalama wa abiria na chombo chetu,” alisema waziri huyo.Alisema wanafanya utaratibu kuhakikisha abiria watapelekwa kupitia ATCL kwa kutumia ndege nyingine kwa lengo la kulinda safari za ndege hiyo kwenda Afrika Kusini ili isipotee.Amesema baada ya kurejea kwa ndege hiyo iliyokuwa ikishikiliwa imefanyiwa uchunguzi kwani ilikaa kwa siku zaidi ya nane na imebainika haina matatizo itaendelea na ratiba ya safari zake kama kawaida.Alisema kutokana na changamoto hiyo, kulitokea kuathirika kwa safari kwa baadhi ya maeneo, lakini sasa zimekaa sawa wakati serikali ikijiandaa kupokea ndege mpya Novemba mwaka huu.Akizungumzia sakata la kukamatwa kwa ndege na maamuzi ya serikali, alibainisha kuwa baada ya hukumu kutolewa na ndege kurejea nchini wanasheia wanaendelea kushughulikia hukumu iliyotolewa ili aliyeshtaki anatakiwa kulipa gharama na wataendelea kutoa taarifa. | uchumi |
MKUU wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla ameshauri mkoa wa Tabora kuanzisha dawati maalumu litakalotumika kutoa taarifa zote muhimu za fursa za uwekezaji ziwasaidie watu wenye nia ya kuwekeza kuchagua maeneo kulingana na vipaumbele vyao.Makalla alitoa kauli hiyo hivi karibuni mkoani Tabora alipokaribishwa kushiriki na kufungua mkutano wa maandalizi ya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao.Amesema ni jukumu la dawati hilo kunadi vitu muhimu ambavyo ni vya kipekee vinavyopatikana mkoani humo vinavyoweza kuwa fursa kwa wawekezaji kuanzisha viwanda, hoteli za kitalii na ufugaji wa kisasa.Alisema hatua hiyo iende sanjari na kila wilaya mkoani humo kuainisha maeneo ya kipekee yanayofaa kwa uwekezaji na ikiwezekana yapimwe.“Kwa mfano mnaweza kusema kwa sababu Sikonge wana misitu mingi hapo panafaa kujenga kiwanda cha kusindika na kuchakata asali, Igunga wanazalisha pamba kwa wingi kijengwe kiwanda cha kuchambua pamba na nyuzi zake, Nzega kuna ng’ombe kijengwe kiwanda cha ngozi na kusindika nyama, Urambo wanalima sana tumbaku kijengwe kiwanda cha tumbaku na Kaliua kijengwe kiwanda cha unga,” alishauri. | uchumi |
WASANII wa fani tofauti na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii watafanya ziara kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC).Mratibu wa safari hiyo, msanii wa filamu Steve Mengele 'Nyerere' ameupongeza uongozi wa TRC kwa kutambua mchango wa wasanii katika jamii na kuwapa fursa.Nyerere amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kufanikisha safari hiyo itayojumuisha waimbaji wa muziki wa bendi, bongo fleva, taarabu, singeli, waigizaji wa filamu, bongo movie, komedi, wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu na waandishi wa habari wa vyombo wakiwemo wa mitandao ya kijamii.Wasanii na waandishi wa habari wameelezwa jijini Dar es Salaam kuwa, safari hiyo itaanza saa moja asubuhi kwa treni ya TRC kutoka eneo la Kamata jijini Dar es Salaam na kupitia maeneo yote ambayo mradi huo unatekelezwa.Wakati wa safari wahandisi wa reli watakuwa wakitoa maelezo kuhusu ujenzi wa mradi huo mkubwa.Nyerere pia amewaeleza wasanii kuwa, kuna mikopo inayotolewa kwa wasanii kupitia Halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam kutekeleza sera ya Serikali inayoziagiza mamlaka hizo kutenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vijana, walemavu na wanawake.“Mkuu wa Mkoa Paul Makonda anakaribisha maombi ya mkopo kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa mkutano wa wasanii wa maigizo waimbaji wa muziki wa bendi, bongo fleva, taarab, singeli, waigizaji wa filamu, bongo movie, komedi , wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu na waandishi wa habari nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi na kukuza kipato kwa tasnia zote nchini.” amesema Nyerere.Kaimu Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TRC Jamila Mbarouk amesema safari hiyo ni fursa kwa wasanii na waandishi wa habari kwenda kuona mradi wa ujenzi wa SGR unavyotekelezwa.Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku spidi yake ikiwa ni kilomita 160 kwa saa.“Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii ,wacheza mpira, ma MC ,waimbaji, wachekeshaji, waigizaji wa filamu na wengine ambao wanaweza kuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma kuhusu mradi huo wa treni mpya ya umeme itakayotoka Dar es Salaam -Morogoro hadi Dodoma ” amesema Mbarouk.Amesema, reli hiyo inajengwa kwa fedha za Watanzania kutokana na kodi. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwani mradi huo ukikamilika utasaidia kukuza uchumi pia kwa wafanyabiashara kwa kusafirisha bidhaa zao na mizigo kwa haraka zaidi. | kitaifa |
Kati ya Sh milioni 300 za kila siku katika promosheni hiyo, mtu mmoja atakuwa anajishindia Sh milioni 100, watu kumi kila mmoja atapata Sh milioni 10, wengine 100 kila mmoja akipata Sh milioni moja na wengine 15,000 wakipata muda wa maongezi wa Sh 1,000 kila mmoja.Akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa alisema promosheni ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom na kwamba; “Kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”Alisema ili kushiriki katika promosheni hiyo, mteja yeyote wa Vodacom, anapaswa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la.Kila SMS itagharimu Sh 300. Katika uzinduzi huo, Balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daudi `Zembwela’ ambaye kutokana na promosheni hiyo anajulikana kama ”JayMillions” alikuwa kivutio, akiuliza maswali wageni waliohudhuria na kuwapatia fedha taslimu waliojibu vizuri kuhusiana na ushiriki wa promosheni hiyo. | uchumi |
KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo katika kilele cha Wiki ya wananchi (Kubwa Kuliko) imepania kupita mtaa kwa mtaa na kufanya matamasha mbalimbali kupitia wasanii wa muziki na maigizo.Yanga inataka kuwatumia wasanii ambao ni wapenzi wa klabu hiyo kurudisha hamasa kwa mashabiki wake.Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wanataka wakusanye kijiji kupitia burudani hizo zitakazoenda sambamba na utoaji zawadi mbalimbali kwa wananchi.“Wanayanga wajiandae pindi tutakapofika mitaani kwa burudani kutoka kwa wasanii pamoja na zawadi kibao zitatolewa, hakika watafurahia kile tunachotarajiwa kukifanya,” alisema.Mipango hiyo ya mtaa kwa mtaa inatarajiwa kufanyika kuanzia wiki ijayo lengo ni kuwapa burudani wananchi kuelekea katika kilele Agosti 4, mwaka huu.Alisema mbali na burudani wanazotarajia kutoa, watafanya shughuli nyingi za kijamii na hivi karibuni watatangaza watakapoanzia.Hii itakuwa ni mara ya kwanza Yanga inatumia ushawishi wa kiburudani wa mtaa kwa mtaa kuhamasisha wapenzi na mashabiki wake kuhusu yajayo.Mwakelebela alisema wanataka kutumia burudani hiyo ya muziki na michezo ya kirafiki kukutana pamoja na kufurahia, kujenga ushirikiano kitu ambacho huko nyuma hakijawahi kutokea. | michezo |
WATAALAMU na wadau wa malezi na makuzi ya mtoto wamehimiza wazazi kuzungumza na kumjengea mtoto upendo na ukaribu tangu akiwa tumboni ili kumuandaa kwa makuzi bora kiakili, kihisia na kimwili. Kupitia mradi wa Malezi kwa Makuzi ya Mtoto unaotekelezwa na Shirika la kimataifa la Elizabeth Glasser Pediatric AIDS (EGPAF) mkoani Tabora, imeelezwa kwamba tangu akiwa tumboni ambako ndipo ubongo huanzia kukua hivyo ni rahisi kunasa mawasiliano. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na timu ya watendaji wa EGPAF waliotembelea wilayani hapa, wataalamu na wadau wa afya walipongeza mradi huo kuelimisha wazazi na walezi juu ya makuzi yanayozingatia afya na maendeleo ya kisaikolojia hivyo kuwahakikishia watoto haki ya kuishi na kukua. Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji Nzega, Mariam Michael alisema mradi umesaidia kwa kiwango kikubwa kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa watoto waliokuwa katika hatari ya kutofikia hatua za makuzi, baada ya wazazi kuelimishwa mbinu mbalimbali. Alisema chini ya mradi huo unaotekelezwa kwa awamu ya pili kuanzia mwaka jana hadi mwakani, miongoni mwa elimu inayotolewa ni kuhusu wazazi kushiriki malezi ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa kuzungumza na kucheza nao. “Baadhi ya familia, unaweza kukuta baba na mama wana malumbano tangu mtoto akiwa tumboni na ikamuathiri mtoto anayezaliwa…unakuta mtoto ni mnyonge, hataki kucheza na kuchangamana,”alisema Michael. | kitaifa |
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba, Maji, Nishati, Salama Aboud Talib amesema vyanzo vya maji safi na salama vilivyopo Zanzibar vipo katika hatari ya kutoweka kutokana na tabia ya wananchi kuvamia na kujenga nyumba za kudumu.Salama alisema hayo wakati akifanya majumuisho na kujibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20. Alisema kitendo cha uvamizi na kujenga katika maeneo ya vyanzo vya maji ni hatari na kinatishia kukauka kwa vyanzo hivyo.Alivitaja baadhi ya vyanzo vya maji ambavyo vipo katika hatari ya kutoweka ni pamoja na Mwanyanya ambayo ni maarufu kwa uzalishaji mkubwa wa maji yanayotumika katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.‘’Hiki chanzo cha maji safi na salama kilichopo Mwanyanya Mkoa wa mjini Magharibi Unguja kipo tangu enzi za ukoloni, kinaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa maji safi na salama, lakini kimeanza kupungua kutokana na kasi ya ujenzi wa nyumba,’’ alisema. Alivitaja baadhi ya vyanzo vya maji safi na salama ambavyo vimetoweka kutokana na tabia ya wananchi kujenga nyumba za kudumu karibu na vyanzo hivyo ni Bububu, Kiyanga na Masingini Unguja.Alizitaja juhudi zinazochukuliwa kwa sasa na Mamlaka ya Majisafi na Salama(ZAWA) ni kujenga uzio katika vyanzo hivyo ili kuzuia uvamizi na matukio ya aina hiyo. Alisema ujenzi wa uzio wa chemchemi ya Mwanyanya upo katika hatua nzuri na unasubiri mkandarasi kwa ajili ya kazi hiyo.‘’Ujenzi wa ukuta wa chanzo cha maji cha Mwanyanya upo katika hatua nzuri, tunasubiri mkandarasi kwa sasa lakini baadhi ya visima kama vile Matuleni na Ngwachani tumefanikiwa kujenga uzio,”alisema.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/20 ya Sh bilioni 156.582 kwa kazi za kawaida na maendeleo.Alisema mafanikio ya wizara yapo katika utekelezaji wa sera ya maji ya mwaka 2004, Sheria ya maji ya mwaka 2006, pamoja na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umasikini (MKUZA 111) na Dira ya Maendeleo ya 2020 na malengo endelevu ya SDGs. | kitaifa |
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema, Rais John Magufuli alifanya uamuzi mgumu kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme kwenye Bonde la Mto Rufiji.Amesema mjini Kibaha kuwa, mradi huo utakaozalisha megawati 2,115 ni miongoni mwa miradi ya kimkakati itakayokuwa na matokeo makubwa kwenye ujenzi wa sekta ya viwanda na nyingine.Ameitaja miradi mingine kuwa ni kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya, na kujenga reli ya kati ya kisasa.“Ni miradi ya kimkakati kweli kweli maana sio lele mama hata kidogo” amesema Pinda mjini Kibaha wakati anafunga maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani.Amesema mradi wa kuzalisha umeme kwenye bwawa la Nyerere unamfurahisha, una hadithi ndefu na kulikuwa na maneno mengi kuhusu gharama na uharibifu wa mazingira.“Utafikiri la kwao, sasa bwana mkubwa alipoingia pale akawasikiliza akasema ninyi watu wa ajabu sana, kwa nini msihangaike na ya kwenu huko mnafuata ya kwangu. Wataalamu wakamuelimisha vizuri akakuta kumbe hata kule kulalamikia kwamba kunaharibu ni asilimia ndogo sana ya pori lile la Selous, ndogo sana, akasema mimi naendelea, ni mradi wa Watanzania, najua manufaa yake ni nini. Na mradi ule unaenda na amedhamiria utakwisha”amesema Pinda.Amesema mrai huo ukikamilika viwanda vitakuwa na uhakika wa umeme na amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliofanya. | uchumi |
Msemaji wa TDU, Geofrey Willis, ameeleza kuwa kwa mwongozo huo wawekezaji watapata habari wanazohitaji kuhusu sekta ndogo ya faida za uwekezaji, motisha za uwekezaji na dhamana na habari ya vitendo kuhusu kuanzisha biashara nchini Tanzania.Sekta ndogo ya viwanda vya nguo, huwapatia wawekezaji fursa bora ya kutumia uwezo wake mkubwa, lakini ambao unatumiwa chini ya kiwango.Alisema kuwa serikali ya awamu ya nne, ina jukumu la kusaidia katika sekta ndogo. Tanzania inatoa ulinzi zaidi wa ushindani nafuu na uwekezaji wenye kuaminika.Tanzania ina kanda mbili kubwa za uzalishaji pamba, ambazo ni Eneo la Magharibi la Uzalishaji Pamba (WCGA), ambalo linahusisha mikoa saba ya Shinyanga, Mwanza, Tabora, Mara, Singida, Geita na Simiyu.Mikoa hiyo huzalisha asilimia 97 ya pamba ya Tanzania. La pili ni Eneo la Mashariki la Uzalishaji Pamba (ECGA), linalohusisha mikoa mitatu ya Pwani, Morogoro na Tanga.Mwaka 2012 Tanzania ilizalisha tani 350,000 za mbegu za pamba, ambapo asilimia 80 ziliuzwa nje zikiwa ghafi. | uchumi |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kufungua jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji mkoani Lindi, ambalo limeanza rasmi leo mkoani humo.Hiyo ni mara ya pili jukwaa hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu. Jukwaa la nane lililofanyika mkoani Tabora, lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Jukwaa la tisa Lindi, linafanyika katika hoteli ya Sea View likitanguliwa na maonesho yatakayofanyika siku tatu mfululizo na siku ya ufunguzi kesho yanayotarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 350.Ratiba iliyotolewa na Kamati ya maandalizi ya jukwaa hilo inayoshirikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kampuni ya TSN, inaonesha mawaziri wanatarajia kushiriki jukwaa hilo pia.Mmojawao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe; anayetarajiwa kuwa Mwenyekiti wa jukwaa.Jukwaa hilo ni la nane kuandaliwa na TSN kwa kushirikiana na mikoa. Majukwaa yaliyopita yalifanyika mikoa ya Simiyu, Mwanza, Tanga, Shinyanga, Zanzibar, Arusha, Tabora na Geita.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema mkoa huo uko tayari kulipokea jukwaa hilo na wanatarajia kupata matokeo mazuri ya maendeleo ya mkoa huo kupitia jukwaa hilo.“Kwa muda mrefu tulikuwa tunataka mkoa wetu usikike, sasa hii ni fursa adhimu kwetu. Tunatarajia makubwa baada ya jukwaa hili, fursa zetu za uwekezaji na biashara zitajulikana Tanzania nzima na dunia kote,” alisisitiza.Anasema washiriki mbalimbali wa mkoa huo, watajitokeza kwa wingi. Miongoni mwao ni wajasiriamali kutoka halmashauri zote sita za mkoa huo watakaonesha bidhaa wakishirikiana na taasisi na mashirika ya umma na binafsi.Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah alisema jana maandalizi kwa TSN yanakwenda vizuri katika kuhakikisha jukwaa hilo linakwenda vizuri kama lilivyopangwa.Alisema ana uhakika jukwaa hilo litaacha alama kwa maendeleo ya mkoa wa Lindi kama ilivyokuwa katika mikoa mingine lilikofanyika.Aidha, aliipongeza timu ya waandishi wa habari wa TSN ambayo imekuwa Lindi kwa wiki tatu kwa kazi nzuri kutangaza fursa zinazopatikana huko baada ya kupita wilaya moja hadi nyingine na kuandaa toleo maalumu litakalotoka kesho.Kwa mujibu wa ratiba, wengine wanaotarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo ni wakuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa | uchumi |
SERIKALI imewasilisha bungeni Muswada wa kuanzisha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).Muswada huo pia unapendekeza makosa ya jinai na adhabu zake chini ya sheria inayopendekezwa, ambapo watumiaji maji vibaya watatozwa faini ya Sh milioni tano hadi milioni 10, huku watumiaji maji kinyume cha matumizi yaliyoidhinishwa, watatozwa Sh milioni tano au kifungo kisichopungua miezi sita. Muswada huo ulisomwa kwa mara ya pili na tatu bungeni jana na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ambao unaonesha kuwa Ruwasa pamoja na majukumu mengine, itasimamia miradi na utoaji wa huduma za maji vijijini, ikiwemo uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa.Muswada huo wenye sehemu 15, katika sehemu ya 11 inapendekeza uanzishwaji wa Ruwasa pamoja na kazi zake, hatua ambayo itaongeza ufanisi na uwajibaji katika utoaji wa huduma, kwani watalaamu wote wa maji watawajibika kwa wizara yenye dhamana ya maji. Pia, hatua hiyo itaimarisha ujenzi, usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji vijiji kutokana na kuboreshwa kwa muundo na usimamizi wa vyombo va watumiaji wa maji nchini.Muswada pia unaonesha kwamba kutakuwepo na uendelevu wa huduma za maji nchini, hivyo kuchochea utendaji katika sekta nyingine na kuongeza mchango wa sekta ya maji katika ukuaji wa uchumi. Pia muswada huo unabainisha majukumu ya watendaji au wasimamizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na jukumu la waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa, majukumu ya Sekretarieti ya Mkoa na majukumu ya Serikali za Mitaa.Muswada pia unalenga kuendelea kutambua na kuanisha majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati za Maji (EWURA). Pia unaainisha ushiriki wa jamii kwa kuruhusu uanzishwaji wa vyombo vya watumiaji maji na kuainisha masharti ya mbalimbali, yanayohusu uanzishwaji wake na masuala ya fedha. Lakini pia unaonesha kuendelea kutambuliwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa wa Maji, ambao una lengo la kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia uwekezaji katika miradi ya maji.Akitoa ufafanuzi kuhusu muswada huo, Waziri Mbarawa alisema Muswada huo ukipitishwa kuwa sheria baada ya kusainiwa na Rais, utafuta Sheria ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira namba 12 ya Mwaka 2009 Sura ya 272. “Na pia utafuta Sheria ya Huduma ya Majitaka na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) namba 20 ya Mwaka 2001 sura namba 273 ili kubaki na sheria moja ya utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira nchini,” alisema.Alisema hivyo serikali imeamua kuangalia upya mfumo wa utoaji maji nchini uliokuwa ukisimamiwa na taasisi mbili kufuta sheria za kuanzishwa kwake ili kuondoa mkanganyiko katika kutoa huduma za maji nchini. Profesa Mbarawa alisema wakati mwingine vyombo hivyo, vinakabiliwa na changamoto na kukosekana kwa watalaamu katika kusimamia miradi hiyo, na kuongeza kuwa;”ipo haja ya kuangalia upya mfumo wa utoaji maji hapa nchini.”Muswada huo umegawanyika katika sehemu 15, pamoja na mambo mengine unataka kuimarisha mfuko wa utoaji huduma ya maji nchini kwa kuanzisha Mfuko wa Uwekezaji wa Maji nchini, kama ilivyooneshwa katika Sheria ya Maji ya Mwaka 2009. Katika kifungu cha 66, muswada huo pia umebainisha adhabu kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuosha au kufua, kuoga, kutupa, kusababisha au kuruhusu kitu kuingia kwenye miundombinu ya maji, ambapo mtu atakayetenda atatozwa faini ya Sh 50,000 hadi Sh milioni 1. | kitaifa |
SERIKALI ya Finland inatarajia kutoa Euro 9.5 sawa na Sh bilioni 24/- kwa ajili ya mradi wa awamu ya pili wa Panda Miti Kibiashara.Mradi huo utakaodumu kwa miaka minne ni kwa ajili ya wakulima wadogo wa miti wa mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu aliagiza Idara ya Misitu na Nyuki ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa mradi huo kwa niaba ya Wizara, iweke utaratibu wa kusimamia na itoe taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo yake kwa wizara.Aliwataka wataalamu wote watakaotekeleza mradi huo, wafanye kazi kwa weledi mkubwa, kwa kuzingatia thamani ya fedha hiyo .Ametoa kauli hiyo Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa alipokuwa akizindua awamu ya pili ya mradi huo.Awali serikali hiyo ya Finland katika mradi wa awamu ya kwanza, kati ya mwaka 2014 hadi mwaka 2018, ilitoa Euro milioni 19.5 sawa na Sh billioni 40.Kupitia uwezeshaji huo, hekta 12,000 za miti bora zimepandwa na zinamilikiwa na wananchi wapatao 9,030.Katika awamu hiyo ya kwanza, fedha hizo zilitumika kuanzisha kituo cha mafunzo ya misitu na Kiwanda cha Misitu cha Mafinga.Kituo hicho mpaka sasa kimeshatoa mafunzo kwa wakulima wapatao 8,555. Akizungumzia lengo la matumizi ya fedha hizo za awamu ya pili ya mradi, Kanyasu alisema fedha hizo zitatumika kuwajengea uwezo wakulima wa miti na wajasiriamali wadogo na wa katiAlisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kupambana na matukio ya moto na kuongeza ubora wa mazao ya misitu yaliyo kwenye mnyororo wa thamani.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo aliishukuru Finland kwa kufadhili mradi mwingine wa kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya misitu uitwao FORVAC, unaotekelezwa na wizara katika wilaya kumi za mikoa ya Tanga, Dodoma, Lindi na Ruvuma.Alisema sekta ya misitu nchini isingefika hapa ilipo leo, kama hapangekuwepo msaada wa wananchi wa Finland. Balozi wa Finland nchini Tanzania, Riita Swan alisema nchi yake imeatoa fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo wa miti ili wajikwamue na umasikini.Kwamba Finland inataka kuona wakulima wadogo wa miti, wanajengewa mazingira mazuri ya kushiriki katika shughuli za kuendeleza misitu kibiashara. | uchumi |
WANANCHI wamehadharishwa kukabiliana na mionzi iliyopo katika simu za mkononi za kisasa kwa kuzungumza chini ya dakika tano, vinginevyo inaweza sababisha madhara mbalimbali mwilini, ikiwemo ugonjwa wa saratani.Aidha wananchi wametakiwa kuacha kuwapatia watoto kutumia simu hizo mara kwa mara kwani mionzi yake inaathiri mifumo ya ukuaji wao. Hivyo wananchi wameshauriwa wanapotumia simu zaidi ya dakika tano kutumia ‘earphone’ au kuweka ‘loudspeaker’ kuepuka madhara ya mionzi, huku wakieleza matumizi ya simu hizo ikiwa imeisha au inalalamika chaji ni hatari zaidi kwani mionzi inakuwa mikubwa.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Peter Ngamilo aliwaeleza wananchi katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwa lengo la kuwapo katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kukabiliana na mionzi katika shughuli zao za kila siku.Alisema mionzi ya simu iko katika aina ya mionzi ambayo haileti madhara ya moja kwa moja, lakini unapozungumza kwa muda mrefu inaweza kusababisha kichwa kuuma au joto la mwili kupanda huku kwa watoto wadogo ubongo bado ni teke na wako katika ukuaji hivyo kuweza kuharibu ukuaji.“Tunawashauri wazazi matumizi ya simu za mkononi hasa hizi smartphone kwa watoto siyo mazuri lakini ni vema zaidi kutumia simu hizi tunazoita za vitochi kwani ni tofauti na hizi za kisasa zenye mionzi mingi sana, kwani ina mionzi mara 1,000 zaidi ya iliyopo kwenye minara,” alisema. Alisema kwa wale wanaopenda kulala na simu kwa kuweka pembeni ya mito ni hatari kwani mionzi inakuwa kwa kasi zaidi.Alitaja madhara ya mionzi ni mengi ikiwemo ugonjwa wa saratani ya ubongo, damu au mapafu kutegemea na eneo lililopigwa na mionzi. Ngamilo alisema pia katika sekta ya afya, mionzi ina madhara kwa wanawake wenye mimba changa na wanapotaka kupiga X-Ray wawaarifu madaktari kwani mionzi itaathiri kiumbe kilichopo tumboni na kuzaa mtoto mwenye mapungufu.Alisema katika kuepuka madhara ya mionzi wananchi wanatakuwa makini na baadhi ya vyuma wanavyovikuta maeneo yao kwa kutotumia kama vyuma chakavu kwani baadhi yake vina mionzo. Aidha aliwaasa wananchi kuwa makini kwa kuangalia nembo ya mionzi yenye rangi njano na nyeusi na maandishi kuwa chanzo cha mionzi. | kitaifa |
WAKATI Simba imetinga fainali ya mashindano ya SportsPesa Super Cup, swali ni je, wameachana na makocha wao baada ya jana kuwa jukwaani wakishuhudia timu yao ikishinda kwa penalti 5-4 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru. Kocha Mkuu, Pierre Lechantre na kocha wa viungo wa timu hiyo kutoka Morocco, jana walishuhudia pambano hilo kutokea jukwaani na taarifa zilidai kuwa tayari wameachana na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wao.Hata hivyo, taarifa nyingine zilidai kuwa, Mfaransa Lechantre ametofautiana na uongozi wa Simba na hivyo hawako tayari kumuongezea mkataba mwingine, licha ya kuipatia mafanikio timu hiyo ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoukosa kwa karibu miaka mitano.Hatahivyo, hakuna kiongozi wa Simba aliyekuwa tayari kulizungumzia hilo, lakini walisema wangekuwa na kikao jana usiku na taarifa kamili wangezitoa baadae. Timu hiyo jana ilikuwa chini ya kocha msaidizi Mburundi Masoud Djuma, ambaye ndiye alipewa mikoba hiyo.Wakati huohuo, Singida United ya Tanzania jana ilitolewa katika mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kulambwa mabao 2-0 na mabingwa wa Kenya katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Afraha mjini hapa.Kwa kipigo hicho, Singida United wanaungana na mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga na JKU ya Zanzibar kuyaaga mashindano hayo baada ya kutolewa katika nusu fainali, Yanga na JKU wenyewe walitolewa katika robo fainali. Mabao yote ya Gor Mahia yalifungwa na Meddy Kagere katika kila kipindi na kuifanya timu hiyo kujihakikishia nafasi ya kucheza dhidi ya Simba katika fainali itakayopigwa Jumapili kwenye uwanja huo. | michezo |
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amewataka Watanzania kutembea kifua mbele kwa ushiriki wao wa michuano ya fainali za Kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019.Stars ipo mjini hapa kushiriki fainali za Afcon, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 39, tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980. Ilianza vibaya kwa kufungwa mabao 2-0 na Senegal katika mechi ya kwanza na jana usiku ilitarajiwa kumenyana na Kenya katika mechi ya pili. Stars ipo katika Kundi C pamoja na Kenya, Senegal na Algeria.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa juzi, Samatta anayecheza KR Genk ya Ubelgiji alisema Watanzania hawapaswi kukata tamaa na kuwa wanyonge kwa matokeo mabaya na badala yake watembee kifua mbele, kwani kufuzu peke yake fainali hizi ni jambo kubwa.“Sote ni mashahidi, imetuchukua miaka 39 toka tulipofuzu fainali za kwanza mimi naomba watanzania wenzangu watembee kifua mbele wasiwe wanyonge wapokee matokeo yoyote,” alisema.Alisema wao kama wachezaji wana mengi ya kunifunza kwenye michuano hii hivyo suala si kushiriki tu. “Wachezaji tunajifunza mengi huku. Suala sio ushiriki tu lazima ujue kufuzu fainali unajua nini na nini na unatakiwa uwe vipi,” alisema. “Kujifunza huko sio kwa wachezaji tu hata viongozi wetu naamini wamejifunza mengi...watanzania wajue fainali zina mambo mengi,” alisema.“Naona viongozi wengi wamekuja, wa mpira wa siasa yote hiyo ni kutaka kujifunza kipo watakachopata hawataondoka bure,” alisema. Aliwataka wachezaji na viongozi kuondoka na yote mazuri kwa akili ya kwenda kujifunza.“Nakuhakikishia ikitokea tumefuzu tena tutaona mabadiliko makubwa sana kwetu, na tutajitahidi kufuzu kwa sababu si tumeshaona…,” alisema huku akimaliza kwa kicheko. | michezo |
Imesema kuanzia mwezi Februari mosi mwaka huu, itaanza kutoa adhabu kwa watakaokuwa hawana mashine hizo.Imesema licha ya kuwepo kwa maandamano na migomo ya kufunga maduka kwa baadhi ya mikoa, matumizi ya mashine hizo na gharama zake ziko pale pale. Imeeleza kuwa imejipanga kuondoa kero mbalimbali zilizopo.Hayo yalitangazwa jana na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya baada ya kikao na wafanyabiashara pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda na watendaji wa TRA.Mkuya alisema baada ya kusitisha matumizi ya mashine hizo mpaka jana, kuanzia leo inatakiwa kila mfanyabiashara kununua na kuwa na kifaa hicho na kukitumia kwa ajili ya manufaa yake na Serikali.“Baada ya kuzungumza na wafanyabiashara na kusikia kilio chao, kuanzia Februari mosi ndiyo tutaanza kuchukua hatua kwa wale wasiotumia mashine hizo, hivyo tumewapa mwezi mmoja kujiandaa kwa kununua na kuanza kutumia, ”alisema Mkuya.Alisisitiza kuwa baada ya muda huo,wataanza kuchukua hatua kwa kufuata sheria kwa kuwapa siku 14 kununua mashine hizo,baadaye siku saba za mwisho kwa ajili ya matumizi hayo.Alisema siyo kweli kuwa wafanyabiashara hawataki kulipa kodi, bali kumekuwa na watu wanaopotosha kuhusu matumizi ya mashine hizo huku baadhi ya wafanyakazi wa TRA, wakiwabugudhi wafanyabiashara kwa kutumia ufahamu mdogo wa masuala hayo.“Kutokana na malalamiko hayo, nawahakikishia kuwachukulia hatua wafanyakazi hao wa TRA wanaowabughudhi wafanyabiashara,” alisema.Akizungumzia adhabu kwa wafanyabiashara watakaokiuka taratibu hizo, Kamishna wa Kodi za ndani wa TRA, Patrick Kassera alisema baada ya kumpa siku saba mfanyabiashara asiyetumia mashine hizo, watamtoza faini asilimia tano ya mauzo aliyoficha ;na ikiwa hana mashine, ina maana ni asilimia hizo za mauzo yote. | uchumi |
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwenye mchezo ujao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids atatumia mbinu mpya kwa lengo la kupata matokeo chanya tofauti na mbinu alizotumia kwenye mchezo uliopita.Zahera ametoa kauli hiyo baada ya kikosi hicho kutua salama nchini Misri kikiwa na msafara wa wachezaji 20 tayari kwa mchezo wao unatarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa 30 June jijini Cairo, Misri.Yanga katika mchezo huo wanahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo kufuatia mchezo wa awali kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Akizungumza na gazeti hili, Zahera alisema mbinu zao walizopanga kutumia zilishindwa kufanya kazi ni moja ya changamoto zilizowafanya kushindwa kupata matokeo chanya kwenye mchezo uliopita.Alisema kwenye mchezo huo kikosi chake alikipanga kucheza mchezo wa ushirikiano zaidi, huku mbele akimtumia mshambuliaji mmoja lakini mfumo huo haukufanikiwa kutokana na wachezaji wa upande wa pili kugundua mapema mtego huo.“Nikweli kwenye mchezo wa awali tulizidiwa kwenye mbinu kutokana na mfumo tuliopanga kutumia wapinzani wetu kugundua mapema. Katika mchezo wa pili na sisi tunaingia na mbinu mpya, ambazo naamini zitatunufaisha kupata matokeo mazuri, “alisema Zahera. | michezo |
Katika jukwaa hilo, washiriki kutoka makundi mbalimbali ya kijamii, wafanyabiashara ndogo na wakubwa, wawekezaji, maofisa wa serikali na wananchi watapata pia nafasi ya kukutana na maofisa wa taasisi muhimu za maendeleo na kuwauliza maswali pamoja na kuanzisha mawasiliano.Hili ni Jukwaa lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Ni jukwaa linalolenga kutoa elimu ya namna nzuri ya kuziendea fursa za uwekezaji zinazoibuliwa na kuboresha zaidi zilizopo.Baadhi ya wadau ambao washiriki watapata nafasi ya kusikia mada zinazowasilishwa katika jukwaa hilo na kuwauliza maswali huku wakijenga nao mtandao mpya ni pamoja na; Benki za NMB, TIB (Development), TIB (Corporate) na Benki TPB, Mamlaka ya Mapato (TRA), Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Wengine ni Watumishi Housing Company (WHC), Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Baraza la Biashara Tanzania, Kampuni ya Simu ya nchini (TTCL, Kampuni ya Simu ya Vodacom na Mfuko wa Pensheni wa PPF.Jana tulianza kuangazia shughuli za kiuchumi mkoani Mwanza kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tovuti ya mkoa ya www. mwanza.go.tz. Tuliona, japo kwa kifupi, hali ya kilimo na ufugaji vinavyoendeshwa mkoani hapa.Leo tunaangalia shughuli zaidi za uzalishaji ambazo wadau wake watashiriki kwenye Jukwaa la Biashara na hivyo kujiongezea maarifa zaidi pamoja na maeneo yanayofaa kwa uwekezaji mwingine.UvuviUvuvi ni moja ya shughuli kubwa inayofanyika katika Ziwa Victoria. Sekta hii ya uvuvi inachangia asilimia saba ya uchumi wa mkoa kwa mujibu wa tovuti ya mkoa. Inaelezwa kwamba shughuli za uvuvi ndizo zinazoongoza katika kuingiza fedha za kigeni katika mkoa huu. Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2011, mkoa ulikuwa na jumla ya wavuvi 52,942 huku boti na mitumbwi ikiwa 14,480.Ufugaji wa samakiUfugaji wa samaki imekuwa shughuli mpya inayoanza kuchukua nafasi yake katika siku za hivi karibuni kutokana na kupungua kwa samaki ziwani na hivyo kupunguza pia kipato kwa wavuvi. Hali hii inaelezwa kwamba imesababishwa na uvuvi wa kupita kiasi, uvuvi haramu na usimamizi mbaya wa maji ya Ziwa Victoria.Kwa kipindi cha miaka minne (2009 - 2011) mkoa ulikuwa na jumla ya mabwawa 128 ya samaki. Ni kwa msingi huo, uwekezaji zaidi katika ufugaji samaki na uvuvi endelevu ni kati ya mambo muhimu yanayohitajika sana kwa sasa.Mauzo ya samakiTakribani tani 16,913 za samaki husafirishwa kwenda katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na nchi za Mashariki ya Mbali za Japan na Australia. Jumla ya tani 426,633.50 za samaki huuzwa katika mikoa mingine ndani ya nchi na takribani tani 6,214.10 hutumika ndani ya Mwanza yenyewe. Kimsingi soko la samaki limekuwa siyo tatizo sana kama upatikanaji.Maliasili na UtaliiSekta ya rasilimali za asili nchini inajumuisha ardhi, madini, misitu, ufugaji nyuki, wanyamapori na uvuvi. Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo hazijaendelezwa kwa kiwango kikubwa, hali inayotoa fursa zaidi za uwekezaji katika kuzivuna na mafunzo.Mbali na ardhi, kuna maeneo yanayofaa kwa utalii, baadhi yakiwa tayari yana wanyamapori na mazingira yanayoweza kutumika kama vivutio vya utalii. Mkoa wa Mwanza pia unayo maeneo mengi yenye vivutio na yanayofaa kuendelezwa kwa ajili hiyo.Kama ilivyo kwa sekta nyingine, sekta zinazohusu maliasili na utalii, zinahitaji pia uwekezaji zaidi, uwe wa serikali, sekta binafsi au sekta hizi mbili kushirikiana (PPP).Ukiendelea kufuatilia makala haya katika kipindi chote cha Jukwaa la Biashara linapokuwa mkoani hapa, tutakujuza baadhi ya sekta zilizopo na mipango kambambe ya mkoa wa Mwanza katika kuendeleza sekta ya utalii ambapo sekta binafsi inahitajika sana katika kushirikiana na serikali.MadiniSekta ya madini mkoani Mwanza inaelezwa kwamba haijaendelezwa kwa kiwango cha kutosha. Kwa sasa tafiti kadhaa zinaendelea katika kugundua hifadhi za madini, shughuli ambazo zinafanywa na makampuni ya kigeni na ya ndani. Hivi sasa, kuna kiwango kidogo cha uchimbaji madini kinachofanyika katika wilaya za Misungwi, Ilemela na Nyamagana.Madini yanayovunwa ni dhahabu na yanayohusu shughuli za ujenzi. Madini haya, zaidi hununuliwa na wafanyabiashara katika jiji la Mwanza.Fursa zaidi za uwekezaji*Sekta ya afya Mkoa wa Mwanza unaokuwa kwa haraka una fursa za uwekezaji katika ujenzi wa hospitali mpya za kisasa, vituo vya afya na zahanati.Hali kadhalika, kutakuwa na fursa katika ujenzi wa viwanda vya dawa, maji maalumu yanayotumika kwa ajili ya dripu hospitalini, oksijeni zinatumika kwenye matibabu na vifaa tiba kama vile vitanda na kadhalika. Zinatakiwa pia menejimenti zinazoweza kuendesha hospitali za kisasa na uwekezaji zaidi katika huduma za bima za afya.Sekta ya elimuFursa lukuki pia zipo katika kuanzisha taasisi za elimu na mafunzo katika mkoa wa Mwanza. Mkoa umekuwa ukihimiza sana sekta binafsi kuanzisha shule na vyuo vitakavyotoa mafunzo bora katika fani za menejimenti, sayansi na teknolojia, fedha, masoko na utalii.Viwanda na BiasharaKatika miaka ya karibuni, sekta ya viwanda na biashara mkoani Mwanza imeonesha kukua kwa kasi ya asilimia 4. Sekta hii kwa sasa ni ya tatu katika kutoa mchango wake kwenye pato la mkoa na ni sekta ya tatu pia katika kuvutia mitaji ya moja kwa moja kutoka nje (FDI) baada ya kilimo na utalii.Shughuli zinazofanywa na sekta hii ni pamoja na uzalishaji bidhaa za majumbani kama usindikaji wa chakula, vinywaji, nguo na bidhaa zitokanazo na mbao. Mkoa wa Mwanza una uwezo wa kutoa malighafi nyingi na zenye ubora. Malighafi hizo ni zinazotokana na kilimo na mifugo, pia madini na uvuvi.Kuna fursa kubwa mkoani Mwanza za uanzishwaji wa viwanda vikubwa kama vya kemikali (chemical industries), chakula, vinywaji, nguo, ngozi, metali na kadhalika. Je, kesho nini kitamulikwa katika mkoa wa Mwanza? Fuatilia zaidi. | uchumi |
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema kutokana na juhudi kubwa za serikali za kuimarisha uchumi, ukusanyaji wa mapato umeongezeka na kwamba kwa mwaka 2017/18 serikali ilikusanya Sh bilioni 688.7 ikilinganishwa na Sh bilioni 521.8 zilizokusanywa na taasisi za ukusanyaji kodi kwa mwaka 2016/17.Taasisi zinazokusanya kodi kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni mamlaka ya mapato ya Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).Akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika katika Uwanja wa Gombani, Chakechake kisiwani Pemba jana kuhitimisha kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi, Dk Shein alisema kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi imefikia asilimia 7.7 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 5.8 kwa mwaka 2016.Kadhalika alisema pato la mtu binafsi liliongezeka na kufikia Sh milioni 2.1 sawa na dola za Marekani 944 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na Sh milioni 1.89 sawa na dola za Marekani 868 kwa mwaka 2016, huku mfumuko wa bei ukiendelea kudhibitiwa katika tarakimu moja.Kwa mwaka 2018 kasi ya mfumuko wa bei ilifikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 5.6 katika mwaka 2017.Utegemezi Aidha, Dk Shein alisema kwamba mafanikio ya ukuaji wa uchumi kumeifanya serikali yake kupunguza hali ya utegemezi wa bajeti ambao kwa sasa umefikia asilimia 5.1 kwa mwaka 2018/20219 ikilinganishwa na utegemezi wa asilimia 7.3 kwa mwaka 2017/18.“Wakati serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya saba inaingia madarakani mwaka 2010/11 kiwango cha utegemezi kilikuwa ni asilimia 30.2,” alisema Dk Shein na kuongeza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi mbalimbali za serikali ikiwemo kuwashajiisha wazalishaji wa ndani na kuweka mazingira mazuri ya biashara katika uagizaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya Zanzibar.Aidha alisema kwamba serikali yake imeendelea kuimarisha sekta ya viwanda na mchango wake katika pato la taifa umefikia shilingi bilioni 631.6 sawa na asilimia 19.6 kwa mwaka 2017, kutoka shilingi bilioni 528.6 mwaka 2016 sawa na asilimia 19.2 na kuongeza kuwa hilo limechangiwa na kuimarika kwa viwanda mbalimbali vilivyopo Zanzibar.Kwa upande wa biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, alisema jumla ya bidhaa zenye thamani ya Sh bilioni 17.21 zilisafirishwa kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara na bidhaa zenye thamani ya Sh bilioni 232.59 zilisafirishwa kutoka Tanzania Bara kuja Zanzibar.Uinuaji wa pato la watuKatika kuinua pato la mtu mmoja mmoja, Rais Shein alisema kwamba kwa miaka saba mfululizo serikali yake imeendelea kutekeleza sera yake ya kumlipa mkulima kiwango cha asilimia 80 ya bei ya karafuu katika soko la dunia ambayo ni sawa n ash 14,000 kwa kilogramu moja.Hata hivyo, alisema kwamba jumla ya tani 7,464 za karafuu zenye thamani ya Sh bilioni 131.955 zimeuzwa nje ya nchi kwa mwaka 2017/18 ikilinganishwa na tani 2,253 za karafuu zenye thamani ya Sh bilioni 38 zilizouzwa mwaka 2016/17.Pia alisema lipo ongezeko la pato kutokana na utalii kuongezeka kwa idadi yao kila mwaka na kuwa kwa mwaka 2018 jumla ya watalii 520,809 waliwasili nchini ukilinganisha na watalii 433,116 waliwasili mwaka 2017.Aidha alisema wataendelea na kujitangaza pamoja na kufanya maonesho kila mwaka ya utalii ili kuvutia watalii zaidi.Akizungumzia mafanikio mengine mengi ya mapinduzi alisema kwamba serikali yake imeyaishi malengo ya mapinduzi kwa kusogeza huduma nzuri na bora kwa wananchi.Huduma hizo ni katika sekta ya maji, elimu, uchukuzi na utetezi wa wanyonge hasa watoto na wanawake.ElimuAlisema katika hotuba yake hiyo kwamba miongoni mwa malengo makuu ya mapinduzi yalikuwa ni kuwapa elimu bila malipo na yenye manufaa wananchi wake kwa ajili ya maisha yao na kwamba katika kipindi cha miaka 55 ya mapinduzi yamepatikana mafanikio makubwa sana na kuimarika kwa huduma za elimu.“Kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964 huduma hizo zilikuwa chache na zikitolewa kwa ubaguzi na wachache waliopata fursa ya elimu, walilazimika elimu hiyo wailipie” alisema na kuongeza kwa idadi ya shule zilikuwa chache lakini kwa sasa zipo nyingi na elimu inatolewa bure toka awali msingi hadi sekondari na wale wanoafika chuo kikuu wanasomeshwa kwa mkopo.Alisema siku za maandalizi zimeongezeka kwa mara 272 zenye wanafunzi 72,151 kwa mwaka 2018 ukilinganisha na skuli mbili zilizokujwa na wanafunzi 60 kwa mwaka 1963.Upande wa sekoindrai nao umeongezeka mara 67 kufikia junmla ya shule 268 zenye idadi ya wanafunzi 126,913 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na skuli 4 zilizokuwa na idadi ya wanafunzi 734 kwa mwaka1963.AfyaAlisema serikali inaendelea na uamuzi wake ilioutoa Machi 3,1965 wa kuwapa wananchi matibabu bure na huduma zake zinaendelea kuimrishwa kwa kuajiri wataalamu zaidi, kujenga hospitali kupandisha hadhi zilizopo na kuhakikishakwamba wahudumu wanakuwa na nafasi ya kusikiliza wagonjwa wao kwa kupunguza kiwango cha uwiano kati ya wahudumu na wagonjwa.Rais Shein alisema kutokana na juhudi hizo kiwango cha malaria kimepungua na kubaki asilimia 0.4 mwaka 2018.Pamoja na mafanikio alisema kwamba taifa hilo linachangamoto ya maradhi yanayoambatana na kuimarika kwa uchumi wa wananchi kama kisukari,maradhi ya moyo ambayo mengi yanatokana na kubadilika kw atabia za ulaji.Kuhusu tatizo la dawa alisema litaisha kwa sababu wametanua bajeti ya wizara ya afya kwa kutenga Sh bilioni 12.7 ikilinganishwa na Sh bilioni 7.0 mwaka 2017/18.MajiDk Shein amesema kwamba ni jambo la kufurahishwa kwamba hivi sasa vijiji mbalimbali vya mkoa wa Kaskazini Unguja vinaendelea kupata maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliotekelezwa na kampuni ya First Highway Engneering of China ; huku upande wa pemba huduma za maji safi na salama zinapatikana kw akiwango cha kuridhisha.Kilimo Katika kuimarisha kilimo cha umwagiliaji cha mpunga, miundombinu ya umwagiliaji katika hekta 1,524 kwenye bonde la Cheju, Bumbwisudi na Kibokwa kwa Unguja na bonde la Makwararani na Chamanangwe kwa Pemba zitajengwa na mkandarasi kutoka Korea na mkataba umeshatiwa saini.Aidha mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo utakaogharimu dola za Marekani milioni 148 utaketelezwa kwa muda wa miaka 10 kwa v ipindi viwili vya miaka mitatu mitatu na kipindi kimoja cha miaka mine.MiundombinuAlisema serikali inaendelea na ujenzi wa barabara kuu na barabara za ndani unguja na Pemba. Alisema kuwa baadhi ya bara zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa huku zingine zikitafitiwa fedha.Pia alisema kwamba juhudi zinaendelea kuhakikisha kwamba ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume unakamilika na fedha za kujenga bandari mpya ya Mpigaduri zinapatikana na ujenzi unaanza mwaka huu.Uwezeshaji Aidha alisema serikali yake inaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumni na kupambana na tatizo la ajira na kuongeza kuwa mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi utaendelea kuimarishwa ili kutoa mikopo zaidi kwa wananchi.Kwa mwaka 2018 alisema mikopo 451 yenye thamani ya Sh milioni 685 imetolewa kwa wajasiriamali wa Unguja na Pemba. | kitaifa |
Kituo hicho kilichoko eneo la Kabanga nchini na Kobero nchini Burundi, kitasaidia uvukaji wa abiria na usafirishaji wa bidhaa.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastina Justinian alisema hayo jana katika Maonesho ya 38 Biashara ya Kimataifa.Alisema matumizi ya vituo hivyo vya pamoja, yatafanya msafiri kukaguliwa sehemu moja ya anakoelekea, huku idara zote zikiwa katika jengo moja.“Kuanza kwa kituo hiki, kutasaidia katika kuweza kuangalia changamoto mbalimbali zitakazojitokeza ili kuzifanyia kazi, ingawa hatutegemei changamoto kubwa kutokana na kuwa mfumo huu wa vituo vya pamoja unafanyika katika nchi nyingi,” alisema.Justinian alisema vituo vingine vya pamoja vya Holili/Taveta, Sirari /Isebania, Namanga, Rusumo, Horohoro/Lungalunga vimefikia katika hatua mbalimbali kukamilika.Vingine ambavyo haviko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kama Tunduma/Nakonde mpakani mwa Zambia, Kasumulu/Songwe mpakani na Malawi na Mtambaswala mpakani na Msumbiji, vinatarajia kuanza kujengwa mwaka huu.Alisema vituo hivyo vya pamoja, vitadhibiti na kuboresha utoaji huduma za kiforodha na uhamiaji kwa ushirikiano na ufanisi zaidi, hivyo kukuza biashara, uwekezaji, uzalishaji na usafirishaji. | uchumi |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka vijana mkoani humo kuchangamkia fursa zinazotokana katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ili kuinua maisha yao kwa kuwa kuna soko la uhakika la bidhaa hiyo.“Wakati umefika kwa vijana badala ya kulalamika kuhusu ajira, wangejikita kwenye ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ambao ni mkombozi mkubwa na hasa katika kuinua kipato. Soko la uhakika la maziwa lipo lakini uzalishaji ni mdogo,” amesema Chalamila.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Chalamila alisema sekta ya ufugaji wa ng’ombe imekuwa na uhitaji mkubwa wa maziwa kupitia viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za maziwa kikiwemo kiwanda cha Asas Dairies Limited cha mkoani Iringa.Amesema kiwanda kinazalisha chini ya uwezo wake kutokana na uhaba wa maziwa. Na kwamba ni fursa kwa vijana kujikita katika ufugaji na kubadilisha maisha yao.“Kampuni ya Asas inanunua maziwa katika wilaya za Rungwe na Busokelo mkoani hapa. Vijana wengi wamefanikiwa katika maisha yao kupitia ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini bado maziwa hayatoshi,” amesema.Amesema fursa kama hiyo ikichangamkiwa itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana walio wengi mkoani hapa na mikoa ya jirani tayari wameshapata mafanikio makubwa kupitia ufugaji.“Kampuni ya maziwa ya Asas imesongeza huduma kwa wafugaji ikiwemo kutoa elimu ya namna bora ya kufuga ng’ombe wachache wa maziwa ambao watawaletea faida kubwa kutoka na uzalishaji wa maziwa kwa wingi,” amesema Chalamila.Amesema, kampuni hiyo imeweka vituo vya kukusanya maziwa kutoka kwa wafugaji katika wilaya ya Rungwe na halmashauri ya Busokelo ili kumsaidia mfugaji kutopoteza maziwa yake na pia kiwanda kipate maziwa yatakayokwenda kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana na maziwa.“Nina taarifa kuwa Asas imepeleka madume ya ng’ombe manne Rungwe kwa lengo la kuendeleza kizazi cha ng’ombe bora wa maziwa ili kuongezeka uzalishaji wa maziwa,” amesema Chalamila.Aliongezea kuwa hilo limefanyika kutokana na uhitaji mkubwa wa maziwa kiwanda cha Asas na hivyo kuhamasisha watu kujikita katika sekta ya ufugaji.Ajira nyingi zimeweza kutengenezwa kupitia ufugaji.“Jitihada hizi zinaonesha uzalendo wa dhati alionao mwekezaji huyo katika kumsaidia mfugaji kuongeza kipato kupitia maziwa. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inahamasisha uwekezaji kwenye lengo la kumwinua Mtanzania wa kawaida,” alisisitiza.Mratibu wa Kitaifa wa Asas Dairies, Lipita Mtimila amesema, kiwanda bado kinahitaji maziwa kutoka kwa wafugaji, kwani uhitaji wa bidhaa zinazotokana na maziwa ni mkubwa hivyo ni muhimu kuhamasisha wakulima kufuga ng’ombe wachache watakaoweza kuwahudumia.“Sisi kama Asas Dairies tutaendelea kutoa huduma kwa wafugaji ili kuongeza uzalishaji maziwa kwa wingi na yenye ubora unaohitajika kiwandani,” alisema Mtimila na kuongeza kuwa jamii ya wafugaji katika mnyororo wa thamani ya maziwa wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa. | uchumi |
SIKU chache baada ya uongozi wa Simba SC kumsimamisha kazi kwa muda kocha wao mkuu, Patrick Aussems na timu kukabidhiwa kocha msaidizi, Denis Kitambi, kocha huyo amefunguka kuwa timu itaendelea na makali yake yale yale.Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba umemsimamisha kazi Aussems kwa muda huku ukipanga leo kufanya kikao cha kumjadili na kutoa uamuzi wa kuendelea na kibarua chake au kumtupia virago.Akizungumza juu ya kukabidhiwa timu, Kitambi alisema kuwa nafasi hiyo aliyopewa na uongozi hataki kuichezea, hivyo atakachofanya ni kuipa timu mafanikio ili kuwadhihirishia Wanasimba kuwa anaimudu vilivyo. Alisema kuwa baada ya kupewa jukumu la kuisimamia timu, kazi ya kwanza aliyoifanya ni kuandaa programu ya wiki nzima, ambayo anaamini itamsaidia katika kuiandaa timu na tayari ameanza kuitumia.Alisisitiza kuwa licha ya timu kupitia mabadiliko hayo lakini hakuna kitakachobadilika na malengo ya kuutetea ubingwa wao, yako palepale na anaamini wana uwezo wa kufanya hivyo.“Bado tunaendelea na mazoezi japo ni mageni kwao huwezi kuwapa na waende nayo moja kwa moja, lakini kidogo kidogo watayazoea, nimetakiwa kusimamia timu na tayari nimeshaandaa programu ya wiki.“Mkurugenzi Mtendaji aliniita ofisini kwake na kuniambia Kocha Mkuu tumemsimamisha mpaka pale tupakuwa na kikao naye tarehe 28 (leo) kwa hiyo kwa sasa wewe uisimamie timu kwa wiki nzima.“Kwa sasa tuwe na subira tusubiri maamuzi yatakayotoka, baada ya kuniambia niisimamie timu wao wameniamini na mimi nataka kudhihirisha kuwa nina uwezo wa kufanya hivyo, hakuna kitakachoharibika,” alisema Kitambi. | michezo |
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars sasa ina kazi nzito ya kupindua matokeo katika mechi ya marudiano dhidi ya Sudan baada ya jana kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan ilikuwa ya vuta nikuvute na Stars itabidi ijilaumu kwani ilikuwa vizuri zaidi kipindi cha kwanza lakini ikashindwa kutumia nafasi ilizopata. Stars ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Sudan, lakini umaliziaji ulikuwa mbovu kwa ama washambuliaji kutokuwa makini kulenga lango ama kupokwa mpira na wapinzani. Shaaban Nado alikosa bao dakika ya 17 na 18 akiwa ametengenezewa pasi safi na Mzamiru Yassin lakini lakini akashindwa kumalizia huku kipa wa Sudan akiwa hayupo langoni mwake. Sudan ilikianza kipindi cha pili kwa kasi na kupata bao dakika ya 62 kupitia kwa mchezaji wake Ahmed Adam kwa mkwaju hafifu baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Stars.Matokeo hayo yanaiweka Stars pabaya kwani sasa ugenini itabidi apate ushindi kuanzia mabao mawili ili kujiweka sawa, ikitokea ameshinda bao moja, basi watapigiana matuta. Mshindi wa mechi hiyo atafuzu fainali za Chan mwakani zitakazofanyika Cameroon. | michezo |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Mkoa wa Tabora unafaa kwa uwekezaji kwa kuwa una fursa nyingi na upo tayari kupokea wawekezaji.Amesema, anaufahamu vizuri mkoa huo wenye fursa nyingi zikiwemo za kwenye sekta ya kilimo, mifugo, ufugaji wa nyuki, huduma zikiwemo za hoteli, benki, mawasiliano na biashara kwa ujumla.Majaliwa ameyasema hayo leo mjini Tabora wakati anafungua Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoa wa Tabora. Jukwaa hilo la nane la fursa za biashara limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa huo.“Kuwekeza Mkoa wa Tabora unajihakikishia na usalama wako kwa sababu usalama wa mkoa huu ni mkubwa na ni hii ni sababu ya kazi kubwa inayofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na wananchi wake”amesema Majaliwa.Amesema Tabora inafikika kwa barabara za lami, ndege, reli zinazokwenda Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo mwekezaji anaweza kufika kwa urahisi mkoani humo kufanya shughuli zake.“Kwa maana hiyo Tabora inafikika na inafaa kuwekeza kwa sababu unafika na kurudi kwa haraka zaidi. Lakini Tabora ni mkoa wenye ardhi nzuri yenye rutuba, na una ardhi ya kutosha. Mpaka sasa ardhi tuliyoitumia ni asilimia hamsini tu, bado tuna asilimia 50, hii peke yake inatoa fursa kwa mwekezaji yeyote kuja kuwekeza kwenye sekta ya ardhi” amesema.Majaliwa amesema, yeyote anayehitaji ardhi Tabora kwa ajili ya kilimo au kujenga kiwanda atapata, na kwamba, wilaya zote saba mkoani humo zimetenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji.“Kwa hiyo nawakaribisha nyote kuja kuwekeza, ardhi ipo na mtapata hati. Pia tuna hali ya hewa nzuri mkoani Tabora. Baridi kidogo nyakati za usiku, mchana joto kidogo lisilotoa jasho, na hali ya hewa hii inakwenda sambamba na mazao yanayozalishwa mkoani Tabora”amesema.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kila wilaya mkoani Tabora imejiandaa kukaribisha na kupokea wawekezaji ili fursa zilizopo zitumike kwa manufaa ya wananchi, wilaya husika, mkoa na Taifa kwa ujumla.“Lakini pia Tabora inatosha kuwekeza kwa sababu ina nishati ya umeme. Wakati Serikali inaongeza uzalishaji wa umeme na kuingiza kwenye gridi, Tabora na wilaya zake zote zimepitiwa na gridi ya Taifa ya umeme. Kwa hiyo uwekezaji Tabora unatosha, uwekezaji Tabora unafaa, uwekezaji Tabora ni mahali pake” amesema.Majaliwa pia amesema, Tabora pia ipo vizuri kwenye sekta za elimu kwa kuwa na shule za vyuo, ina huduma nzuri za kiafya ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa, hospitali za wilaya, na vituo vya afya, kuna huduma ya maji na inaboreshwa kwa kufikisha maji kutoka Ziwa Viktoria.Amesema, Tabora pia ni mahali sahihi kuwekeza kwa kuwa unajitosheleza kwa chakula, na yanalimwa mazao karibu yote ya chakula na biashara yakiwemo mahindi, pamba, karanga, tumbaku, alizeti, mpunga na sasa kimeanza kilimo cha korosho wilayani Uyui.“Tabora pia kuna wafugaji, nyama zinapatikana, hatuagizi nyama kutoka nje ya Tabora, zinapatikana hapa hapa Tabora” amesema na kuongeza kuwa, Tabora pia kuna samaki na mkoa huo ni jirani na maziwa makubwa ya Viktoria na Tanganyika ambako kitoweo hicho kinapatikana kwa wingi.Majaliwa amesema Tabora kuna fursa ya kuwekeza kwenye sekta ya madini, sekta za fedha zikiwemo benki na kwamba, Serikali itafungua tawi la Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) mkoani humo.Amesema kupita kwa bomba la mafuta linalotoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa hoteli, kumbi za mikutano, maeneo ya starehe ni fursa kubwa mkoani Tabora hivyo wawekezaji wa aina zote wanaweza kwenda kuzitumia. | uchumi |
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa anatoa mwendelezo wa taarifa za kifedha za benki hiyo kwa vyombo vya habari.Aidha, Bussemaker alisema kumekuwepo sababu mbalimbali za ongezeko hilo kuwa dogo miongoni mwake ikiwa ni kulegalega kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani na hivyo kukuza gharama za ununuzi. Pia amana za wateja zimeongezeka kwa kasi ndogo.Alisema hatua hiyo inafanya NMB kupata faida ya Sh bilioni 77 hadi Juni mwaka huu baada ya makato ya kodi. Hata hivyo alisema faida hiyo inaifanya benki hiyo kuwa katika mazingira salama katika biashara ya fedha nchini.“Nusu ya pili kwenda hadi Desemba tunategemea hali ya biashara kuwa nzuri kwani zipo jitihada mbalimbali zinafanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika kuimarisha thamani ya Shilingi.” “… lakini pia tunaamini mchakato wa uchaguzi mkuu utakuwa wa amani na utulivu na hivyo mazingira ya biashara yatakuwa bora,” alisema Bussemaker.Akizungumzia mizania ya benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema inaendelea vizuri kutokana na kuwepo kwa asilimia 2.8 tu ya mikopo isiyolipika, kutoka katika mikopo yenye thamani ya Sh trilioni 2.3 iliyotolewa na benki hiyo hadi sasa, huku wastani wa usalama wa benki kwa mikopo isiyolipika ikiwa ni asilimia sita.Kwa upande wa mali za benki hiyo, Mkurugenzi huyo anajigamba kuendelea kuwa salama hatua iliyowezesha pia ukarabati wa matawi 100 ya benki hiyo kwa gharama ya Sh bilioni 60.Alisema uwiano wa uwekezaji katika ukarabati wa matawi hayo pamoja na ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la Makao Makuu mapya ya NMB jijini Dar es Salaam, ukifikia wastani wa asilimia 53.“Kwa upande wa mtaji, ipo vizuri sana. Biashara ya benki ipo vizuri, tukiwa pia na mawakala 200 wanaoendesha biashara zetu kwa nchi nzima. Pia tupo katika utaratibu wa kubadili kadi zetu ili wateja waweze kutumia kadi za kisasa zaidi zinazokwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia za kadi za Master,” alisema. | uchumi |
Kamala alisema hayo alipozungumza katika mkutano uliowakutanisha wawekezaji kutoka Ubelgiji, Ugiriki na Italia mjini hapa, ukiwa na lengo la kuitangaza Zanzibar katika utalii na uwekezaji.Alisema mhimili mmoja wa utalii ni kuimarika kwa amani na utulivu na kwa sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa chini ya uongozi wa Rais Dk Ali Mohamed Shein.“Mkutano huu unawakutanisha wawekezaji kutoka nchi za Ulaya, Ubelgiji pamoja na Italia na kipaumbele ni uwekezaji na mazingira yaliopo Zanzibar kwa sasa ni rafiki,” alisema.Alisema kazi kubwa inayotakiwa kufanywa kwa sasa ni kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini vitakavyotoa fursa nzuri kwa wawekezaji.Awali Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Khamis Mussa, alisema Zanzibar imeunganishwa na miundo mbinu yote ikiwemo inayokwenda vijijini.Alisema barabara zote za vijijini zimejengwa kwa kiwango cha lami pamoja na kuwepo huduma ya umeme ambao unatosheleza kwa mahitaji ya sekta ya uwekezaji.“Zanzibar imejiweka tayari kwa ajili ya uwekezaji baada ya kuimarisha miundombinu ya barabara na nishati ya umeme baada ya kukamilika kwa mradi wa Changamoto za Milenium,” alisema.Alisema mradi wa umeme wa changamoto za milenium uliofadhiliwa na Serikali ya Marekani kwa kiasi kikubwa unaiwezesha Zanzibar kuzalisha jumla ya megawati mia moja za umeme.Wawekezaji hao wapo nchini baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Ubelgiji pamoja na jumuiya ya Ulaya. | uchumi |
Hali hiyo inatokana na wakulima hao kushindwa kulipa deni kwa zaidi ya miaka miwili, kinyume na makubaliano ya mkataba.Mwanasheria wa ZSTC, Ali Hilali Vuai alisema kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya wakulima na uongozi wa shirika hilo, wanatakiwa kulipa mikopo hiyo katika kipindi cha miezi mitatu.Alisema juhudi za kuwataka wakulima hao, kulipa madeni hayo kwa sasa zimeshindikana na uongozi wa shirika unatarajia kunadi mali za wakulima waliokopa mikopo hiyo.“Mikataba ya wakulima waliokopa fedha kutoka ZSTC ipo wazi kama wakishindwa kulipa basi ni kuchukua mali zao na kuzinadi kwa ajili ya kupata fedha tunazowadai,” alisema.ZSTC imetoa mikopo zaidi ya Sh milioni 60 kwa wakulima wa karafuu katika kisiwa cha Pemba, kuimarisha kilimo cha zao hilo.Fedha hizo ni za kusafisha mashamba ya karafuu na kupanda mikarafuu mipya, kuchukua nafasi ya mikarafuu iliyozeeka, ambayo kwa sasa haina uzao tena.Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba, Jabu Khamis Mbwana alisema agizo la rais wa Zanzibar, linawataka kufuatilia kwa karibu zaidi, kujua hatma ya wakulima waliochukua fedha ZSTC, ambao hawajarudisha deni hilo hadi sasa.Alisema wakulima ambao wameshindwa kulipa mikopo waliyopewa na ZSTC, watashtakiwa na mali zao kunadiwa kulipa fidia na kurudisha fedha hizo.Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis alisema wakulima waliochukua mikopo ZSTC, wanalazimika kulipa deni hilo kwani aliyekopa anatakiwa kulipa.ZSTC katika miaka ya 1995, lilipata hasara zaidi ya Sh milioni 360 ambazo zilitolewa kuimarisha mashamba ya karafuu kwa wakulima, ambazo hazikurudishwa tena. | uchumi |
HASSAN Dilunga jana aliamua matokeo na kuipa timu yake ya Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Dilunga aliyeingia dakika ya 28 kuchukua nafasi ya nahodha John Bocco aliyetoka kutokana na kuumia baada ya mechi hiyo aliwataka mashabiki wa Simba kushusha presha kwani wao (wachezaji) wanajua kitu gani kinahitajika kutetea ubingwa wao. Alifunga bao hilo kwenye dakika za nyongeza katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Elly Sasii ambapo aliunganisha vema pasi ya Emmanuel Okwi. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 72 na sasa ana safari ya Mbeya ambapo atacheza na Prisons na Mbeya City.Katika mechi ya jana, Simba ilionekana kutawala vipindi vyote huku washambuliaji wake wakiongozwa na Okwi wakifanya mashambulizi mengi langoni mwa wapinzani wao lakini safu ya ulinzi ya JKT ilikuwa imara kuzuia mashambulizi ama wakati mwingine mashuti ya wachezaji wa Simba yalitoka nje ama kupaa juu. Okwi alikosa mabao kadhaa kwa Simba jana hasa katika dakika ya tisa, 69, 76 ambapo ama alipiga pembeni au alipaisha juu ya lango.Aidha Meddie Kagere pia alikosa bao dakika ya 56 akiachia shuti lililogonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa JKT Tanzania. JKT ilimaliza mechi hiyo pungufu baada ya mwamuzi Sasii kumwonyesha kadi nyekundu Anuari Kilemile katika dakika ya 75 kwa kumchezea madhambi Clatous Chama.Mechi nyingine ya Ligi Kuu jana ilichezwa Mara ambapo Biashara ya huko ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Lipuli. Matokeo hayo yanaifanya Biashara kujiondoa kwenye ukanda wa kushuka daraja na sasa kazi imebaki kwenye jitihada za kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi zilizosalia ili isirudi tena chini. | michezo |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inautegemea mkoa wa Pwani kwa uwekezaji.Ameyasema hayo leo mjini Kibaha wakati anafungua Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani.Amesema, Mkoa wa Pwani upo mbele katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuleta maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi kupitia uwekezaji na hasa kwa kujenga viwanda.“Nimefurahishwa pia na kauli mbiu ya kongamano hilo ambayo inasema Ijenge Tanzania, Wekeza Pwani Mahali Sahihi kwa Uwekezaji…kauli mbiu hii kwa mtazamo wangu ina maana kubwa, licha ya mkoa wa Pwani kubainisha na kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo, mkoa huu unajipambanua vizuri sana kwa kuonyesha ni kwa namna gani umejiandaa kwa kutengeneza mazingira mazuri kwa uwekezaji “amesema.Majaliwa amesema kauli mbiu hiyo inasadifu azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda, na kwamba, mkoa wa Pwani una fursa nyingi hivyo zikisimamiwa na kuendelezwa vizuri zinaweza kuwa na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.“Kauli mbiu hii inaweka wazi dhamira ya dhati ya mkoa wa Pwani ya kuondoa vikwazo vyote vya uwekezaji na biashara kwa wawekezaji wetu, vilevile inatoa uhakika kwa wawekezaji wote waliopo hapa na waliopo nje na ambao wanatarajia kuja kwamba Pwani ni mkoa salama na ni mahali sahihi kwa uwekezaji”amesema.Amesema, Rais John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wana matarajio makubwa na kongamano hilo linalofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.Ameupongeza mkoa huo kuwa kujenga viwanda vingi na kuandaa kongamano linalowakutanisha wawekezaji, viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali na taasisi wezeshi.Miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji, Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, wakuu wa taasisi binafsi za umma na wawekezaji. | uchumi |